Harufu nimeshindwa kukoti uzi ulionijibu nitawaumiza watumia simu, nimeshangaa sana labda kichwa chako ni kizuri nimewahi hadithiwa na mtu wangu wa karibu kuwa siku aliyovuta sigara alilala bafuni. Je inawezekana wewe kichwa chako ni tofauti? unajisikiaje ukivuta maana unasema unavutia starehe? je huoni kuwa bangi inachukua nafasi ya mke?.
mama kubwa siku nyingine niite, maana kukosa kutembelea Uzi wote wala nisingejua kama umeniitikia, na ukanijia na Swali lingine.
Karibu sana na ujisikie huru kuniuliza Suali lolote lile, lengo hapa ni kuweka mambo sawa na kuelimishana, au sijui niseme kufahamishana.
Ujue si vizuri kupotoshana, simshawishi Mtu yoyote yule avute. Ninachojaribu kukifanya hapa ni kukanusha yale mambo mengi yanayozungumziwa kuhusiana na JANI.
Na hapa nitajitahidi sana kufupisha, sababu hata ile jana sikutaka niteremke sana kuhusiana na majukumu niliogopa bandiko langu lingekuwa refu sana. Naomba niongezee kidogo pale kwenye Majukumu.
Ukiachilia Mdogo wangu ambae mimi ndio kila kitu juu yake, nina Watoto (Wanangu) Wawili ambao nao najitahidi kwa Hali na Mali kuwahudumia, ukiachilia Watoto zangu, kumbuka sisi Waswahili Familia zetu zinakuwa kubwa sana yaani, Mtoto wa Baba Mkubwa, Mtoto wa Baba Mdogo, Mara Mtoto wa Mjomba, Mara Mtoto wa Shangazi, inaweza ikatokea dharura yoyote ukapigiwa Simu "Bwa Mdogo, Fanya maarifa Mdogo wako kasimamishwa Shule na mimi hali yangu si nzuri" Inabidi niokoe Jahazi ili Maisha yaendelee, huu ni mfano mdogo tu, na mwingine anaweza akakupigia yeye mwenyewe moja kwa moja "Kaka nina shida Biashara zangu zimekwama naomba unipige JEKI" inabidi nidhamini pambano ili Maisha yasonge Mbele. Hii ndio hali halisi ya Maisha yetu.
Ngoja niendelee na Suali la leo, Bangi kuchukua nafasi ya Mke kama nimekupata na kama sijakupata vilevile. Naogopa kujibu moja kwa moja pengine nitakuwa nimeelewa Suali lako vibaya. Kama hutojali unaweza kuninyambulia japo kidogo tu ili niwe na uhakika zaidi ya nitakachokijibu.
Kuhusu Mtu wako wa Karibu, kuna mawili:- Inawezekana kabla ya kuvuta alishapata Kilevi tayari, mfano Pombe na alipoongezea na Bangi na kwa kuwa ilikuwa mara yake ya kwanza ikamchukua zaidi, au inawezekana pia huko alipovuta, au huko aliponunua inawezekana ilichanganywa na Sumu (Unga), maana kuna Wavuta Unga wana kawaida ya kuchanganya na Bangi ili Stimu ziongezeke. Na ndio maana mimi binafsi naiamini sana Bangi ambayo naichambua mwenyewe, na nainyonga mwenyewe kabla ya Kuivuta.
Ni kweli kabisa navutia starehe, maana ukishapata Mistari yako halafu ukatulia sehemu kwanza Mwili unausikia una joto sana, kama ulikuwa unajihisi Uchovu kabla ya kuvuta basi ukishavuta unajihisi uchangamfu wa hali ya juu. Kuna mambo mengine nashindwa namna ya kuelezea kuna hali fulani, yaani hailezeki, nashindwa namna ya kuilezea kwa ambae si mvutaji.
Nakaribisha Masuali zaidi, ila usisahau kuninyambulia "
je huoni kuwa Bangi inachukua nafasi ya Mke?"