Bandari kusimamiwa na wageni, siri za Jeshi letu haziwezi kuvuja kwa vifaa vinavyopitia bandarini?

Kiuhalisia Jeshi halina nafasi ya kuhoji kwakua linaendeshwa kisiasa na kupokea maelekezo ya wanasiasa.
Amiri jeshi mkuu ni Rais ambae ni mwanasiasa na mwenyekiti wa ccm, na huyo ndo kamteua CDF mkuu wa majeshi
huyu mwenyekiti wa ccm anampa maelekezo CDF na CDF anapokea Kama amri kutoka kwa amiri jeshi kumbuka jeshini hakuna kuhoji ni kupokea maelekezo tu

ukionekana siyo mwepesi kupokea maelekezo huyu mwenyekiti wa ccm anayo mamlaka ya kukuondoa na kumtea CDF mwingine

Duu!KATIBA mpya ni muhimu sana
 
Wakuu mimi najaribu kuwaza tu kwa wepesi wangu wa akili.

Sote tunajua kwamba mambo ya usalama wa nchi na hasa yale yanayohusu jeshi huwa ni siri ya jeshi japo wananchi tuna nafasi yetu ya kushirikiana na jeshi maana nchi ni yetu sote na jeshi ni mali ya wananchi kikatiba.

Sasa swali langu ni pale kunapotokea maamuzi ya mambo fulani fulani yanayofanywa na viongozi wa serikali afu hayo mambo yakawa yanagusa maslahi ya jeshi kwa namna moja au nyingine, jeshi halina nafasi ya kufanya au halipaswi kufanya lolote?

Kwa mfano hili suala la bandari, tunajua silaha na vifaa mbalimbali vya kijeshi inawezekana vinapitia bandarini, sasa kama bandari zitakuwa zinasimamiwa na wageni badala ya serikali yetu, siri za jeshi letu haziwezi kuvuja?

Naomba kuwasilisha.
Wenye kutunza siri ni wanaozalisha wenyewe vifaa vya kujeshi sio nyinyi mnao-import mseme kuwa siri zenu zitavuja.
 
Back
Top Bottom