Bandari kusimamiwa na wageni, siri za Jeshi letu haziwezi kuvuja kwa vifaa vinavyopitia bandarini?

Darren2019

JF-Expert Member
Nov 23, 2019
1,112
2,379
Wakuu mimi najaribu kuwaza tu kwa wepesi wangu wa akili.

Sote tunajua kwamba mambo ya usalama wa nchi na hasa yale yanayohusu jeshi huwa ni siri ya jeshi japo wananchi tuna nafasi yetu ya kushirikiana na jeshi maana nchi ni yetu sote na jeshi ni mali ya wananchi kikatiba.

Sasa swali langu ni pale kunapotokea maamuzi ya mambo fulani fulani yanayofanywa na viongozi wa serikali afu hayo mambo yakawa yanagusa maslahi ya jeshi kwa namna moja au nyingine, jeshi halina nafasi ya kufanya au halipaswi kufanya lolote?

Kwa mfano hili suala la bandari, tunajua silaha na vifaa mbalimbali vya kijeshi inawezekana vinapitia bandarini, sasa kama bandari zitakuwa zinasimamiwa na wageni badala ya serikali yetu, siri za jeshi letu haziwezi kuvuja?

Naomba kuwasilisha.
 
Jeshi sidhani kama linaweza kuingilia sector za kiutendaji kwa nchi ambazo haziwezi kuingilia military sectors.
 
Indeed certain things require a serious intervention by any means so as to safeguard a country as a whole !! Otherwise things will irreversibly fall apart and with fatal consequences !!
 
Huko ambako hawa Viburi, insensitive kwa hisia za umma madhalimu na wauza nchi wanapotupeleka, may be tutahitaji masoldier Shupavu kama Gamal Abdel Nasser na Muammar Ghadafi, watunusuru kabla hawa wahuni hawajatuuza kutumaliza moja kwa moja

Nasser na vijana wenzao waliingilia kati wakatwaa Suez Canal kibabe wakainusuru Misri dhidi ya mkataba wa kikoloni wa Suez canal.

Ghadafi na vijana wenzie masoldier wakasaidia kurudisha mafuta yao mikononi mwa wananchi.
 
Kiuhalisia Jeshi halina nafasi ya kuhoji kwakua linaendeshwa kisiasa na kupokea maelekezo ya wanasiasa.
Amiri jeshi mkuu ni Rais ambae ni mwanasiasa na mwenyekiti wa ccm, na huyo ndo kamteua CDF mkuu wa majeshi
huyu mwenyekiti wa ccm anampa maelekezo CDF na CDF anapokea Kama amri kutoka kwa amiri jeshi kumbuka jeshini hakuna kuhoji ni kupokea maelekezo tu

ukionekana siyo mwepesi kupokea maelekezo huyu mwenyekiti wa ccm anayo mamlaka ya kukuondoa na kumtea CDF mwingine
 
Sawa, kwaheri.
Alafu ukitaka kujua siri zao wanapoingiza mzigo bandarini vifaa vya vita wafate pale makao makuuu kuna vitu huwa wanafanya kwani hapo nyuma Bandarini ilikuwa iko chini ya Kampuni binafsi vilevile walikuwa wanatumia hizo njia zao
 
Issue ya bandari imeleta kila aina ya nyuzi humu jf
Sisi wengine wasomaji tu

Ova
Mkuu ulifuatlia bunge jana?
Unaweza kunitajia wabunge wataru tu ulioona wewe wana ufahamu na walichokuwa wanachangia?
 
Wakuu mimi najaribu kuwaza tu kwa wepesi wangu wa akili.

Sote tunajua kwamba mambo ya usalama wa nchi na hasa yale yanayohusu jeshi huwa ni siri ya jeshi japo wananchi tuna nafasi yetu ya kushirikiana na jeshi maana nchi ni yetu sote na jeshi ni mali ya wananchi kikatiba...
jeshi linashirikishwa na linamchango mkubwa sana,sema jeshi letu halina mfumo wa kujiweka wazi mbele ya jamii,kuanzia mission wanazofanya mpaka kazi zao ndani na nje ya nchi.

Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo unakuta mpaka mke wa mwanajeshi hajui majukum ya mme wake kambini zaidi ukimuuliza atakwambia tu mme wangu mwanajeshi.

Na ukitaka kulijua hili kuwa wanashiriki ni kwenye kamati zote kuanzia za wilaya mpaka vikao vya kimataifa huwa hawakosi hawa jamaa sema ndo hivyo,wanafanya kazi kubwa pongezi zinaenda kwa wakubwa wenyewe wana remain kuwa kama shadow
 
Back
Top Bottom