Akiwa amejawa na furaha na bashasha baada ya kuzukiwa na muujiza wa kusamahewa madhambi yake bila kuomba msamaha mdharauliwa, waziri mkuu mizengo pinda, jana jioni alilidanganya bunge kwa kuliahidi kwamba kila kilichoazimiwa na bunge kitatekelezwa kama kilivyoazimiwa kwa ukamilifu.
Pinda,akiwa na nguvu mpya zilizomuwezesha kucheka kwa mara ya kwanza toka siku ile PAC wasome report yao bungeni,akadai atatumia mfumo wa BANGO KITITA katika kuhakikisha utekelezaji wa maadhimio hayo.
Moja ya azimio ni utaifisishaji wa MALI ZA IPTL.
Najiuliza,Pinda atatekelezaje hili kwa ukamilifu?
Mkuu,
Hakuna sehemu ambayo maazimio ya bunge yameitaka serikali kutaifisha mali za IPTL.
Bunge limeiomba serikali iangalie uwezekano wa kuinunua mitambo ya IPTL.
Nadhani Kununua na kutaifisha ni vitu viwili tofauti.
Mapendekezo ya PAC ikiwa ni pamoja ma kutaifisha mitambo ya IPTL yaliondolewa bungeni na Mwenyekiti wa PAC, Zitto na kuweka mapendekezo ya Kamati ya maridhiano.
Mkuu
Naona unatengeneza maazimio yako sasa.
Na hata kama ni kununua,atawezaje kutekeleza wakati acquisition ya namna hiyo haipo kwenye mipango ya serikali ya mwaka,miaka mitano wala ishirini?
Si tu kwa ukamilifu bali hata kwa robo yake, hatatekeleza!Akiwa amejawa na furaha na bashasha baada ya kuzukiwa na muujiza wa kusamahewa madhambi yake bila kuomba msamaha mdharauliwa, waziri mkuu mizengo pinda, jana jioni alilidanganya bunge kwa kuliahidi kwamba kila kilichoazimiwa na bunge kitatekelezwa kama kilivyoazimiwa kwa ukamilifu.
Pinda,akiwa na nguvu mpya zilizomuwezesha kucheka kwa mara ya kwanza toka siku ile PAC wasome report yao bungeni,akadai atatumia mfumo wa BANGO KITITA katika kuhakikisha utekelezaji wa maadhimio hayo.
Moja ya azimio ni utaifisishaji wa MALI ZA IPTL.
Najiuliza,Pinda atatekelezaje hili kwa ukamilifu?
Jambo ambalo tunasahau ni kwamba ni rahisi sana kikao cha januari ku-postpone issue kama hiyo... kuna issues elfu kidogo ambazo zimeshapata kuwa postponed. Watadanganywa hadi bunge la Aprili... bunge la April litakuwa bize na bajeti na baada ya hapo, bunge la July wabunge wanakuwa washavurugwa tayari... kila mtu anafikiria jinsi ya kurudi mjengoni... ni kwamba watu watakuwa wanaombea kikao cha bunge kiishe warudi majimboni kujisalimisha kwa wananchi na baada ya hapo, kila mtu na lwake!!Januari sio mbali.Mbivu ama mbichi zitajulikana.
Mkuu
Naona unatengeneza maazimio yako sasa.
Na hata kama ni kununua,atawezaje kutekeleza wakati acquisition ya namna hiyo haipo kwenye mipango ya serikali ya mwaka,miaka mitano wala ishirini?
Kama unataka kusoma maazimio yote gongaHAPA7. KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati imeonesha jinsi ambavyo TANESCO imekuwa ikitumia mabilioni ya fedha kulipa gharama za umeme unaozalishwa na IPTL na hivyo kuathiri hali ya kifedha ya Shirika hilo;
KWA KUWA, Taarifa Maalum ya Kamati inaonesha kwamba TANESCO itaendelea kulipa fedha nyingi kwa ajili ya gharama za umeme huo wa IPTL;
HIVYO BASI, Bunge linaazimia kwamba Serikali iangalie uwezekano wa kununua mitambo ya kufua umeme ya IPTL na kuimilikisha kwa TANESCO kwa lengo la kuokoa fedha za Shirika hilo.
Mkuu ni kweli kua hakuna azimio la kutaifisha mitambo ya iptl...bali kuangalia uwezekano wa kuinunua....hilo swala la kutokuwepo kwenye bajeyi ya serikali....n comment