Dkt. Mahiga ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum na ITV ambapo amesema baada ya mkutano wa SADC uliofanyika hivi karibuni Addis Ababa walitegemea utekelezaji wa makubaliano yaliyoafikiwa uanze.
Aidha Balozi Mahiga amesema juhudi za kuwapatanisha Rais wa Sudani ya Kusini Silva Kiir na makamu wake Bw.Riek Machar zilichukuwa zaidi ya mwaka mmoja na kwamba kuingia kwao kwenye jumuiya ya Afrika Mashariki kutachangia kuharakisha mapatano.
Zaidi ya watu 200 wameuawa katika mapigano yaliyoanza alhamisi iliyopita kati ya majeshi yanayowatii viongozi hasimu Rais Salva Kiir na makamu wake Bw Riek Machar.
Wakati huo huo Balozi Mahiga amepokea msaada wa Madawati kutoka jumuiya ya Maboora ambapo amesema utekelezaji wa elimu bure umeanza na changamoto nyingi ikiwemo ya madawati.
Chanzo: ITV
======
Kwa upande wangu naipongeza sana serikali kwa hatua hii kwani Tanzania tumekuwa kisiwa cha amani na utamaduni wetu ni kusaidia nchi nyingine toka uhuru.