Barabara ya Kilwa kipande cha Mzinga Kongowe kinatumaliza

othiambo

JF-Expert Member
Nov 15, 2014
1,983
2,770
Wasalaam wakuu, mpaka muda huu nina huzuni ya nafsi baada ya kuiona maiti ya bajaji iliyogongwa na roli la cement mzinga, njia ile wallah finyu barabara ni mbovu, vyombo vinavyopita pale ni vyenye uzito wa hali ya juu kuliko ubora wa barabara malori ni mengi maswali yamenijaa kichwani najiuliza serikali inamikakati gani na kipande kile kidogo?
 
Wasalaam wakuu, mpaka muda huu nina huzuni ya nafsi baada ya kuiona maiti ya bajaji iliyogongwa na roli la cement mzinga, njia ile wallah finyu barabara ni mbovu,vyombo vinavyopita pale ni vyenye uzito wa hali ya juukuliko ubora wa barabara malori ni mengi maswali yamenijaa kichwani najiuliza serikali inamikakati gani na kipande kile kidogo?
Barabara yote ya kusini yani Kilwa - Lindi - Mtwara ni mbovu mno inamaliza watu kila siku na serikali ipo kimya
 
, vyombo vinavyopita pale ni vyenye uzito wa hali ya juu kuliko ubora wa barabara malori ni mengi

Nafikiri barabara zote kubwa kama Bagamoyo Road, Kilwa Road, Morogoro Road, Mandela Express, Sam Nujoma jijini Dar es Salaam na barabara za aina hiyo katika majiji ya Mwanza, Mbeya, Iringa n.k hazifai kutumiwa na bajaji, bodaboda kufanya usafirishaji abiria.

Hata zile barabara za kuunganisha mikoa au nchi na nchi vyombo hivi vidogo vopigwe marufuku kutumia highways, barabara kuu. Vyombo hivyo vidogo viruhusiwe kupokea abiria kutoka barabara kuu kuingia mitaani na vijijini tu.

Vyombo hivyo vidogo vipangiwe barabara ndogo za michepuko mitaani lakini barabara kuu ziachiwe malori, mabasi, magari madogo ya binafsi, teksi, mabasi ya mwendokasi na daladala kubwa tu.

Hii ya kulazimisha vyombo vidogo kama bajaji, bodaboda kuingia katika barabara kuu ni hatari na vurugu.
 
Hawawezi kujua shida zetu kama bado tunajaa kwenye mikutano Yao na kuwaomba watuongoze tena huku tukiwaambia wamefanya makubwa mno.
 
Nafikiri barabara zote kubwa kama Bagamoyo Road, Kilwa Road, Morogoro Road, Mandela Express, Sam Nujoma jijini Dar es Salaam na barabara za aina hiyo katika majiji ya Mwanza, Mbeya, Iringa n.k hazifai kutumiwa na bajaji, bodaboda kufanya usafirishaji abiria.

Hata zile barabara za kuunganisha mikoa au nchi na nchi vyombo hivi vidogo vopigwe marufuku kutumia highways, barabara kuu. Vyombo hivyo vidogo viruhusiwe kupokea abiria kutoka barabara kuu kuingia mitaani na vijijini tu.

Vyombo hivyo vidogo vipangiwe barabara ndogo za michepuko mitaani lakini barabara kuu ziachiwe malori, mabasi, magari madogo ya binafsi, teksi, mabasi ya mwendokasi na daladala kubwa tu.

Hii ya kulazimisha vyombo vidogo kama bajaji, bodaboda kuingia katika barabara kuu ni hatari na vurugu.
Kweli kabisa mkuu
 
Nakubaliana na mtoa post, pointi ya msingi na iliyowazi. SERIKALI imefanya mambo mazuri mengi mengi sana ya maendeleo hususani ujenzi wa barabara.

Jiji la Dar es Salaam, kwa kiasi kikubwa limefunguka kwa barabara kuu karibu kila upande na kulipendezesha. ISIPOKUWA huu upande wa kusini.

Ni OMBI kwa wahusika siyo mpaka Mama AONE, jiongezeni na nyinyi ongezeni msukumo wa ujenzi wa barabara kutoka ROUNDABOUT pale Rangi tatu kwenda CHANIKA . VILEVILE kutoka pale kuelekea MKURANGA.

Pia kupiga kona kuelekea FERRY, Wahusika jitahidini mtekeleze hayo mtalifanya mpaka jiji LIPUMUE eneo la Mkuranga litajengeka na kufumua fursa mpya. Mbagala mpaka CHANIKA kuzunguka jiji PATAPENDEZA SANA.
 
NISHAWAI KUANDIKA HAPA KUHUSU ILE BARABARA KWANZA NI NDOGO IKISHAFIKA SAA KUMI TU FOLENI ALAFU KULE NJIA YA MKURANGA KUMEKUWA KWA KASI VIKINDU NA KISEMVULE KWAHIYO WATU NI WENGI SANA. GARI NDIO USISEME LAKIN NJIA NDIO CHANGAMOTO
WAZOEFU WANASEMA SERIKALI INAOGOPA ZILE GHARAMA ZA DARAJA LA MZINGA PALE KWENYE KULITANUA.

KIUFUPI JJIA YA KUSINI IMESAHAULIKA
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom