ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,116
- 49,840
Bandari ya Kasanga ni miongoni mwa Bandari kadhaa za Ziwa Tanganyika ambazo zikijengwa kwa mbwembwe nyingi na Serikali ya Mwendazake bila kusoma Geografia ya eneo husika.
Bandari hii pia imeunganisgwa na Barabara ya lami kutoka Sumbawanga mjini ambayo ujenzi wake ukichagizwa na uvumi kwamba eti malori yataacha kupitia Tunduma badala yake yaje kupita huku.
Kwa miaka ya nyuma Bandari ya Kasanga ilikuwa inahudumia meli kati ya 30-34 na nyingi ya meli hizo ni zile zilikuja kubeba saruji ya kiwanda Cha Mbeya cement kupelekea DRC Congo lakini kwa sasa DRC wamejenga kiwanda upande wao na kuua soko la saruji ya Tanzania na kuacha Bandari ikiwa tembo mweupe.
---
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo akimsikiliza, Ofisa wa Bandari ya Kasanga, mkoani Rukwa, Rodriguez Valentin alipotembelea na kujionea mradi wa upanuzi na uboreshaji wa bandari hiyo jana Jumatatu, Oktoba 9, 2023 Wilaya ya Kalambo.
Ni katika siku ya pili kati ya nne ya ziara yake mkoani humo ya kukagua miradi ya maendeleo, utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25, kukagua uhai wa chama pamoja na
kusikiliza kero za wananchi.
Chongolo ameambatana na Katibu wa Idara ya Oganaizesheni ya chama hicho, Issa Ussi Gavu.
Akiwa bandari hapo, Chongolo amesema Serikali inaendelea kuziboresha bandari zote kubwa na ndogo ili kuziongezea tija ya utoaji wa huduma kwa wananchi na kuchangia pato la Taifa na la wananchi wenyewe.
Alisema kuna hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali, kuboresha huduma za uchukuzi, usafiri na usafirishaji katika Ziwa Tanganyika, ambapo kufikia Disemba, 2023, wananchi wataanza kupata nafuu, kuelekea kumalizika kwa adha kubwa iliyopo sasa.
Hiyo ni kutokana na kukamilika kwa matengenezo ya moja ya meli, kati ya mbili zilizopo sasa, Mv Mwongozo na Mv Liemba, ambazo zote zinafanyiwa matengenezo, ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya muda mfupi, wa kati na mrefu na MV Mwongozo ndio itaanza kutoa huduma hivi karibuni.
Awali, Valentin akisoma taarifa mbele ya Chongolo na ujumbe wake alisema maboresho mbalimbali katika bandari hiyo ndogo yanaendelea ikiwemo kufunga mashine za kupakia na kushusha mizigo.
Alisema katika mwaka wa fedha 2021/22 bandari hiyo ilihudumia meli 34 na mwaka 2022/23 meli 32. Kuanzia Julai mwaka huu hadi Oktoba 23 wamehudumia meli moja pekee.
Valentin alibainisha changamoto zinazowakabili ikiwemo ya kufunguliwa kwa kiwanda cha saruji cha Kibimba huku DR Congo kimeongeza ushindani wa kibiashara kwa wateja wa Congo waliokuwa wanatumia bandari hiyo.
Alisema bandari hiyo ilijengwa kuanzia 1995 hadi 1998 na awamu ya pili 2018 hadi mwaka huu ikihudumia nchi za Burundi, Zambia na DR Congo ikiwa na gati lenye urefu wa mita 120 na wastani wa kina cha maji mita 14.
Chanzo: Mwananchi
My Take
Serikali mnapofanya vitu muwe mnasoma Geografia ya eneo lenu na la jirani badala ya kukurupuka Kwa mihemko.
Kuna mifano Mingi sana ya kukurupaka ambayo imesababisha miradi Mingi kuwa white elephant.