Bangi ijadiliwe kwa uwazi na kwa mapana yake

NkumbiSon

JF-Expert Member
Sep 22, 2013
2,390
3,332
Kama kichwa cha habari hapo juu, kumekuwa na hoja nuingi zihusuzo bangi. Lakini michango yake mingi imekuwa katika mtazamo mmoja wa ubaya wake pasi na kushusha hoja zinazothibitisha huo ubaya au madhara ya kilevi cha mmea wa bangi.Hivyo basi kwa wenye uelewa na bangi kama ina faida na kwa wale wnye uelewa na bangi kama ina madhara nawaomba mshike hapa tuujadili huu mmea kwa kina.Uzi wangu unatokana na maswali yanayoniumiza sana kila siku so naimani katika hyo michango nitapata majibu.

Maswali hayo ni;

1. Nitamtambuaje mtu aliyelewa bangi?

2. Katika vilevi vyote hasa unga pombe na bangi, ni case gani huua watu wengi kwa mwaka, au kuzalisha matatizo ya akili, na kwa maisha yetu ya kila siku ni kilevi gani kinapotumiwa na mtumiaji mara nyingi ni huwa kero kwa wengine?

3. Je ni mlevi wa kilevi gani kati ya unga pombe na bangi anayeweza kutenda majukumu yake pasi nakujulikana katumia kilevi chake.Ni hayo na mengine mengi, ila nitafurahi sana kama watakaochangia watakuwa wale wanaoijua bangi iwe kwakuwahi kuitumia, kuiona, na hata kuisoma. Watu wa masuala ya afya yaani ma dr na watu wa taasisi zinazopambana na madawa ya kulevya na watu wa jamii zinazoitumia bangi kama sehem ya maisha yao watatusaidia sana himu kama wapo.
Wengineo sio mbaya yukiwa wanafunzi juu ya hili.

#kikubwa elimu.
#tupate uhalisia kuliko kuishi kwa hisia
 
pombe,mirungi,unga,na sigara vinamadhara makubwa mnoo!! na tunashuhudia baada ya kuelezwa kinagaubaga na wataalamu wa afya,bangi INA madhara kwa mtumiaji ambaye ktk ukoo wao kuna tatizo LA ugonjwa wa akili wa kurihi,lipo hili wataalamu watatuambia hapa,zaidi ya hapo sioni shida na ganja KBS,naitumia toka drs LA NNE,nmefika chuo vzr na nna kazi yngu na familia na bado natumia km starehe kwangu,hainisumbui hata kdg,onyo ckushauri utumie bila kuijua vzr taarifa zake
 
Bangi siyo mbaya wabaya ni wavutaji anageuza bangi kama chakula tumia bangi ukiwa umetulia huna stress wala msongo wa mawazo
 
Mi binafsi bange huwa inanisaidia sana, nashangaa watu wanaisema vibaya kwa nadharia tu, hawakuwahi hata kujaribu kuivuta.
Eti wanasema pafu moja sijui unapata wehu mwaka mzima.
Mbona babu hadi amefariki anavuta bangi tu na hajawa mwehu na sisi tulikuwa tunamwibia na kuvuta tangu darasa la sita!
 
Unajua sisi kama watanzania ama watanganyika hatujawahi kukaa nakukubalia bangi ipingwe hapo tungekuwa na sababu ya kwanini ni haramu, uharamu tumeupokea tuu lakini kuna uwezekano kila familia Ina mvuta bangi, kuna watu nawashuhudia mpaka leo bado wanavuta na hawajawahi kuzingua. Wala kuwehuka,.

Kuna jambo moja mtu mwny matatizo ya akili anaweza kupata vuta bangi, kunywa pombe hata vilevi vingine, je matokeo ya matatizo yake yanafaa kuhusishwa na kilevi alichotumia, mara bangi inadatisha je waliodata wote ni wavuta bangi?

Kuna watu wanaamini ktk bangi mfano ma jah ras tafarian, mbona wao wanahubiri upendo na amani.? Au ndio bangi, sasa kwanini wote tusivute dunia isiingie vitani
 
Bangi ni mmea wa mungu kwa sababu ni mmea ambao binadamu hatengenezi.....ila madawa ya kulevya na viroba ni vtu vya kupigwa vita kwasababu vinatengenezwa na watu
 
Back
Top Bottom