Banc ABC ichunguzwe kwanza kabla ya kuuzwa

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,320
Reaction score
117,672
Nimeona Banc ABC inauzwa.

Kabla ya kuuzwa naomba Serikali ichunguze; je, zile pesa zaidi ya Dollar Milioni 100 walizotoa US kwa wajasiriamali wa Tanzania wakati wa Rais Bush.

Ziliwafikia walengwa?

Nafikiri hili muhimu kabla hawajauza Bank na kuacha maswali kwa muwekezaji mpya.
 
THE BOSS

Mbona unakubuka shuka kumeisha kucha
Izo pesa tangia kipindi icho

Bush
Obama
Trump

Izo pesa zitakuwa bado zipo kweli?

Vyovyote vile wakichunguza hawatakosa ukweli zilienda wapi??
 
Nimeona Banc ABC inauzwa.

Kabla ya kuuzwa naomba Serikali ichunguze; je, zile pesa zaidi ya Dollar Milioni 100 walizotoa US kwa wajasiriamali wa Tanzania wakati wa Rais Bush.

Ziliwafikia walengwa?

Nafikiri hili muhimu kabla hawajauza Bank na kuacha maswali kwa muwekezaji mpya.

Mkuu hii bank ilishauzwa 100% ni kama mwaka sasa kwa equity bank
Cha kushangaza ilikua iunganishwe na equity baada ya mauziano ila hizo process zilisimama ghafla

Ila wale wazungu waliokua wamiliki ni wasanii mnoo na lazima wamewaachia wenzao majanga😂😂

Cc Mr English
 
Mkuu hii bank ilishauzwa 100% ni kama mwaka sasa kwa equity bank
Cha kushangaza ilikua iunganishwe na equity baada ya mauziano ila hizo process zilisimama ghafla

Ila wale wazungu waliokua wamiliki ni wasanii mnoo na lazima wamewaachia wenzao majanga😂😂😂

Sasa hivi mchakato ulipo ni wa kuiuza kwa KCB.
 
Ndio najiuliza mmiliki nani au nani haswa anayeiuza bank ABC sasa ni nani? Na kwanini haiwekwi kwamba wamiliki wa bank ABC ni equity
 
Wamiliki ni Atlas Mara ambao HQ yao ipo Kaskazini mwa Afrika. Equity Bank walishaanza mchakato wa kuinunua lakini baadae wakajitoa. Sasa hivi KCB Bank ndio wanainunua BancABC Tanzania kwa 100%. Wanasubiria tu approval ya Shareholders na clearance ya mamlaka husika za Tanzania(BOT)
 
Nimeona Banc ABC inauzwa.

Kabla ya kuuzwa naomba Serikali ichunguze; je, zile pesa zaidi ya Dollar Milioni 100 walizotoa US kwa wajasiriamali wa Tanzania wakati wa Rais Bush.

Ziliwafikia walengwa?

Nafikiri hili muhimu kabla hawajauza Bank na kuacha maswali kwa muwekezaji mpya.

Awamu ya nne? Kama zipo zitakuwa kwenye makabati ya nani?
 
Wamiliki ni Atlas Mara ambao HQ yao ipo Kaskazini mwa Afrika. Equity Bank walishaanza mchakato wa kuinunua lakini baadae wakajitoa. Sasa hivi KCB Bank ndio wanainunua BancABC Tanzania kwa 100%. Wanasubiria tu approval ya Shareholders na clearance ya mamlaka husika za Tanzania(BOT)

Wale majamaa ni wasanii haswa, kumbe equity pamoja na taratibu zote zile walichomoka🤣
BOT tuwashukuru sana kwa kunoa meno yenu
 
Nimeona Banc ABC inauzwa.

Kabla ya kuuzwa naomba Serikali ichunguze; je, zile pesa zaidi ya Dollar Milioni 100 walizotoa US kwa wajasiriamali wa Tanzania wakati wa Rais Bush.

Ziliwafikia walengwa?

Nafikiri hili muhimu kabla hawajauza Bank na kuacha maswali kwa muwekezaji mpya.
Labda nikukumbushe bank inapouzwa ina involve experts wengi sana.....
wana conduct due diligence
hawauziani kama mkate dukani....
na mm ni miongoni mwa wadau
 
Mkuu wamiliki wa hii bank wana issues.... nakumbuka mchakato ulifanyika kwa equity hadi taarifa rasmi ikatolewa kwa management ya bank jinsi ya ku conduct due diligence

Naona haya anafanana na yale ya boss wa Coca-Cola kutoka Kenya na kuishia airport kwa kukosa vibali😁😁
 
Wamiliki ni Atlas Mara ambao HQ yao ipo Kaskazini mwa Afrika. Equity Bank walishaanza mchakato wa kuinunua lakini baadae wakajitoa. Sasa hivi KCB Bank ndio wanainunua BancABC Tanzania kwa 100%. Wanasubiria tu approval ya Shareholders na clearance ya mamlaka husika za Tanzania(BOT)
Benki hizi zina mambo mengi sana hasa za kibongo pana upigaji mkubwa sana, ukiona benki inauzwa usikurupuke tu kununua, watu wanafanya "Window in accounting" ili tu uingie mkenge!?
Niliona kwa taasisi moja ya mikopo ipo al dua tower walitaka kununua benki wilaya ya Mwanga walikutana na ufundo mzito, Npl za kumwaga na hazieleweki taarifa kibao zimepotea watu wamefanya yao, ndio maana sikushangaa kuona wanaungana na kujiita Mwanga wa uhakika, hata benki abc tatizo #npl kibao pale, wanapumulia gesi ndio maana equity walijitoa baada ya kuona mzigo mzito anyway acha KCB abebe mzigo uenda anauweza.
Sisi watu weusi tunashida sana kwakweli kwenye kuwa wakweli uongo umetujaa mno.
 
Wakati mwingine unakuta minority shareholders ambao ni matapeli wanacheza hizi deal kotekote.... Kisha wanajifanyia yao wakishamaliza wanasukuma mzigo upande mwingine na bado wanaendelea kula.

Baadhi ya investors na professionals ambao ni matapeli wako smart sana kwenye huo utapeli wao na wana influence kubwa sana
 
Wamiliki ni Atlas Mara ambao HQ yao ipo Kaskazini mwa Afrika. Equity Bank walishaanza mchakato wa kuinunua lakini baadae wakajitoa. Sasa hivi KCB Bank ndio wanainunua BancABC Tanzania kwa 100%. Wanasubiria tu approval ya Shareholders na clearance ya mamlaka husika za Tanzania(BOT)
Questions:
wamiliki wa benki uzwa ni nani?
Kwanini wanataka kuiuza?
 
Back
Top Bottom