Bar hii sintakunywa tena!

Na wewe huna tofauti na hao "nzi".. Unashindwa nini kuitaja jina?

Kaka JF inasomwa na mamilioni ya watanzania, nikiweka jina hapa, nitamuharibia biashara, naamini hata yeye ni memba wa JF ataona ujumbe huu na kuufanyia kazi
 
Mkuu hao ndio vijana tunaowaita wajanja wajanja!! Wanajua stori zote za mjini!
Ukiwekwa kati utasema hawa ndio watu ikija bili imekula kwako! Hizi bia za vilinge hizi hazifai aiseee!
 
wewe ni mmojawao nini?

LIKUD sehemu unayosema siifahamu lakini mwanaume mwenzio anakuamisha bar kwa maneno tu!vipi kama angekuwa anamfuatilia mkeo,ungeama nyumba?
 
Last edited by a moderator:
sioni sababu za kuhifadhi jina la hiyo baa maana hapa tupo kujuzana ili na sisi tuwe na uelewa wa mambo katika jamii hii yetu ndio maana halisi ya jamii forum. Nami naungana mkono na wadau wengine kwamba sio sababu ya ww kuacha kunywa hapo eti kwasbb ya jamaa wanaopiga mizinga!!! ww waambie sina hela full stop! au ukiwanyima watakufanyia saa ya kutoka?
 
LIKUD sehemu unayosema siifahamu lakini mwanaume mwenzio anakuamisha bar kwa maneno tu!vipi kama angekuwa anamfuatilia mkeo,ungeama nyumba?

hahahaha!! unajua mkuu tunatofautiana kwenye hulka,wengine hawawezi kumkoma nyani!!
 
Last edited by a moderator:
kama huweki jina la hiyo bar whats a point ya kutujazia seva humu jf,nenda kwa mwenye bar,umwambie
 
Hebu taja jina la hiyo bar ili walevi wenzako wawe makini nayo.
 
Nomba ufike pale NBC CLUB au zamani zetu GEORGE'S GRILL ndio utajua mizinga ya baa ikoje! Pole lakini ila fundisho dawa ya mizinga kaa counter

Mkuu utakuwa hujatutendea haki kama hutatuambia mizinga ya hapo ikoje! Haa haa haa, nimejikuta nacheka mwenyewe
 
Kesi za walevi bwana.inawekekana mleta hoja ni pombe tuu imemzidia
 
LIKUD wewe ni muungwana sana kwa kuwa hukumezea kilichokukera ingawa kwa makusudi umeficha jina la bar.

Huwezi kutahadharisha watu kuwa kuna kichochoro hapa jijini ukipita unakabwa na usipataje.

Please pataje no matter what!
 
Last edited by a moderator:
mbaazi ikikosa maua husingizia jua, kaka naona na wewe kidogo salio halisomi......unaogopa kivuli chako maneno kibao mara ooh wananinywea hahahaha kama vip wanao wakuletee sebuleni ama hazinogi tehetehetehte
 
wacha kusema wenzio wewe, we mwenyewe usikute huachi hela ya kutosha home na kuwafanya wa bargain wanapnunua vitu mpaka inakuwa aibu. ACHA POMBE
 
Hii tabia inaniboa sana tena dar ndo imekethiri sana unakuta mtu hakujui wala nini anajidai anakupa ushauri lakini huo ushauri ni kwa faida yake kisa unanunua bia za kutosha!
 
Hivi mwanaume na suruali yako unaomba bia? Yaani bia kweli?
Mimi hata nikiitwa na washkaji zangu Bar fulani kama sina chochote siendi seuze kuomba!
 
Basi usinune mkuu twende pale Baa Pasaka hii nitakununulia bia mimi
 

Lazima nianze kwa kusema samahani sana kama nitakuudhi kwa ushauri wangu! Jamaa kama wewe hujulikana kwa jina la kebehi kama ''mlenda''. Yaani watu wa dizaini yako wana ule upole uliopitiliza (umechanganyika na ushamba) na mara zote unakuta uso unang'aa ng'aa kwa jasho la mafuta mafuta na hawaishi kukenulia watu meno. Sasa mtu wa dizaini yako mtoto wa mjini hakuangalii mara mbili kujua zoba hiloooo! Ndio maana wanakupiga mzinga na wakija marafiki zao, wanaagiza, halafu wanasukumizia oda kwako. Jaribu kuwa serious usichekecheke na mpe mtu laivu. Jivue gamba la ushamba la sivyo kuna siku utadaiwa kodi kwa sababu unatembea mchana wa jua kali!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…