Bandari kavu walalamikia TPA..................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,613
Likes
610,864
Points
280

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,613 610,864 280
Bandari kavu walalamikia TPA Send to a friend Friday, 10 December 2010 21:03

Boniface Meena
BANDARI ya Dar es Salaam imelalamikiwa kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi kutokana na kuzidi kwa ukiritimba ndani ya bandari hiyo.

Kutokana na hilo, serikali imetakiwa kuingilia kati hali ya kwa sababu imekuwa ikiendeshwa kisiasa na kusababisha wateja kutaka kukimbia.

Akizungumza ofisini kwake jana, Mwenyekiti wa Chama cha Bandari ya Nchi Kavu (CIDAT), Ashraf Khan, alisema bandari hiyo imeshindwa kupeleka makontena bendari kavu kwa uwiano unaotakiwa.
Khan alisema serikali ndio yenye amri ya makontena kupelekwa bandari kavu, hivyo kitendo cha bandari kushindwa kufanya hivyo ni kukiuka amri iliyotolewa na serikali.

“Makontena ya wateja yamejaa bandari jijini Dar es Salaam na hayatolewi kupelekwa nchi kavu, haya ni mazingira hatarishi ambayo serikali na vyombo vyake inatuchanganya kuhusu utaratibu wao,” alisema Khan.
Alisema nia ya kuwa na bandari kavu ni kuongeza ufanisi Bandari ya Dar es Salaam, mategemeo yao ni kupata ushirikiano kutoka bandari na Kitengo cha Makontena (Ticts).

“Tumepata mafanikio na maendeleo ya kutosha, lakini sasa kuna matatizo kwa sababu, hata mgawo wa makontena tunaopata hautusaidii tumeshindwa kufikia malengo,” alisema Khan.
Alisema kama makontena yangekuwa yanatoka kwa wingi kwa siku saba, wateja wangenufaika kutokana na kutolipishwa gharama za ziada.

“Sababu za msongamano bandarini ni kubwa na tunaweza kulifanyia kazi, lakini upungufu mwingine haukubaliki kwa kuwa unajirudia na biashara ni ngumu,” alisema Khan.Friday, 10 December 2010 21:03

Boniface Meena
BANDARI ya Dar es Salaam imelalamikiwa kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi kutokana na kuzidi kwa ukiritimba ndani ya bandari hiyo.

Kutokana na hilo, serikali imetakiwa kuingilia kati hali ya kwa sababu imekuwa ikiendeshwa kisiasa na kusababisha wateja kutaka kukimbia.

Akizungumza ofisini kwake jana, Mwenyekiti wa Chama cha Bandari ya Nchi Kavu (CIDAT), Ashraf Khan, alisema bandari hiyo imeshindwa kupeleka makontena bendari kavu kwa uwiano unaotakiwa.
Khan alisema serikali ndio yenye amri ya makontena kupelekwa bandari kavu, hivyo kitendo cha bandari kushindwa kufanya hivyo ni kukiuka amri iliyotolewa na serikali.

“Makontena ya wateja yamejaa bandari jijini Dar es Salaam na hayatolewi kupelekwa nchi kavu, haya ni mazingira hatarishi ambayo serikali na vyombo vyake inatuchanganya kuhusu utaratibu wao,” alisema Khan.
Alisema nia ya kuwa na bandari kavu ni kuongeza ufanisi Bandari ya Dar es Salaam, mategemeo yao ni kupata ushirikiano kutoka bandari na Kitengo cha Makontena (Ticts).

“Tumepata mafanikio na maendeleo ya kutosha, lakini sasa kuna matatizo kwa sababu, hata mgawo wa makontena tunaopata hautusaidii tumeshindwa kufikia malengo,” alisema Khan.
Alisema kama makontena yangekuwa yanatoka kwa wingi kwa siku saba, wateja wangenufaika kutokana na kutolipishwa gharama za ziada.

“Sababu za msongamano bandarini ni kubwa na tunaweza kulifanyia kazi, lakini upungufu mwingine haukubaliki kwa kuwa unajirudia na biashara ni ngumu,” alisema Khan.

Forum statistics

Threads 1,204,475
Members 457,330
Posts 28,160,117