badison
JF-Expert Member
- May 29, 2015
- 1,450
- 2,757
Balozi wa Saudi Arabia nchini Romania ambaye anakabiliwa na tuhuma ya kumbaka na kumuua sekretari amepewa masaa 48 afungashe virago na kuondoka nchini humo.
Mtandao wa Habari wa al-Sharq al-Awsat unaripoti kwamba, Abdulrahman bin Ibrahim Al-Rassi balozi wa Saudi Arabia nchini Romania amembaka na kisha kumuua sekretari wake ambaye ni raia wa Romania. Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Romania inamtuhumu balozi huyo wa Saudia kwamba, alimbaka Ivan Wilisco binti wa Kiromania mwenye umri wa miaka 25 na aliyekuwa akifanya kazi katika ubalozi huo kama sekretari wa balozi.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, uchunguzi wa kitiba uliofanywa unaonesha kwamba, binti huyo alibakwa na kisha kunyongwa kwa kutumia mkanda.
Jana Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Romania ilimpa mwanadiplomasia huyo wa Saudia anayekabiliwa na tuhuma za muaji na utovu wa maadili muda wa masaa 48 awe ameondoka nchini humo.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, katika kesi nyingine mfanyakazi mwingine wa ndani wa Kiromania mapema mwaka huu alibakwa, kupigwa na kudhalilishwa katika nyumba ya balozi wa Saudia mjini Bucharest.
Chanzo: Iran Swahili Radio