Bandari ya Dar es Salaam yafunga kamera 486 kudhibiti wizi

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
739
484
Bandari ya Dar es Salaam yafunga kamera 486 kudhibiti wizi.
kamera24.jpg

Zikiwa zimepita siku chache tangu waziri mkuu Mh Kassim Majaliwa kufanya ziara ya kushtukiza bandari ya Dar es Salaam na kubaini uozo wa kuchepushwa kwa bomba la mafuta mamlaka hiyo imekuja na mpango madhubuti wa kuimarisha usalama katika bandari hiyo kwa kufunga mfumo mpya wa kamera 486 zenye uwezo wa kuonyesha matukio yote yanayotokea nje na ndni ya bandari hiyo na hasa katika eneo la kupakulia mafuta.

ITV ilifika bandarini hapo na kushuhudia namna kamera hizo zinavyofanya kazi huku afisa mlinzi mwandamizi Bw Kiswiza Lukasi akielezea namna mashine hizo zinavyofanya kazi.

Naye Bi Janeth Ruzangi meneja mawasilino wa TPA amesema mashine hizo zinaonganisha na banadari zote lengo ni kuakikisha kuwa usalama unaimarika katika bandari za hapa nchini.

Baadhi ya watumiaji wa bandari hiyo wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia utendaji na usalama wa bandari hiyo lakini kwa sasa wanapata imani kuwa mali zao zitakuwa salama.
 
Hapa kuna mtu anatafuta credit, siyo bure. Hizi kamera zimeanza kufungwa tangu Enzi za Mwakyembe nae aliukuta mradi unasuasua akina Mgawe wanaupiga danadana ndo akaukomalia.
 
Asante kwa kuongeza ulinzi

Lakini
eti ndo kwa mara ya kwanza zinafungwa Ni usaniiiiiii

Yale yale yale kununua Tscan mpya kumbe imetolewa Dodoma hosp
 
Namlilia nyerere tu baas. Naye alikuwa binadam ila alijitahid cha kushangaza vijana wake aliowalea kwenye chama mmoja baadaye alimweka kuwa rais na my engine alimkataa ndio wamelifikisha taifa letu hapa.
 
Je zimeunganishwa na TRA na Usalama? Sitoshangaa baadhi ya kamera muhimu kuzimwa au kuharibiwa kimtindo.
 
Aha ha aha kamuulize sefue atakukuambia Kilichotolewa

hospital I ya dodama Na kuletwa Muhimbili kinaitwaje ?

Wakatudanganya wamenunia mpya ili jakaya aonekane hakufanya kitu ,!

Lakini pale bungeni wameaibika baada ya yule mbunge wa ccm dodoma

kuuliza kwa nini wameiondoa kwenye hospitqli yao kwani hakuna watu ,?

Hapa mbwembwe tuu!!
 
Hapo CCTV Operators watapiga Sana hela, majizi yatakuwa yanacheza dili na hao jamaa. Ngoja niombe kibarua cha kuoperate CCTV hapo bandari
 
BOT wamefunga kamera mpaka chooni, na wanaulinzi mpaka chooni lakini mabilioni yanapigwa hapohapo na walinzi hawaoni. Na wachunguzi wanafika sehemu wanafahamu kwa aina hiyo ya wizi walinzi hawausiki
 
Zinazimwa tu hizo. Hata Stanbic wana camera kila uchochoro na bado watu wakapiga dili...
 
Kuna kifaa ambacho unakivaa mkononi hata kama kuna CCTV camera inakuwa haina uwezo wa kukuchukua picha !!
 
Bandari ya Dar es Salaam yafunga kamera 486 kudhibiti wizi.
kamera24.jpg

Zikiwa zimepita siku chache tangu waziri mkuu Mh Kassim Majaliwa kufanya ziara ya kushtukiza bandari ya Dar es Salaam na kubaini uozo wa kuchepushwa kwa bomba la mafuta mamlaka hiyo imekuja na mpango madhubuti wa kuimarisha usalama katika bandari hiyo kwa kufunga mfumo mpya wa kamera 486 zenye uwezo wa kuonyesha matukio yote yanayotokea nje na ndni ya bandari hiyo na hasa katika eneo la kupakulia mafuta.

ITV ilifika bandarini hapo na kushuhudia namna kamera hizo zinavyofanya kazi huku afisa mlinzi mwandamizi Bw Kiswiza Lukasi akielezea namna mashine hizo zinavyofanya kazi.

Naye Bi Janeth Ruzangi meneja mawasilino wa TPA amesema mashine hizo zinaonganisha na banadari zote lengo ni kuakikisha kuwa usalama unaimarika katika bandari za hapa nchini.

Baadhi ya watumiaji wa bandari hiyo wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia utendaji na usalama wa bandari hiyo lakini kwa sasa wanapata imani kuwa mali zao zitakuwa salama.

SASA MHUSIKA MKUU WA CAMERA PAMOJA NA KULIPOTI KWA MOSS WAKE WA BANDARI PIA AWE RESPONSIBLE DIRECT KWA PM. OLE WAKE TUTAKE KUJUA TUKIO LA SIKU FULANI ILIENDAJE ATUAMBIE UMEME, MTANDAO ULIKUWA CHINI SIKU HIYO NK.
 
486 Cameras. Wataalam tuelezeni Management n Monitoring yake.

On Average 1 person ana Monitor Display ya Cameras Ngapi kwa masaa Mangapi?

to Me is bit insane.
 
Hapa kuna mtu anatafuta credit, siyo bure. Hizi kamera zimeanza kufungwa tangu Enzi za Mwakyembe nae aliukuta mradi unasuasua akina Mgawe wanaupiga danadana ndo akaukomalia.

Wewe unastahili kutembelea Milembe hospital; credit gani wakati ametekeleza kilichostahili kufanywa?!
 
Bandari ya Dar es Salaam yafunga kamera 486 kudhibiti wizi.
kamera24.jpg

Zikiwa zimepita siku chache tangu waziri mkuu Mh Kassim Majaliwa kufanya ziara ya kushtukiza bandari ya Dar es Salaam na kubaini uozo wa kuchepushwa kwa bomba la mafuta mamlaka hiyo imekuja na mpango madhubuti wa kuimarisha usalama katika bandari hiyo kwa kufunga mfumo mpya wa kamera 486 zenye uwezo wa kuonyesha matukio yote yanayotokea nje na ndni ya bandari hiyo na hasa katika eneo la kupakulia mafuta.

ITV ilifika bandarini hapo na kushuhudia namna kamera hizo zinavyofanya kazi huku afisa mlinzi mwandamizi Bw Kiswiza Lukasi akielezea namna mashine hizo zinavyofanya kazi.

Naye Bi Janeth Ruzangi meneja mawasilino wa TPA amesema mashine hizo zinaonganisha na banadari zote lengo ni kuakikisha kuwa usalama unaimarika katika bandari za hapa nchini.

Baadhi ya watumiaji wa bandari hiyo wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia utendaji na usalama wa bandari hiyo lakini kwa sasa wanapata imani kuwa mali zao zitakuwa salama.

Tenda ya mradi wa kufunga kamera ilitangazwa lini, kwenye gazeti gani?
 
Camera 486, My God!!
Hiz ni camera zilizofungwa jiji la zima la Dar au Bandar peke yake.Huu ni upuuz mkubwa sana. Hii ni resources mismanagement. Kwann wameweka Camera zote hizo?? Hiyo monitoring itakuwa inafanyikaje? Hiyo Security Central Control Room itakuwa na watu wangap wakuchek camera zote hizo? I am sure kuna camera zinaweza kukaa hata zaid ya mwez hazifuatiliwa. Haya ni maamuz ya kutokutumia weledi. Sio kila sehem mtu unaweka camera for the sake of kuwe na camera. Lazima uangalie utaimonitor vp na kuimanage vp. Camera 486 ni nyng sana kwa eneo km la bandari. Ni upotevu wa hela usiokuwa na lazima. Zingefungwa chache, maeneo ambayo yana ulazima ili iwe rahis kuzimonitor.
 
Back
Top Bottom