Balozi Jaka Mwambi alisahaulika kabla ya mauti kumkuta

GARETHBALE

Member
Dec 22, 2013
76
332
BALOZI JAKA MWAMBI ALISAHAULIKA KABLA YA UMAUTI KUMFIKA.

Nichukie fursa hii kuwapa pole familia,marafiki, wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na watumishi wote wa umma waliowahi kufanya kazi na marehemu Balozi Jaka Mwambi.

Balozi Jaka Mwambi sio jina geni kwenye masikio ya wengi.Wazee wa rika lake,watu wa makamu na sisi vijana wenye kufuatilia masuala ya siasa na diplomasia kwakweli hakuwa mgeni machoni au masikioni kwetu.

Hakuwa mwanasiasa wa kuongea sana.Alikuwa mtu wa "field" aliyeshika nyadhifa zake bila kuacha alama ya makandokando yoyote mabaya.

Binafsi kama kijana mwenye kupenda siasa nilianza kumjua marehemu Balozi Jaka Mwambi mwaka 2001.Enzi hizo alikuwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa.Familia yake na yetu ni marafiki wakubwa.

Lakini kumfuatilia zaidi katika nyanja ya siasa ni hadi pale alipoteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM(bara).Alipokuwa Mkuu wa mikoa tofauti kama vile Rukwa,Tanga na Iringa sikuweza kumfuatilia sana katika ulingo wa siasa.Niliona alipata uteuzi tu kama zawadi,kumbe sikuwa sahihi.

Na hivi ndivyo nilivyomjua marehemu Balozi Jaka Mwambi kabla ya kifo chake:

Alikuwa rafiki mkubwa sana na rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete.Walisoma wote shule ya sekondari Kibaha(A level)na kujiunga pamoja kwenye chuo kikuu cha Dar es salaam na kusomea masomo ya uchumi.

Baada ya kuhitimu masomo yao ya chuo kikuu walijiunga pamoja na Jeshi la Wananchi(Tpdf)na kutunikiwa vyeo vya uafisa.Marehemu Balozi Jaka Mwambi alifika katika cheo cha ukapteni hadi anastaafu jeshini.

Kuna "tweet" ya rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu ukaribu wake na marehemu Balozi Jaka Mwambi.Wanaojua mahusiano yao watakuwa wameelewa ni kwa namna gani rais mstaafu kaguswa na msiba huu.

Lakini inasikitisha namna chama tawala na serikali ilivyoukalia kimya msiba huu.Tena kwa mtu ambaye amehudumu katika nyadhifa mbalimbali kwa uadilifu mkubwa sana.

Hatuoni magazeti yakiandika.Hatusikii redio zikitangaza.Hatuoni luninga ya taifa ikiweka katika taarifa yao ya habari msiba huu.Ni kama marehemu hakuwa sehemu ya utumishi wa umma na chama.

Huyu ni Mkuu wa wilaya tofauti mstaafu,huyu ni Mkuu wa mikoa tofauti mstaafu,huyu ni mwanajeshi mstaafu,huyu ni Balozi mstaafu lakini kubwa zaidi huyu ni Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa chama tawala upande wa bara.

Iko wapi taarifa ya Hamphrey Polepole,iko wapi taarifa ya Wizara ya mambo ya nje,iko wapi taarifa ya jeshi?Tunafeli wapi?Utu unapotea hata kwa aliyetumikia nchi kwa uaminifu mkubwa mno.

Tangu astaafu hakuwahi kusikika mahali popote.He was a low profile Comrade.Lakini hii haina maana jamii haipaswi kujua kuhusu yeye.Inasikitisha.

Kwaheri Balozi Jaka Mwambi.Tukujuao tutakuenzi milele.Mungu akulaze mahali pema peponi,amina.

Imeandikwa na:
Ofisi ya wabobezi wa siasa.
 
Mtu akishastaafu inatosha kila mstaafu akifariki tukitaka taasisi alizofanya kazi zitoe matangazo na kuuvalia njuga msiba nchi itakuwa hoi hatutaweza kufanya kazi kutwa yatakuwa matangazo ya misiba na shughuli za misiba tu leo kafa mstaafu huyu alitumikia kwa uaminifu kesho mwingine ohh naye alitumikia kwa uaminifu !!!!

Mtu akishastaafu na akalipwa chake mengine ni yake yeye,majirani,ndugu marafiki na waumini wenzie anakosali taasisi alizofanyia kazi hazitakiwi kuwajibika kwake milele kisa tu eti alishawahi kufanya kazi kwao!!!!

Tukubali ukishatoka kazini umetoka huko ulikotoka si wajibu wao kuwajibika kwako Tena
 
Usilete urafiki wenu wa kifamilia kwenye mambo ya kisiasa,wangapi wametumikia nchi hii na wanapokufa tunakuja kujua baada ya miaka kupita ndio tunajua ala komredi fulani kesha tangulia mbele ya haki,hizo porojo za kutaka kumulikwa kwenye runinga ndio zitamfanya aenziwe?

Mambo ya kusema sijui katumikia sana chama /serikali ni ujinga tu unakusumbua ,je alitumikia bure?si ilikuwa ni ajira,kila mtu katumikia nchi hii kwa nafasi yake,we nnda tu kaomboleza huko kwake ,kila mmoja ameitumikia nchi pamoja na hata akina Kingwendu kwa wakati wao nao wametumikia nchi hii kwa kuitangaza.
 
Kwahiyo shida yako aandikwe na magazet kuwa kafariki ndo roho yako itulie?

Shwain
Mkuu wanapopewa vyeo,marupurupu hatualikani bali wanaofaidi ni wanafamilia wao,leo hii kutulazimisha sote tumuenzi ni kukosa busara,tutawaenzi wangapi nchi hii?kila mtu ana mchango wake kwa nchi hii.naona jamaa akiona kwenye runinga basi roho yake itakuwa kwatu,kufahamiana kwao isiwe tabu kwetu,
 
usilete urafiki wenu wa kifamilia kwenye mambo ya kisiasa,wangapi wametumikia nchi hii na wanapokufa tunakuja kujua baada ya miaka kupita ndio tunajua ala komredi fulani kesha tangulia mbele ya haki,hizo porojo za kutaka kumulikwa kwenye runinga ndio zitamfanya aenziwe?mambo ya kusema sijui katumikia sana chama /serikali ni ujinga tu unakusumbua ,je alitumikia bure?si ilikuwa ni ajira,kila mtu katumikia nchi hii kwa nafasi yake,we nnda tu kaomboleza huko kwake ,kila mmoja ameitumikia nchi pamoja na hata akina Kingwendu kwa wakati wao nao wametumikia nchi hii kwa kuitangaza.
Shetani hana rafiki
 
BALOZI JAKA MWAMBI ALISAHAULIKA KABLA YA UMAUTI KUMFIKA.

Nichukie fursa hii kuwapa pole familia,marafiki, wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na watumishi wote wa umma waliowahi kufanya kazi na marehemu Balozi Jaka Mwambi.

Balozi Jaka Mwambi sio jina geni kwenye masikio ya wengi.Wazee wa rika lake,watu wa makamu na sisi vijana wenye kufuatilia masuala ya siasa na diplomasia kwakweli hakuwa mgeni machoni au masikioni kwetu.

Hakuwa mwanasiasa wa kuongea sana.Alikuwa mtu wa "field" aliyeshika nyadhifa zake bila kuacha alama ya makandokando yoyote mabaya.

Binafsi kama kijana mwenye kupenda siasa nilianza kumjua marehemu Balozi Jaka Mwambi mwaka 2001.Enzi hizo alikuwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa.Familia yake na yetu ni marafiki wakubwa.

Lakini kumfuatilia zaidi katika nyanja ya siasa ni hadi pale alipoteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM(bara).Alipokuwa Mkuu wa mikoa tofauti kama vile Rukwa,Tanga na Iringa sikuweza kumfuatilia sana katika ulingo wa siasa.Niliona alipata uteuzi tu kama zawadi,kumbe sikuwa sahihi.

Na hivi ndivyo nilivyomjua marehemu Balozi Jaka Mwambi kabla ya kifo chake:

Alikuwa rafiki mkubwa sana na rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete.Walisoma wote shule ya sekondari Kibaha(A level)na kujiunga pamoja kwenye chuo kikuu cha Dar es salaam na kusomea masomo ya uchumi.

Baada ya kuhitimu masomo yao ya chuo kikuu walijiunga pamoja na Jeshi la Wananchi(Tpdf)na kutunikiwa vyeo vya uafisa.Marehemu Balozi Jaka Mwambi alifika katika cheo cha ukapteni hadi anastaafu jeshini.

Kuna "tweet" ya rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu ukaribu wake na marehemu Balozi Jaka Mwambi.Wanaojua mahusiano yao watakuwa wameelewa ni kwa namna gani rais mstaafu kaguswa na msiba huu.

Lakini inasikitisha namna chama tawala na serikali ilivyoukalia kimya msiba huu.Tena kwa mtu ambaye amehudumu katika nyadhifa mbalimbali kwa uadilifu mkubwa sana.

Hatuoni magazeti yakiandika.Hatusikii redio zikitangaza.Hatuoni luninga ya taifa ikiweka katika taarifa yao ya habari msiba huu.Ni kama marehemu hakuwa sehemu ya utumishi wa umma na chama.

Huyu ni Mkuu wa wilaya tofauti mstaafu,huyu ni Mkuu wa mikoa tofauti mstaafu,huyu ni mwanajeshi mstaafu,huyu ni Balozi mstaafu lakini kubwa zaidi huyu ni Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa chama tawala upande wa bara.

Iko wapi taarifa ya Hamphrey Polepole,iko wapi taarifa ya Wizara ya mambo ya nje,iko wapi taarifa ya jeshi?Tunafeli wapi?Utu unapotea hata kwa aliyetumikia nchi kwa uaminifu mkubwa mno.

Tangu astaafu hakuwahi kusikika mahali popote.He was a low profile Comrade.Lakini hii haina maana jamii haipaswi kujua kuhusu yeye.Inasikitisha.

Kwaheri Balozi Jaka Mwambi.Tukujuao tutakuenzi milele.Mungu akulaze mahali pema peponi,amina.

Imeandikwa na:
Ofisi ya wabobezi wa siasa.
AMEKUJA FARAO ASIYEMFAHAMU YOSEPH
 
Balozi Jaka Mwambi alipata kuiwakilisha Tanzania Urusi.

Pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki.
 
Hii nakumbuka baada ya Patrick Chokala, ndio akaja Balozi Jaka Mwambi, Pale mitaa ya Bol'shaya Nikitskaya ulitsa 51.
 
Back
Top Bottom