Balozi Iddi afichua mahusiano mabaya ma-RC, ma-RAS

Balozi Iddi afichua mahusiano mabaya ma-RC, ma-RAS

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,933
Balozi-Iddi--July22-2014.jpg

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi

Balozi Iddi afichua mahusiano mabaya ma-RC, ma-RAS

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amewataka wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa nchini kuacha misuguano ya kiutendaji baina yao, kwani vitendo hivyo vimeleta dosari kwenye ofisi zao.

Alitoa agizo hilo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya uongozi kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa --ma-RC na ma-RAS kutoka mikoa yote nchini, jana jijini Dar es Salaam.

Balozi Iddi alisema kumekuwapo changamoto ya mahusiano na muingiliano wa kiutendaji miongoni mwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala na kuwasababisha baadhi yao kuamua kufanya kama wanavyoona.

Alisema misuguano hiyo imewafanya baadhi ya viongozi kupeleka malalamiko ama kwa Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) au Katibu Mkuu Tamisemi.

"Ninyi viongozi, ambao mmekabidhiwa dhamana kubwa katika mikoa yenu, ambako ndiko Watanzania wote wanaishi, ndiyo wawakilishi wa Rais. Uwajibikaji na mshikamano wenu ndiyo sababu pekee itakayowezesha Watanzania kuboresha maisha yao," alisema Balozi Iddi.

Aliongeza: "Kumekuwa na changamaoto ya mahusiano na muingiliano wa kiutendaji miongoni mwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa. Hali hii imesababisha baadhi yenu kuamua kufanya anavyoona kwake inafaa."

Alisema wakuu wa mikoa ni viongozi wa kisiasa, huku makatibu tawala wa mikoa wakiwa ni watendaji wakuu kwenye ngazi hiyo, hivyo akataka kuwapo uwazi wa mawasiliano baina yao, mshikamano, kuacha kushikilia misimamo na kutekeleza majukumu yao kwa muingiliano.

Pia aliitataka Taasisi ya Uongozi nchini, ambayo ndiyo waratibu wakuu wa mafunzo hayo, kuandaa mafunzo mengine ya jinsi hiyo kwa ajili ya wakuu wa wilaya na makatibu tawala wa wilaya pamoja na wakurugenzi wao kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja, alisema mafunzo hayo yanalenga kuimarisha mawasiliano, mahusiano na muingiliano baina ya wakuu wa mikoa na makatibu tawala wa mikoa pamoja na kubadilishana uzoefu wa kiutendaji kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa Ghasia, alisema mafunzo hayo ni kwa ajili ya mikoa yote nchini, lakini ni mikoa 20 pekee hadi jana ndiyo iliyothibitisha kuwapo, huku mingine ikiwa na udhuru maalumu.

Alisema mikoa ambayo haikuhudhuria kwa upande wa Tanzania Bara itashiriki katika mafunzo mengine yatakayotolewa hivi karibuni kwa upande wa Zanzibar.

Aliungana na Balozi Iddi kuwataka wakuu wa mikoa na makatibu tawala kuheshimiana kwa kuwa kila mmoja ana nafasi yake.

Chanzo:Nipashe
 
Semina ya nini sasa ma mikuu ya mikoa ni yale yale miaka nenda miaka rudi.

Toka wadogo yapo tu.

Bora tupate katiba mpya, tufute ma vyeo ya upendeleo.
 
Ushauri aliowapa Makamu wa Rais ndiyo suluhu na siyo vinginevyo.
 
Semina ya nini sasa ma mikuu ya mikoa ni yale yale miaka nenda miaka rudi.

Toka wadogo yapo tu.

Bora tupate katiba mpya, tufute ma vyeo ya upendeleo.

Nani alikufundisha kishwahili. Halafu wewe unaishi kwa matusi ya JF nini, manake kila saa, kila siku ni matusi tu , mwezi wa toba huu mkuu usije ukaanza kutafuta mchawi mungu atakapoanza kukuchapa fimbo.
 
Kuna nchi zilishafuta nafasi hizi za watawala kisiasa maana wanaleta tu mitafaruku. Hawa makatibu taweala wa mikoa ndio wenye ujuzi katika utawala na utendaji, hizi nafasi za ukuu wa wilaya na mkoa ni kukirimiana na wanasababisha mitafaruku tu.
 
Nani alikufundisha kishwahili. Halafu wewe unaishi kwa matusi ya JF nini, manake kila saa, kila siku ni matusi tu , mwezi wa toba huu mkuu usije ukaanza kutafuta mchawi mungu atakapoanza kukuchapa fimbo.
1.thatha ni sasa
2.Kishwahili ni Kiswahili,
3.mungu ni Mungu
4.Manake ni maanayake

Kajifunze halafu Jipange Mburula
 
kwani huyo Seif ni kiongozi pia huku kwetu? nijuavyo ni kiongozi kule nchi jirani. mbona hatujawahi muona Mh. Pinda akiwa huko kwao kwenye shughuli kama hizi?
kuhusu hao wakuu wa mikoa wangefuta hivyo vyeo hata leo. wanatumia kodi zetu bila sababu za msingi. Ma-ras watosha mikoani na ma-das watosha mawilayani. natamani katiba mpya ingeanza kufanya kazi leo tuusahau huu upuuzi.
 
i agree with you Abunuwas. hivi vyeo ni upuuzi mtupu. wanafanya kazi ya kulinda maslahi ya ccm na mafisadi basi. angalia sehemu nyingi zenye migodi, pia sehemu zenye kilimo cha mashamba makubwa, ma rc na dc wamesababisha taharuki kubwa mpaka vifo vya raia.
 
Too Much presidential apointees in this country.

Mwisho wa siku wanavimbishiana vifua.

Yale yake ya waziri na Katibu mkuu.

Bullshitsssssssss
 
Kama kawaida yake, BALOZI MKAAZI WA TANGANYIKA VISIWANI ZANZIBAR.....
 
kwani huyo Seif ni kiongozi pia huku kwetu? nijuavyo ni kiongozi kule nchi jirani. mbona hatujawahi muona Mh. Pinda akiwa huko kwao kwenye shughuli kama hizi?
kuhusu hao wakuu wa mikoa wangefuta hivyo vyeo hata leo. wanatumia kodi zetu bila sababu za msingi. Ma-ras watosha mikoani na ma-das watosha mawilayani. natamani katiba mpya ingeanza kufanya kazi leo tuusahau huu upuuzi.

unashangaa nini mjomba.? Kwani hujui....? huyo ni balozi wenu visiwani Zanzibar, amerudi nyumbani kutekeleza majukumu ya taifa lake
 
Nani alikufundisha kishwahili. Halafu wewe unaishi kwa matusi ya JF nini, manake kila saa, kila siku ni matusi tu , mwezi wa toba huu mkuu usije ukaanza kutafuta mchawi mungu atakapoanza kukuchapa fimbo.
Ma mikuu ya mikoa ni Yale Yale anamaanisha ni mibaya kama nunda na imekaa kwenye nafasi hizo miaka nenda rudi bila ufanisi. Yuko sahihi kabisa kiswahilically
 
Watu waleteane bifu huko halafu nyie mlete semina kwa kodi za wananchi?

Only in Tanzania
 
Hili lilihitaji semina????

Nchi ya malalamiko sasa!!!!
Hao si wa kutumiwa waraka tu jamani!!!!
 
Huyo balozi Idd ni nani huku Tanganyika hadi aje kusema hayo huku?
 
Back
Top Bottom