MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,643
- 33,439
Wakuu,
Kama wengi tulivyoshuhudia na mitandao mingi inavyoripoti hali ya mafuriko ni mbaya na athari kubwa ni barabara na madaraja kuharibika vibaya kiasi ya njia nyingi kufungwa kwa tahadhari.
Kama tunavyofahamu, tumepata mvua mfululizo na inawezekana matokeo ya leo si sababu ya mvua iliyonyesha leo bali uharibifu kufanyika kidogo kidogo.
Ni vizuri mamlaka zetu ziweke utaratibu wa kukagua barabara na hasa madaraja kuona ustahimivu wake kadri mvua zinaponyesha ili kama kuna athari zilizoanza zirekebishwe kabla ya matokeo makubwa zaidi.
Tanroads na mamlaka zingine ni vizuri wawe wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara utasaidia sana kuimarisha madaraja yetu ambayo wakati mwingine yanaharibika kidogo kidogo kabla ya kushindwa kabisa kuhimili mvua kubwa.
Janga halipigi hodi lakini ukaguzi na ukarabati kila baada ya mvua kubwa ingepunguza athari tunazoona zimetokeo leo maeneo mengi.
Sasa ni wito kwa serikali kufanya ukaguzi mkubwa haraka kabla mvua nyingine kubwa haijasomba barabara na madaraja yaliyosalia tukaingia hasara kubwa.