Barabara ipelekayo wengi mapenzini !!

Barabara ipelekayo wengi mapenzini !!

Tetra

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
1,526
Reaction score
771
Wengi wetu tumeingia katika mapenzi kwa matarajio mema,,japo mwisho wake umekuwa ni machozi kwa wengi wetu.
Hizi ni baadhi tu ya sababu zinazowafanya wengi wetu tuishie katika Mapenzi.
::
KUTAFUTA USALAMA KUNDINI
Inatokea mara nyingi pale mtu anapokuwa amezungukwa na marafiki ambao wana wapenzi.Hivyo anashawishiwa pasipo hiari yake atafute mpenzi ili apate usalama kundini.Anaogopa kutengwa au kuitwa mshamba.
::
PESA
Hili limeongelewa sana.Nathubutu kuita sababu hii kama "Main road" iendayo katika mapenzi.Wapo ambao wanafanya mapenzi wapate pesa kukidhi njaa zinazowasonga.Na watoao pesa hufanya hivyo si kwa sababu ya upendo wa dhati la! Bali pesa itawapa mapenzi.
::
KUTOA SHUKRANI
Sababu hii inawakumba sana wanawake.Baadhi hutoa miili yao kama tu namna ya kushukuru waliposaidiwa,walipookolewa na wanadhani hawana namna nyingine.
::
KULINDA AHADI YA NDOA
Wengi wameingia mapenzini kwa njia hii,hususani wachumba ili kujuana kimwili.Waamini kwa kufanya hivi atamteka mwenzi asibadili wazo la ndoa.Hili limewaacha wanawake wengi na mimba na wanaume wamebaki na maumivu ya kukimbiwa kwa wenzi wao kuchukuliwa na wengine.
::
TEKNOLOJIA
Kukua kwa mawasiliano ya simu,mitandao ya kijamii kumewakutanisha watu ktk mazingira ya kimapenzi pasipo kujielewa.Simu zimeondoa aibu.Na bila kutegemea wamejikuta tayari wamo mapenzini.
::
MAARIFA YA MAPENZI
Haya yamezagaa juu ya kufanya ngono,mf magazetini,redioni ktk mitandao n.k Vijana wengi wanaamua kujaribu staili wanazosoma au kuona ili wajiweke fiti.Na tayari wapo mapenzini.
::
UPWEKE,USEJA
Wapo ambao wameingia ktk mapenzi ili kuukimbia upweke.Wamechoka kuwa peke yao.
::
ALAMA YA KUPENDA
Wapo ambao wanaona njia bora ya kuonyesha kupenda kwa dhati basi ni kufanya mapenzi.Maua,zawadi na maneno hazijawa njia zilizokomaa kuonyesha mapenzi ya kweli.
::
TAMAA ZA MWILI TU
Wapo ambao wamesukumwa na miili yao na hawana sababu nyingine.
::
SHINIKIZO
Wapo walioshinikizwa na wazazi waingie ktk ndoa kabla ya muda wao,wengine ni umri,wengine ni mimba n.k
::
MIVUTO
Wapo ambao wamo ktk mapenzi kwa sababu ya mivuto tu.Wapo waliovutiwa na akili,,umbo safi,,sifa ya mtu kazini/mtaani,,upole,,sauti,,tabia,,umbile (mnene,mwembamba,mfupi,mrefu)n.k
=
MAPENZI YANAWEZA KUKUPA MAKAZI MEMA SIKU ZAKO CHACHE DUNIANI UKAZIONA NYINGI
PIA
Mapenzi yanaweza kuwa anguko la maisha yako.Tumshirikishe Mungu sio tu baada ya matatizo bali hata kabla ya kuzifuata barabara hizi.
=
 
Unasemaje? Kama vile vile sijakusikia vizuri?
 
Back
Top Bottom