Balozi Mulamula: Pamoja na hatua iliyochukuliwa na Denmark, ni matarajio ya Tanzania kuwa Serikali ya Denmark itaendelea kushirikiana na Tanzania

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,064
2,000
Dar es Salaam.

Serikali ya Tanzania imeeleza kusikitishwa na hatua ya Serikali ya Denmark kuamua kufunga shughuli za Ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo mwaka 2024.

Denmark jana ilitangaza uamuzi huo ambao ulihusishwa na mkakati wao mpya wa masuala ya mambo ya nje. Mbali na Tanzania pia nchi hiyo itafunga ubalozi wake nchini Argentina, Ubalozi mdogo wa Chongqing nchini China na ujumbe wa biashara huko Barcelona (Uhispania).

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula leo Jumamosi Agosti 28, 2021 amesema hatua hiyo ya Denmark inasikitisha ikizingatiwa kuwa hivi karibuni Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa ikifanya jitihada za kufufua na kuimarisha diplomasia na uhusiano wa nchi rafiki ikiwemo Denmark.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo imeeleza kulikuwa na jitihada za kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini pamoja na kuimarisha demokrasia na utawala wa sheria.

Aidha taarifa hiyo inaeleza Balozi Mulamula jana alifanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na Waziri wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Denmark, Flemming Mortensen ambapo walikubaliana kuendelea kushirikiana na Mortensen anatarajia kuzulu nchini siku zijazo.

“Pamoja na hatua iliyochukuliwa na Denmark, ni matarajio ya Tanzania kuwa Serikali ya Denmark itaendelea kushirikiana na Tanzania kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuunga mkono ajenda za Tanzania katika Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa na majukwaa mengine ya kimataifa,” inaeleza taarifa hiyo.
 
peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
4,836

Balozi Mulamula: Tanzania IPO uchumi wa Kati.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
15,092

Kuunga mkono kwenye kubambikiziana kesi, dhulumati, nyungu, ukiukwaji wa haki za binadamu na vya namna hiyo ni big NO!
 
captain dunga

JF-Expert Member
Jun 5, 2014
215
500
"Kufufua na kuimarisha Diplomasia"

kwa maana hiyo Diplomasia ilikufa.?? Nani aliiua.??
inakuaje kama aliyepita aliua Diplomasia na huyu wa sasa anasema yeye na 'Hayati' ni kitu kimoja.??
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
58,419
2,000
1. Denmark vyama vya mrengo wa kukataa kutoa misaada nje vimechukua madaraka.
2. Tanzania tumesaidiwa miaka mingi na hatuelekei kusaidika.
3. Rais aliyepita alijifungia sana na kukataa kupalilia mahusiano ya kimataifa.
4. Nchi inaendeshwa kijinga sana, hususan miaka 6 iliyopita. Tanzania ambayo wa Dane walifikiria itajuwa tangu enzi za Nyerere, na ilivyokuja kuwa, ni vitu viwili tofauti.
5. Wa Dane wameona hakuna tija kuendelea kuwa na Ubalozi Tanzania.
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
55,883
2,000
"Kaa kimya, tena wewe ndiyo nilikua nakutafuta nitakuzalilisha wewe na msg zako ninazo hapa" in Haji Manara'voice
 
Josh J

JF-Expert Member
Mar 16, 2021
1,798
2,000
1. Denmark vyama vya mrengo wa kukataa kutoa misaada nje vimechukua madaraka.
2. Tanzania tumesaidiwa miaka mingi na hatuelekei kusaidika.
3. Rais aliyepita alijifungia sana na kukataa kupalilia mahusiano ya kimataifa.
4. Nchi inaendeshwa kijinga sana, hususan miaka 6 iliyopita. Tanzania ambayo wa Dane walifikiria itajuwa tangu enzi za Nyerere, na ilivyokuja kuwa, ni vitu viwili tofauti.
5. Wa Dane wameona hakuna tija kuendelea kuwa na Ubalozi Tanzania.
Bado hawajaondoa.

Wataondoa ubalozi wao hapa nchini mwaka 2024.as of now bado wapo!
 
kipara20

JF-Expert Member
Jul 30, 2021
1,319
2,000
1. Denmark vyama vya mrengo wa kukataa kutoa misaada nje vimechukua madaraka.
2. Tanzania tumesaidiwa miaka mingi na hatuelekei kusaidika.
3. Rais aliyepita alijifungia sana na kukataa kupalilia mahusiano ya kimataifa.
4. Nchi inaendeshwa kijinga sana, hususan miaka 6 iliyopita. Tanzania ambayo wa Dane walifikiria itajuwa tangu enzi za Nyerere, na ilivyokuja kuwa, ni vitu viwili tofauti.
5. Wa Dane wameona hakuna tija kuendelea kuwa na Ubalozi Tanzania.

chanzo cha haya yote JPM
 
komrade

Senior Member
Sep 26, 2019
179
250
Pamoja na misada yao, wamekuwa vinara wa kuhamasisha mambo ya chumbani.

Hiyo 2024 ni mbali sana, waondoke tu hata mwaka huu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom