Bandarini Dar: Rais Magufuli akamata Magari takribani 53 yasiyo na mwenyewe, IGP alaumiwa Mikataba ya Lugumi

Magari hayana mwenyewe ama wameshindwa kulipa kodi?

Mkuu mpaka sasa huo mshikemshike uko live tbc1. Kila mkuu wa taasisi anasema kapata taarifa ya hayo magari leo asubuhi. IGP Sirro alitaka kujifanya kuyaongelea ila kabanwa kayaka, Boss wa Bandari anajiumauma tu, wa Takukuru anasema kpata taarifa leo asubuhi. Waziri Mpango naye anajiumama tu. Wameambiwa wote watoe ripoti ndani ya siku 7. Rais anasema biashara ya upigaji imerudi kama kawaida. Huwa simuungi mkono rais hasa kwenye demokrasia na mambo fulani fulani lakini kwa hiki namuunga mkono.
 
Heshima kwenu wakuu.

Leo rais baada ya kutembelea Meli ta Wagonjwa bandarini, ameamua kuitembelea TPA. Amekuta magari zaidi ya 50 ambayo hayana mwenye. Magari hayo yaliletwa pamoja na Magari ya Polisi.

Magari hayo yameandikwa Ofisi ya rais.

Rais amesema hayo magari siri yake ni kubwa sana. Yamekaa tangu mwezi wa sita Mwaka 2015. Yaleletwa pamoja na Magari ya Serikali.

Amesema haya magari yamefichwa hapa na viongozi wakaa kimya.

Ametoa siku saba aletewe taarifa ya hizi gari.

Amewalaumu Mawaziri kwa kutokufanya kazi zao.

Amewaagiza TAKUKURU, Polisi na Wizara ya Uchukuzi wamletee taarifa taarifa ndani ya siku saba nani amehusika.

Magari haya ni ambulance na yameandikwa Ofisi ya rais.

Pia Rais Magufuli amesema anazo taarifa kuwa 'michezo' ya zamani TRA na Bandarini imeanza kurudi na taarifa hizo anazo..

Inakuwaje rais niapte taarifa za magari kufichwa lakini Waziri, TRa, TPA msijuie? Mnatakiwa muwe na informer wenu sio hadi mimi nije ndo mnaaza kusema sijui..
hapo nashindwa kuelewa juzi juzi tu kakuta vichwa vya treni havina mwenyewe leo kaja kakuta magari hayana mwenyewe au hakikatiza mzee bandarini watu wanatoka mbio kama difenda kutinga kijiweni.
 
Hao akina Sirro ndio wapiga deal wenyewe kisha wanamchomekea rais wanapiga kazi kwa mauaji ya kibiti. Juzi nimemuona Sirro katengeneza igizo la majambazi kumbe hana lolote leo anataka kutetea magari ya wizi.
 
Niko nacheki kupitia tbc hiki ni kituko, nimestaajabu viongozi wote wanaulizwa kimya, eti magari 53 yote yameandikwa ofisi ya rais, rais hayajui na wala viongozi wa bandari, polisi, tpa, tra na takukuru pia wizara ya uchukuzi wote hawajui niya nani.
Usishangae hili magari 53!?

Lilikuwepo la vichwa 13 vya treni nchi ambayo ina mashirika mawili tu ambayo ni ya SERIKALI.
Tanzania hapahapa ambapo mifumo yote ya reli ni ya serikali
 
Niko nacheki kupitia tbc hiki ni kituko, nimestaajabu viongozi wote wanaulizwa kimya, eti magari 53 yote yameandikwa ofisi ya rais, rais hayajui na wala viongozi wa bandari, polisi, tpa, tra na takukuru pia wizara ya uchukuzi wote hawajui niya nani.
Hapo anatafutwa mtu . Utasikia katumbuliwa mtu siyo muda mrefu
 
Back
Top Bottom