Nimeikuta sehemu hii
.....................
Kwa wale mnaoratajia kununua
Hiace kwa ajili ya kutoa huduma ya
usafirishaji maeneo ambayo usafiri
huu bado ni muhimu (hususani
maeneo ya miji midogo na ama
kusafirisha wanafunzi maeneo ya
mijini) kuweni macho na TRA.
Jamaa yangu mmoja amenunua
Hiace baada ya kuona katika
Calculator ya TRA (Tanzania
Revenue Authority - Calculators &
tools) kuwa Hiace zote ziko katika
kundi la Utility ikiwa ni pamoja na
magari mengine kama vile: Toyota
Hilux, Canter, Nissan Hard body,
Rosa, Coaster, Civilian, na kwamba
magari yote katika kundi hili yana
aina tatu tu za ushuru (kwa magari
chini ya 2004) , yaani Import duty
25%,Excise duty 5%, na VAT 18%).
Baada ya Hiace kufika BANDARINI
ndipo yakampata majanga.
· Wanamwambia kwakuwa Hiace
yake ina viti vyote ndani sio utility
· Harmonised system (H.S ) code
(Harmonized System - Wikipedia,
the free encyclopedia) iliyopewa
garin yake ni 87032399 (HS Code
87032399 | Harmonized System Code
Other) badala ya H.S code 87029091
(Motor vehicles for the transport of
ten or more persons, including the
driver ITC HS CODE List.)
· Kwa mujibu wa TRA HIACE yake
iko kwenye kundi la station wagon
au racing cars (Station wagon -
Wikipedia, the free encyclopedia,
Google
search?q=s...w=1366&bih=667) .
· Kwa maana hiyo uwepo wa viti
kwenye Hiace yake umeongeza kodi
kutoka wastani wa milioni 5.5 hadi
milioni 9 (karibu milioni 4!!).
· Kwa maana kwamba sasa
atatakiwa kulipa aina nne za ushuru
(yaani Import duty 25%, uchakavu
25% ,Excise duty 10%, na VAT 18%)
tofauti na calculator inavyosema.
Ushauri:
· Ili kuondoa usumbufu kwa
watanzania, na kuongeza uwazi kwa
taasisi hii, TRA hawana budi
kuorodhesha kwenye mtandao wao
gari zote zinazotambulika kama
utility nchini Tanzania ili wananchi
waweze kujua na kujiandaa. Siyo
lazima na ni usumbufu kama kila
anayetaka kununua kitu nje ya nchi
awasiliane kwanza na TRA kujua
taratibu zinasemaje.
· TRA wanatakiwa kufanya
marekebisho kwenye calculator yao
(hususan eneo hili) maana
linapotosha jamii badala ya
kuelimisha
· Wale wanaotarajia kununua Hiace
hakikisheni hazina viti ndani na/
ama fanyeni utaratibu viti
viondolewe hukokuko gari inapotoka
au mara tu baada ya kufika bandari
kavu. Hii ni kwa sababu marginal
benefit ya Hiace isiyo na viti ni
kubwa kuliko yenye viti.
TRA, HUU KAMA SIO WIZI NI
UPOTOSHAJI MKUBWA