Bandari waanza kuita watu kuripoti kazini

Mtuturas

JF-Expert Member
Apr 18, 2017
458
859
Kwa waliofanya oral na sekretarieti ya ajira.

Waliofaulu wanapigiwa simu na ma hr wa TPA na kutakiwa kwenda.

Kuripoti kazini Jumatatu 25/03/2019.

Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kupata ajira TPA.

kusema kweli mchakato ni wa haki simjui mtu wala sikuhonga chochote sekretarieti ya ajira.

Hongereni kwa walifanikiwa kupigiwa simu na kwa ambao hawakufanikiwa niwaambie waendelee kustruggle na kumuomba Mungu ipo siku mambo yatakuwa vile wanategemea
 
Haya mkuu hongera tushajua kama unafanya kazi bandarini..

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante mkuu, bado sijasaini mkatakaba mkuu, kwa sasa nina ajira yangu nyingine naendelea nayo nikishauona mkataba wao wa kazi ndio nitafanya maamuzi ya kujoini nao au kudecline their offer,
all in all thanks a lot mkuu, sio kwa nyomi lile la kwenye interview,
dah jamani tusikatishwe tamaa na idadi ya watu walioitwa kwenye usaili manake mwisho wa siku lazima aajiriwe mtu na mtu huyo anaweza kuwa wewe kama na wewe upokwenye usaili huo
 
Asante mkuu, bado sijasaini mkatakaba mkuu, kwa sasa nina ajira yangu nyingine naendelea nayo nikishauona mkataba wao wa kazi ndio nitafanya maamuzi ya kujoini nao au kudecline their offer...
Hahah kwahiyo unataka uchungulie mshahara kwanza au sio?
 
Watu hawatangazi kazi waliyopata. Ninaamini umetumwa kuwaaminisha watu kuwa mchakato ulikwenda bila upendeleo. Hilo ndio lengo lako kuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijatumwa na mtu yeyote mkuu,

Ninatoa taarifa tu ya mchakato wa ajira hizo kwani hata huku JF taarifa za ajira hizo zilifika.

Kimsingi unifahamu,sikufahamu <Mtuturas> sio jina langu ni ID Feck.

Halafu sio kweli kwamba hairuhusiwi kutangaza kazi uliyopata,

inategemea na ajira gani,

Halfu ukiacha Jf hadi sasa kiukweli nimemtaarifu mtu mmoja tu mshakaji wangu ambaye tulifanya wote usaili huo.

Mbona sekretarieti ya ajira inatangaza majina ya watu walioitwa kazini, fikra zako zitakuwa finyu sana mkuu, kama unahisi mambo ya kishirikina kuhusu kutoa taarifa ya ajira.

Halafu pia siku hizi mataasisi mengi watu wanavaa mayunifomu ya kampuni siku za ijumaa hivyo mtu hawezi kuficha kazi anayofanya.
Kwa upande wangu mchakato wa nafasi niliyochaguliwa sijanufaika na aina yeyote ya upendeleo ,
 
Acha kuzuga wewe eti nikiuona mkataba ndo nitafanya maamuzi.

Hata ungekuwa wapii lazima uende TPA hata kama mkataba mbovu.

Ulikuwa unaomba kazi na hujui mikataba ya TPA ipoje???
Asante mkuu, bado sijasaini mkatakaba mkuu, kwa sasa nina ajira yangu nyingine naendelea nayo nikishauona mkataba wao wa kazi ndio nitafanya maamuzi ya kujoini nao au kudecline their offer...
Anyway hongera sana.

Siyakudumisa Nkosi Yezulu
 
Kwanini wasitoe majina? ili kama wengine tumekosa tujue.. Wewe uliitwa kwa post gani? maana mimi nilikuwa kwenye management system Officer..
 
Kwa waliofanya oral na sekretarieti ya ajira
waliofaulu wanapigiwa simu na ma hr wa TPA na kutakiwa kwenda
kuripoti kazini Jumatatu 25/03/2019.
Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kupata ajira TPA
kusema kweli mchakato ni wa haki simjui mtu wala sikuhonga chochote sekretarieti ya ajira.
Hongereni kwa walifanikiwa kupigiwa simu na kwa ambao hawakufanikiwa niwaambie waendelee kustruggle na kumuomba Mungu ipo siku mambo yatakuwa vile wanategemea
Zaidi ya barua ya kuitwa kazini mkataba sahau tuna kitambo hapa hatuna hiyo mikataba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukuru Mungu umepata tu hayo maneno menginē eti mchakato wa haki sijui sikuhonga achana nayò
Mimi ni shahidi namba mbili baada ya mtoa mada. Nimefanya interview 3 kupitia sekretarieti ya ajira. Hanijui mtu wala sina hata jamaa huko ila interview ya 3 nikapata ajira. Tulikua candidates 1200+ nafasi 23. Tukafanya interview 3, written, practical na oral.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom