Balozi huyu wa CCM amenishangaza sana...

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Jana kwenye sherehe ya jirani yangu nilikuwa na Mjumbe wa shina wa CCM. Mwaka 2010, baada ya Dk Batilda kushindwa na Lema ktk ubunge, alisikitika sana na kudai kuwa kama Batilda angeshinda, basi angemalizia nyumba yake (angepata pesa nyingi!).
Jana nikataka kujua maoni yake kuh kuengulewa kwa Lema na Mahakama.
Alichonijibu kilinishtua sana! Anasema hata uchaguzi urudiwe wao (CCM) hawatashinda, alienda mbali zaidi kuwa ukirudiwa atawapigia CDM kura lkn bendera ya CCM ataiacha iendelee kupepea nyumbani.
 
Ni vizuri amejitambua,hukumu ya Lema ni ya kipuuzi mno imeshusha hadhi ya Mahakama,unajua wananchi walikuwa wanachukia Polisi,Usalama wa Taifa,serikali lakini angalau imani ilibaki kwenye chombo cha haki Mahakama,sasa CDM watazunguka nchi nzima wakiwasasambula wananchi jinsi mahakama inavyotumiwa na viongozi waroho sasa nisikilizie,wananchi wakijua hakuna wakuwatetea mwisho wake nini
 
Hahaha huyu Balozi ni kama shabiki wa Simba kwenye jukwaa la Yanga...
 
Jana kwenye sherehe ya jirani yangu nilikuwa na Mjumbe wa shina wa CCM. Mwaka 2010, baada ya Dk Batilda kushindwa na Lema ktk ubunge, alisikitika sana na kudai kuwa kama Batilda angeshinda, basi angemalizia nyumba yake (angepata pesa nyingi!).
Jana nikataka kujua maoni yake kuh kuengulewa kwa Lema na Mahakama.
Alichonijibu kilinishtua sana! Anasema hata uchaguzi urudiwe wao (CCM) hawatashinda, alienda mbali zaidi kuwa ukirudiwa atawapigia CDM kura lkn bendera ya CCM ataiacha iendelee kupepea nyumbani.

Wako wengi sana hao, we tulia tu. Kuna mmoja anaitwa kuti kavu, yuko hivyohivvyo.
 
Back
Top Bottom