Balozi Seif Ali Iddi atoa Taarifa Rasmi ya Maadhimisho yaMikaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar

Je amekwenda kinyume na rais wa muungano katika utaratibu wa kusherekea muungano.

  • nice

  • greate

Results are only viewable after voting.

samtz1

JF-Expert Member
Nov 8, 2015
1,197
1,370
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Maadhimisho ya Sherehe za kutimia Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yatafanyika kama kawaida na kupangwa kuanza rasmi leo jumapili ya Tarehe 3 Januri 2016.
Alisema Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha kwamba katika muda wote wa maandamisho hayo kunakuwa na hali ya utulivu na usalama mkubwa katika maeneo yote ya Visiwa vya vya Unguja na Pemba.
Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar alisema hayo wakati akitoa Taarifa rasmi ya ratiba ya maadhimisho ya sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar mbele ya Wana Habari hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Alisema suala la upande wa Upinzani kuzisusia sherehe za Mapinduzi kwa kisingizio cha Rais aliyepo madarakani si halali ni muendelezo wa kuwapotosha Wananchi walio wengi nchini.
Balozi Seif alifafanua kuwa Rais wa sasa Dr. Ali Mohammed Shein ataendelea kuwa rais hadi yule atakayechaguliwa rasmi na kihalali na Wananchi ale kiapo kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kama ilivyokwishatolewa ufafanuzi na wanasheria walio wengi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba Miradi yote ya Maendeleo ipatayo 24 ambapo 16 ikiwa imekamilika na Minane inatarajiwa kuwekwa mawe ya msingi imehusishwa katika maadhimisho hayo itakayoanza Jumatatu ijayo.
Alisema madhimisho hayo yataanza rasmi leo Jumapili ikiwa ni siku maalum kwa kazi za usafishaji wa masingira katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba ukilenga zaidi katika sehemu za kutolea huduma za kijamii kama Hospitali, Vituo vya Afya pamoja na masoko.
Mwenyekiti huyo wa Halmashauri ya Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar alifahamisha kwamba ingawa zoezi hilo hufanyika kila zinapoanza sherehe za Mapinduzi lakini mwaka huu juhudi malum zinapaswa kuchukuliwa ili kuhakikisha maeneo yote yanakuwa katika hali ya usafi muda wote.
Akigusia suala la hatma ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar ambalo limekuwa agenda kubwa kwa baadhi ya watu wakiwemo hata wanasiasa nchini wakiendelea kupotosha Wananchi Balozi Seif alisema Taarifa rasmi ya vikao vinavyowakutanisha Viongozi wa juu kulijadili suala hilo itatolewa rasmi mara baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo.
Hata hivyo Balozi Seif alitanabahisha kwamba Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar { ZEC } kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ndio yenye mamlaka ya kuendesha na kusimamia uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.
Alisema kwa vile tume hiyo kupitia Mwenyekiti wake haikuridhika na mazingira yaliyojichomoza wakati wa zoezi la kupiga kura na kulazimika kufuta Uchaguzi pamoja na matokeo yake yote Taasisi hiyo hiyo ndio yenye uwezo wa kuitisha uchaguzi mwengine kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar.
Akijibu baadhi ya maswali ya Waandishi wa Habari Balozi Seif alisema katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 iko wazi na kutoa mamlaka kwa tume ya uchaguzi ya Zanzibar kupanga uchaguzi mwengine kufuatia kufutwa kwa ule wa mwezi oktoba mwaka 2015.
Chanzo mpekuzi blog.
 
Attachments

  • 1.jpg
    1.jpg
    21.6 KB · Views: 37

Zanzibar ni nchi ya kimapinduzi, hatutaitoa kamwe kwa vipande vya karatasi, mmekosa 1995 kushika dola hampati tena labda mpindue, na sisi tumeshika dola........(by mwanasiasa mkongwe wa CCM Zanzibar)
 
point yako ina uhusiano wowote na habari hyo
 
Nilidhani mwanamaendeleo mkongwe ,kumbe mwanasiasa mkongwe. Hunampya .unaomba upindiliwe ili iweje .watu hawatauana tena huko zanzibar.dhamira yako ya kuona watu wakiuana tena haitotimia
 
Jata mleta uzi unatakiwa utumie akili yako mwenyewe siyo utumie masabuli,kwa sasa hivi znz haina balaza la mawazili lilisha vunjwa kitambo,balozi seif Idd alikua mbunge kwenye bunge au balaza la wawakilishi
lililovunjwa,ungeandika,aliyekuwa makamu wa pili wa Rais wa znz au aliyekuwa Rais wa Znz.Tatizo la znz kama siyo Tanganyika iliyojifunika blanketi ya Tanzania tena mchana wa jua kali bila kuona hata joto,wazanzibar wangeweza kumaliza matatizo yao wenyewe,MaCCM ya Tanganyika ndo machawi na yatawaletea shida wazanzibar.
 
Hivi kuna mtu yeyote anatilia maanani kauli za seif idd ndani au nje ya nchi hii ?
 
Jata mleta uzi unatakiwa utumie akili yako mwenyewe siyo utumie masabuli,kwa sasa hivi znz haina balaza la mawazili lilisha vunjwa kitambo,balozi seif Idd alikua mbunge kwenye bunge au balaza la wawakilishi
lililovunjwa,ungeandika,aliyekuwa makamu wa pili wa Rais wa znz au aliyekuwa Rais wa Znz.Tatizo la znz kama siyo Tanganyika iliyojifunika blanketi ya Tanzania tena mchana wa jua kali bila kuona hata joto,wazanzibar wangeweza kumaliza matatizo yao wenyewe,MaCCM ya Tanganyika ndo machawi na yatawaletea shida wazanzibar.
Punguza jazba
 
Maalim Seif ni shabiki Mkubwa sana wa CCM Zanzibar, baada ya kuona CCM ina hali mbaya akaleta igizo la kujitangaza Mshindi ili Jecha akasirike afute Uchaguzi apate kula pesa za Kamati ya kusuluhisha Gogoro feki
 
Back
Top Bottom