Barabara kuu ziwe MERIT GOODS

  • Thread starter Daniel Anderson
  • Start date

Daniel Anderson

Daniel Anderson

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2011
Messages
878
Likes
1
Points
0
Daniel Anderson

Daniel Anderson

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2011
878 1 0
Nimekuwa nikifuatilia jinsi sekta ya miundombinu ya barabara inavyosimamiwa na kugundua udhaifu wa mfumo uliopo.
Barabara zote hapa nchini zinaendeshwa kwa mtindo wa public goods.
Kwa waliosoma uchumi mnaelewa maana ya public good, tofauti na wengi wanavyoelewa.
Public good inasifa kuu mbili, yaani ni non-rival na non-excludable.
Sifa ya kwanza ni kwamba utumiaji wa bidhaa hiyo wa mtu mmoja haumzuii mwingine kuitumia, mfano mimi ninapoangalia tv, siwezi kuzuia mwingine aliyejirani yangu kuangalia au kuona mwanga, rangi au picha zinazorushwa kwenye tv hiyo.
Sifa ya pili ni kuwa upatikanaji wake haubagui watumiaji yaani hata kama sitaki bidhaa hiyo itapatikana tu! Niwe tayari kulipia au nisiwe tayari.
Hapa ndipo penye kitovu cha mjadala wangu, yaani non-excludability.
Barabara zetu zinawekwa kwenye kundi la public goods na hivyo kuzifanya zijengwe bila kutaka michango ya hiyari ya wananchi, lakini pia zinatunzwa bila kutegemea michango hiyo ya wananchi wa eneo husika, bali serikali kuu.
Hata hivyo mfumo huu haujawa wa ufanisi sana kwani linapokuja suala la utunzaji na marekebisho inapotakiwa, hayafanywi kwa wakati hivyo barabara kuharibika na kuchakaa kwa haraka.
Nivema sasa watumiaji wakaanza kutozwa kiwango kizuri kwa matumizi ya barabara. Hii itawezesha kuwa na mfuko maalum wa ukarabati wa barabara na utafanyika kwa wakati, si kwa kutegemea siasa ziamue.
Nadhani wanajanvi mtanikosoa na kuongeza pale nilipokwama au kupotoka.
Nawasilisha.
 

Forum statistics

Threads 1,236,611
Members 475,218
Posts 29,264,113