Bandeko Nangai Ya Kabila | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bandeko Nangai Ya Kabila

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Oct 20, 2008.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Wakati sisi tunafanya ziara za dunia kutafuta umaarufu na win win situation, huku tukiuza mashirika na viwanda kila kukicha, kijana wa Baba Josefu anaanza vitu vyake!

  Miezi kadhaa nilianzisha thread kuhusu Congo kuanza kufanya mapinduzi ya maendeleo taratibu, lakini watu wakaona kuwa hilo halitoshi.

  Sasa najiuliza ni lini Mwankupuli ataamka na kuanzisha mapinduzi mapya ya maendeleo kwa Taifa letu?

  Congo wametuwashia indiketa kwa muda sasa karibu watatupita, Rwanda nao washatuacha kama lile Scania la Riziki kwa Mungu, Msumbiji wala tusifikirie kuwagusa huku Zambia na Malawi wakipetesha ngano na kuona kuwa Namibia ni bora kwao kimaendeleo kuliko Tanzania.

  Hivi tunakwenda wapi jamani? mbona tunaendelea kuzubaa?

   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Oct 20, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Rev. Kishoka,
  Mkuu unampiga mbuzi gitaa!..nani anataka kulima ikiwa kila kitu imported ndio mali?...
  Utachukua muda mrefu sana kuwafahamisha viongozi wetu ambao wakienda Mlimani city wanaona maendeleo ya Ulaya yakija Tanzania..
  Tunakula kama Ulaya vile..
   
 3. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mkandara,

  Hilo swala la kila kitu imported linaleta swali, tunapata wapi pesa za ku-import vitu?
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Rev.
  Unataka jibu kwa swali lako? Jaribu ufisadi. Hivi yule mama aliyenunua (kujitwalia) nyumba 12 kule Mbeya alipata wapi fedha za mtaji?
   
 5. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Wakati Bi. Salma alipokuja kutibiwa Unyamwezini, nilikuwa na maongezi na mkulu mmoja, nikamuliza inakuwaje kuwa Tanzania inaacha kuwa wabunifu na kutumia fedha kwa ajili ya faida za muda mrefu na kuishia kununua kila kitu ikiwa ni pamoja na vitu ambavyo tungeingia gharama kuvijenga na kuviendeleza, Tanzania ingeweza kujijenga na kujitosheleza kwa vizazi vijavyo?

  Chukulia mfano, badala ya kujenga hospitali za kutosha na kununua vifaa vya kisasa na kugharamia vyma masomo ya Watanzania kuwa madakitari bingwa, sisi tunaona huko ni kuingia gharama sana na suluhisho ni kupeleka watu India, Afrika Kusini, Marekani na hata Uingereza.

  Sasa likija gonjwa baya kushambulia watu elfu kumi, tutawagharamia wote kwenda Ulaya kutibiwa?

  Njoo kwenye Chakula, haieleweki kuwa Tanzania inaona ni bora kuagiza chakula badala ya kubadilisha mfumo wa kilimo na kuwa na uwezo wa kujitosheleza kwa chakula iwe ni nafaka, matunda, mboga hata mifugo na uvuvi.

  Kwa nini tukimbile kuagiza chakula kutoka Malaysia kila siku huku Shinyanga, Rukwa, Rufiji, Mbarali, Kyela na hata Pemba zinaweza kutuzalishia mpunga wa kutosha? Mahindi na maharage wala usiseme! Ukija mafuta ya kupikia kule Singida mializeti na ufuta unaharibika lakini tuko tayari kuagiza Korie na mafuta mengine kutoka nje ya nchi!

  Sasa ni ujinga na ujuha kama tunashindwa kuhamasisha uzalishaji mali ndani ya nchi kukidhi mahitaji na kukimbilia kuagiza.

  Hivyo vijisent vya kuuza mashirika au mapatu finyu ya madini yana mwisho wake, tukishauza viwanda na dhahabu kukauka serikali itapata wapi fedha? au sasa tutakuwa tegemezi wa misaada kwa 100%?

  Vitu vingine havileti maana hata kidogo!
   
 6. M

  MpiganajiNambaMoja Member

  #6
  Oct 20, 2008
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika kipindi kilicho baki cha miaka 2 kwa Mh. Rais tusitegemee mapinduzi ya kiuchumi kutokea. Sasa hivi Rais atakuwa busy kufanya propaganda na ku-deal na watu wachache ambao anaona ni threat kwake kuwania tena uras 2010.

  Ameshapoteza mwelekeo, hivyo kataika kipindi cha miaka 2 ijayo maisha yatazidi kuwa magumu sana. Kumbuka ni katika kipindi ambacho pia wanataka kukusanya fedha kwa ajili ya uchaguzi.
   
 7. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Jasusi na Mkandara,

  Kuna hii sehemu iliyoko ndani ya Azimio la Arusha ambalo inazungumzia mambo ya fedha.

  Ni muhimu kuirudia na kujipima kama kweli tunakwenda kuliko kwema au ndio tunazidi kukongoroka!

   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Oct 20, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,382
  Trophy Points: 280
  Kabila anataka kuanza kufanya vitu vya msingi kwanza; kujenga Taifa.
   
 9. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Sasa sisi tunafanya nini na Mwankupuli wetu?
   
 10. n

  nzela New Member

  #10
  Oct 21, 2008
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hatimaye nimeamua kuchungulia ! ! !
   
 11. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Rev:

  Amani iwe kwako pia. Nadhani kuna makosa makubwa tuliyofanya. Ukiangalia bajeti ya Tanzania mfuko wa hazina unachukua sehemu kubwa. Kwanini mfuko huu unachukua sehemu kubwa ni kwa sababu miaka Ujamaa ulipopamba moto serikali ilipanuka sana, nafasi nyingi za kazi zilianzishwa ambazo zinatumia sehemu kubwa ya pato la nchi.

  Rwanda na DRC nazo zilipanua serikali zao. Lakini vita vya wenyewe kwa wenyewe vilisababisha muundo mzima wa serikali kubadilika. Na kuna uwezekano mkubwa sana kuwa serikali ya Kabila ina watumishi wachache kuliko serikali ya Mobutu.

  Tanzania hivyo vitu vinawezekana lakini tupo tayari kubadili mfumo mzima wa serikali hili uwe wa wafanyakazi wachache na wenye kuleta ufanisi.

  Uwezi kufungua shule za sekondari kwa kila kata na baadaye ununue matrekta wakati kwa ajili ya kuendeleza kilimo. Muhimu wa shule za sekondari hupo lakini gharama za kuendesha shule hizo ni kubwa na inachukua muda mrefu kuleta matokeo.

  Kwa maoni yangu tatizo letu, tulichemsha toka tumepata uhuru kuelewa ni vitu gani vya kuanza. Elimu, Kilimo, Siasa, Afya na mambo mengine ni muhimu sana kwa maisha ya binadamu. Lakini kama resource zako ni ndogo ni lazima uchague.

  Tujiulize ni kitu gani tulitakiwa kukiweka mbele. Juzi naongea familia yangua Tanzania wanasema katika heka 5 za mahindi wamepata gunia 20. Hii inaonyesha kuwa hata kwa standard ya Afrika, watanzania bado ni wakulima primitive.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Oct 21, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,382
  Trophy Points: 280
  Inawezekana vipi nchi kama Rwanda na Congo kuweza kujenga jamii ya kisasa baada ya vita vya wenyewe kwa kwenyewe? Nchi kadhaa ambazo zimewahi kuwa na machafuko ya wenyewe kwa wenyewe ndizo ambazo kwa kiasi kikubwa zinajitahidi sana kujenga jamii bora; Marekani, Indonesia, Rwanda, Angola n.k je kuna somo ambalo tunatakiwa kujifunza?
   
 13. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #13
  Oct 22, 2008
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Apewe muda zaid ataonesha kali zake bado wakati ano wakufanya mengi kwani hata kipindi kimoja haja maliza tusubiri mwishowe mwakipindi cha pili tutaona mzao yake naimani nae ataleta mapinduzi ya kimaendeleo na ulimwengu utashangaa
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Oct 22, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hapa unamzungumzia Kabila au Mwungwana?
   
 15. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #15
  Oct 22, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hili swali linaogopesha, halafu sidhani kama kuna mtu anapenda twende huko. Ila watu wakishachoka ndio hivyo tenaa wanaweza kuanza hayo mambo. nadhani umeona watu walimwanzishia Chief mwankupili Mbeya. Tuombe Mungu.
   
 16. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #16
  Oct 22, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hata mageuzi ya uchumi na civilization ulaya yalianza baada ya vita ya pili ya dunia. antibiotics pia ziligunduliwa baada ya vita ya pili ya dunia.Vita zinafanya watu wakumbuke kuwa maisha sio tu "tambarare" kama wanavyosema bongo, hivyo basi watu huanza kutafuta utatuzi wa matatizo mbalimbali. Hata hivyo, no one in their right mind would consider to start wars just that they can get to think better!!!
   
 17. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #17
  Oct 22, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kwa nini basi nasi tusiepuke vita na kuwa kama Botswana lakini tunataka tushikane mashati kwanza patashika bin kuchanika ndipo tuamke na kuanza kuijali nchi yetu?

  Wenzetu wanatupita kwa kasi ya ajabu. Nitawaambieni hili na kuwa muwazi, kwa mwaka mmoja akiwa Raisi, Kikwete anatumia takribani si chini ya Dola Millioni saba ($7,000,000.00) kuzunguka dunia kwa safari ambazo hazina matunda ya maana. Hizo pesa japo zaonekana ni kidogo, zidisha mara tatu halafu jiulize, zingejenga hospitali ngapi au shule ngapi? au kulipia wanafunzi wangapi? au kuongeza mishahara ya watumishi wa Serikali wangapi?

  Udhaifu wa Kikwete na Serikali yake si ajabu umezidisha uchochezi wa uhujumu kutoka kwa Wananchi wa Tanzania kwa kuona hamna maana ya kuchacharuka na kujituma, hivyo tunasubiri damu imwagike.

  Majaribio tumeyaona Mwanjelwa na Chunya, yalianza mawe....
   
 18. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #18
  Oct 22, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rev,

  Hiyo kwenye red ni very sad but true, wakati mwingine inaumiza sana moyo kuujua ukweli. Inaumiza kiasi cha kutamani usingejua chochote kile ambacho viongozi wa nchi yako wanafanya.

  Kwa mambo kama haya, giza linazidi kutawala ujao (future) wangu zaidi sana sasa kuliko miaka mitatu iliyopita.
   
Loading...