Vita CCM yamgusa mtoto wa JK, Ikulu

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Vita CCM yamgusa mtoto wa JK, Ikulu Send to a friend
Saturday, 22 October 2011 22:25
0diggsdigg

jk-miwani.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete

MAKUNDI MAWILI YATUNISHIANA MISULI URAIS 2015
Na Waandishi Wetu
MINYUKANO inayohusisha makundi mawili ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa imeanza kugusa taasisi ya Urais baada ya jina la Rais Jakaya Kikwete, mwanawe, Ridhwan na Ikulu kuanza kuhusishwa katika malumbano yanayoendelea.Jina la Rais na Ikulu limeanza kutajwa hivi karibuni katika mgogoro ulioanza baada ya moja ya kundi la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa chama hicho, (UVCCM), likiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wake wa taifa, Benno
Malisa na baadhi ya wenyeviti wa mikoa wa umoja huo, kuzuiwa na Jeshi la Polisi kufugua matawi mkoani Arusha, kwa kile kilichodaiwa maelekezo ya mtoto wa kigogo.

Ingawa Malisa na wenzake hawakutaja jina la mtoto huyo wa kigogo
walipohutubia mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Hospitali ya St. Thomas mjini Arusha, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James Ole Millya alimtaja,Ridhwani Kikwete kuhusika na njama za kuzuia shughuli hiyo alipozungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Lash Garden, walikofikia viongozi hao.

“Ingawa polisi wanadai kutunyima kibali cha maandamano ya kufungua mashina ya Umoja wa Vijana na mkutano wa hadhara kwa kile wanachodai taarifa za kiintelijensia kugundua kutatokea uvunjifu wa amani, tumepata habari kuwa Ridhwan ndiye kapiga simu kuelekeza tunyimwe.Sisi tutaendelea na shughuli yetu liwalo na liwe, wacha watupige mabomu kama Chadema,” alisema Millya.

Millya pia alimshambulia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauye na kumtaja kama ugonjwa wa saratani kwa chama hicho na kuonya kwamba kama hatadhibitiwa, atasababisha anguko la chama.

Millya alizungumzia pia tamko la Baraza la UVCCM Mkoa wa Pwani lilotolewa mapema mwaka huu na kuzua mtafaruku miongoni mwa wanaCCM kuwa rais ajaye hawezi kutoka Kanda ya Kaskazini na kwamba ni Rais Kikwete pekee ndiye anayemjua mrithi wake.

Mwenyekiti huyo alisema kauli hiyo ni tata, kandamizi na yenye kuonyesha dharau kwa watu wa Kanda ya Kaskazini na demokrasia nchini na kuongeza kuwa Ikulu na Rais Kikwete, ilipaswa kutolea kauli ya kuthibitisha au kukanusha maneno hayo ya vijana wa Mkoa wa Pwani yaliyotamkwa mbele ya Ridhwan lakini hadi sasa hakuna ufafanuzi uliotolewa, hivyo kuzua hofu kuwa pengine vijana hao walielekezwa kutoa ujumbe huo na mamlaka za juu za nchi (Rais na Ikulu).


Kiongozi mwingine wa CCM ambaye wiki hii alimrushia kombora Nape, ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole aliyedai kuwa Katibu huyo kwa sasa hafanyi kazi ya kueneza na kujenga chama badala yake anakibomoa kwa kung’ang’ania hoja ya kujivua gamba, akilenga watu binafsi hivyo kupotosha nia njema ya Rais Kikwete iliyeanisha falsafa hiyo, akilenga marekebisho ya mfumo mzima wa uongozi, uanachama na chaguzi ndani ya chama.

Ole Nangole ambaye pia alizungumza na waandishi mjini Arusha, alienda mbali zaidi kwa kumuita Nape kuwa ‘muasi namba moja’ ndani ya CCM baada ya kutajwa kuwa miongoni mwa waasisi wa Chama Cha Jamii (CCJ), kilichokwama kupata usajili baada ya kushindwa kutimiza masharti.

Mtu mwingine aliyemshambulia hadharani Nape ni Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM taifa, Malisa aliyedai Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi, anapotosha nia na kauli ya Rais Kikwete kuhusu dhana ya kujivua gamba kwa kung’ang’ania kutaja majina ya viongozi wachache ndani ya chama kuwa ndio walengwa wa falsafa hiyo.

Akijibu tuhuma hizo Nape, alisema kuna kundi dogo la watu ndani ya chama hicho wenye nguvu ya pesa, wanaotaka kufanya njama za kumng'oa mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete, kwa kigezo cha kutenganisha kofia mbili, urais na uenyekiti.

Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ya Makamu Mwenyekiti wa UVCCM taifa, Malisa kutoa matamshi mazito ya kumshutumu Mwenyekiti wa Kamati ya Miradi na Uchumi ya Umoja huo Ridhwan hadharani, yameibua sura mpya ya mvutano huo.

Malisa ambaye awali alikuwa swahiba mkubwa wa Ridhiwan ambaye ni mtoto wa Mwenyekiti wa taifa wa CCM Rais Kikwete, wakati wa kampeni za kuwania Uenyekiti wa Umoja huo mjini Dodoma, walikuwa kambi moja wakipigana kushawishi wajumbe, sasa hawako pamoja tena.

Nguvu za makundi ikoje?

Kundi la watuhumiwa wa ufisadi
Nguvu kubwa ya kundi hili linalodaiwa kuongozwa na makada wanaohumiwa kwa ufisadi ndani ya chama hicho ni;
1. Kuwa na mtandao mkubwa ndani ya chama ambao ulitumika kumwingiza Rais Jakaya Kikwete madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.
2. Jumuia zote za chama ukiwemo Umoja wa Vijana (UVCCM), Umoja wa Wanawake (UWT) na Jumuiya ya Wazazi ambazo zina wanachama hadi ngazi ya shina.

3. Kundi hili linaungwa mkono pia na wenyeviti wa mikoa
19 wa CCM kutoka bara na visiwani

4. Lina nusu ya wajumbe wa Halmashuari Kuu ya Taifa
(NEC) wanaoweza kushinikiza maamuzi magumu
yakapitishwa na chama.
5. Kundi hili pia lina nguvu kubwa ndani ya bunge likiwa
na wabunge wengi wa CCM wanaoliunga mkono.
6. Lina nguvu kubwa ya fedha inayolifanya kutumia
kuwashawishi wana CCM wengi kuliunga mkono.

Nguvu ya kundi la Mwenyekiti Kikwete

Kundi hili ni lile la wana CCM wanaounga mkono maamuzi ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Kikwete ya chama kujivua gamba.

1. Kundi hili linaungwa mkono na viongozi ndani ya CCM ambao wanapambana na ufisadi wakiwamo baadhi ya wabunge, mawaziri, makada na wanachama wa kawaida wa chama hicho.

2. Nguvu nyingine ya kundi hili, ni kwamba linaongozwa na Mwenyekiti ambaye ana dola, ana uwezo wa kuteua viongozi mbalimbali hususan makatibu wa CCM wa mikoa na wilaya.

3. Mwenyekiti ana nguvu kwenye vikao, anaweza kunishikiza jambo ambalo analitaka na likafanyika kama anataka.

4. Mwenyekiti anaungwa mkono na wanachama wa kawaida wa CCM ambao wengi wao wapo katika ngazi ya matawi.

5. Raslimali zote za chama zipo chini ya Mwenyekiti.

6. Nguvu ya kundi hili pia inatokana na kuungwa mkono na kundi la viongozi wastaafu wa chama wakiwamo baadhi ya mawaziri wakuu.

Kauli za makada wa CCM

Kada wa CCM Mwanza

KADA wa CCM na Diwani wa Kata ya Lugata Kome wilayani Sengerema, Adrian Tizeba amesema falsafa ya chama chake ya kujivua gamba haina lolote kwani haina nia ya kukinusuru bali kuongeza minyukano ya makundi ambayo alisema yatasababisha kifo cha chama hicho.

Aliiambia Mwananchi Jumapili kuwa kutokana na hali ilivyo na jinsi anavyoona mambo ndani ya CCM, chama hicho hivi sasa kimegawanyika katika sura mbili kwa wakati mmoja, hivyo kinaweza kufa.

“Ninachoweza kutabiri juu ya chama changu ni jambo ambalo liko wazi, kutokana na kuwa na makundi mawili moja linalomtii na kuamini misingi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, na lingine linaloamini katika kujilimbikizia mali basi, kutaibua fujo kubwa ndani ya chama na kitavunjika,” alieleza.

Alisema kwa upande mwingine wananchi wameanza kuonekana kukichoka kutokana na kutupa misingi ya Baba wa Taifa, hatua ambayo imesababisha chama kutekwa na kundi la wafanyabiashara wanaotaka kujinufaisha.

Mwenyekiti CCM Shinyanga
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, alisema wana CCM wanapaswa kurudi kwenye kanuni na kutoa matatizo yao kwa njia za vikao na kubainisha kuwa kuyasema majukwaani ama hadharani kunakifanya chama kuonekana kama kina matatizo makubwa.

Mgeja alisema hali inavyoonekana sasa siyo nzuri, hii inatokana na baadhi ya wanachama kukiuka utaratibu wa vikao na kuwa wazungumzaji nje ya vikao.Alionya kwamba iwapo jambo hilo litaendelea basi upo uwezekano wa CCM kupoteza mwelekeo.

“Ninavyoona mwelekeo wa sasa siyo mzuri, chama kinaoutaratibu wa kutumia vikao, lakini kama watu wanazungumza nje ya vikao ni tatizo, cha muhimu ni kuwaomba wanaCCM kurejea kwenye utaribu wa vikao. Tukiendelea kuzungumza nje ya vikao, chama kitaonekana kina matatizo makubwa sana,” alieleza Mgeja.


Ole Millya
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, Millya anasema kimsingi mgongano wa kimawazo unaoibuka sasa haulengi kukidhoofisha chama hicho bali ni kuboresha.

"Hiki ni kipindi cha mpito isionekane watu kutoa mawazo kuwa, wanatumiwa au wana njaa, hali kama hii iliwahi kuvikuta vyama vya Labour nchini Uingereza na Democrat nchini Marekani na walikaa na kufikia maamuzi ambayo yamewafanya kuendelea kushika dola,"alisema Millya.

Alisema suala la kusikilizwa maoni ya vijana linapaswa kupewa uzito kwani wao ndio wapigakura wengi kwa sasa na wanaweza kuwa na mawazo chanya ya kukiboresha chama kuelekea uchaguzi mkuu.

"Haya ambayo yanatokea isionekane kuna mpasuko, hapana sote tunataka kujenga chama chetu hivyo maoni na ushauri ufanyiwe kazi na sio kundi moja kudharau lingine,"alisema Millya.

Akizungumzia kauli yake ya mtoto mmoja wa kigogo kuyumbisha chama hicho mkoani Arusha, alisisitiza ni jambo lililowazi na ana ushahidi nalo kama atahitajika kusema.

"Sisi sio vichaa kuibuka majukwaani na kulalamikia hili, tuna ushahidi na nia yetu sio kulumbana ni kutaka mambo yaende vizuri na CCM iendelee kushika dola,"alisema Millya.

Kanda mwingine wa CCM, Julius Mollel alisema katika kila chama ni busara kuzingatia maoni ya pande zote na kufikia maamuzi sahihi badala ya kudharauliana.

"Mimi ninachoona hali ndani ya CCM ni nzuri tu kwani watu wanasema na kuna marekebisho yanafanyika,"alisema Mollel.

Hata hivyo, wanaCCM wengine, Jeremiah Nkya na Solomon Singu, kwa nyakati tofauti walisema kuumbuana hadharani kwa vigogo wa CCM ni mwelekeo wa chama hicho kopoteza heshima na nguvu ya kushika dola.

Nkya alisema ni aibu chama chenye dola, viongozi wake waanze kulaumiana hadharani na kushutumiana kuwa wanataka kuuana halafu waseme ni uhuru wa mawazo.

"Kuna matatizo ndani ya CCM, la muhimu ni kumaliza malalamiko kupitia vikao sahihi," alisema Nkya.

Kwa upande wake, Singu alifafanua zaidi na kusema makundi ndani ya chama hicho, yamekifikisha pabaya na sasa viongozi wake wameshindwa kuheshimiana.

"Leo Nape (Katibu wa Itikadi na Uenezi) anasema hivi, kesho anaibuka Mwenyekiti wa UVCCM anasema vile, hivyo hivyo hata kwa mawaziri hapa hakuna chama tena kila mtu anafanyakazi kivyake"alisema Singu.

Kauli ya Nape
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape alipotafutwa na Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu jana, alijibu kwa kifupi kuwa masuala yote hayo yatazungumzwa kwenye vikao vya chama.
“Masuala yote haya yatajadiliwa kwenye vikao vya chama vitakavyokuja,” alisema Nape bila kutaja ni kikao gani ambacho kitajadili mvutano huo.
“Uamuzi wa kikao gani tutazungumza ni wetu sio wenu, kikao kitakachokuwa na hadhi ya kujadili jambo hili basi litajadiliwa,” aliongeza Nape.

Ridhiwan Kikwete
Ridhwan alipotafutwa kwa njia ya simu kuzungumzia hali hiyo hakupatikana na hata alipoandikiwa ujumbe mfupi wa simu, hakujibu.

Katika kuonyesha kuongezeka kwa fukuto la kisiasa ndani ya chama hicho, kada wa maarufu wa chama hicho, aliyekuwa pia Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, Juni mwaka huu alitangaza kujivua nyadhifa zote ndani ya chama, huku akiweka wazi kwamba amechoshwa na siasa uchwara zinazoendeshwa na baadhi ya wanasiasa ndani ya chama hicho.


Edward Lowassa
Wiki hii Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa naye alivunja ukimya kwa kuzungumzia tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa kwake, huku akisisitiza kuwa amechoka kukashifiwa na sasa kamwe hatawavumilia wanaomzulia mambo.

Alisema kuanzia sasa hatakubali kuchafuliwa jina na mtu yeyote au chombo chochote cha habari na atakayefanya hivyo, ajiandae kukabiliana na mkono wa sheria.

Alisisitiza kuwa ni jambo lisiloingia akilini kumhusisha yeye na kile kinachodaiwa mkakati wa kumhujumu Rais Kikwete au CCM, wakati yeye ni mbunge anayetokana na chama hicho na kiongozi wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nje, Ulinzi na Usalama .

 
[h=1]Kikwete maji ya shingo[/h]
picture-4.jpg

Na Saed Kubenea - Imechapwa 19 October 2011

RAIS Jakaya Kikwete amebakiwa na njia mbili tu kulinda nafasi yake katika Chama cha Mapinduzi (CCM).
Ama aachane na mpango wake wa kufukuza anaowaita "magamba," au afanye maasi ya makusudi na kuwatimua nje ya mpango wake wa awali wa kuwabembeleza kujiondoa.
Wakati watuhumiwa wameonyesha ukaidi na hata kuonyesha kutokusikia anachosema; taarifa zinasema wameanza kutumia Umoja wa Vijana (UV-CCM) kuwatetea kwa njia ya kumshutumu waziwazi Kikwete na hata mtoto wake Ridhiwan.

Wachunguzi wa mambo wanaona njia mbili ambazo Kikwete anaweza kuchangua mojawapo, ni kama ifuatavyo:
Kwanza, kuwaangukia watuhumiwa na kuwataka wajisikie amani katika chama na kuendelea kutafuta uongozi na nafasi nyingine kwa ngazi mbalimbali. Hili, hata hivyo, wachunguzi wanasema linaweza kumgharimu kisiasa.

Pili, kuleta mabadiliko katika mfumo wa katiba ya chama chake ili kupata nafasi ya kuwaengua.
Tayari njia ya kwanza imeelezwa na baadhi ya makada na wazee ndani ya CCM, kuwa ni "kula matapishi," na kudhoofisha nafasi ya mwenyekiti ambaye pia ni rais wa jamhuri.

Waliohojiwa jijini Dar es Salaam, Jumatatu hii na kukataa kutajwa majina gazetini wamesema, akifanya hivyo atakuwa anakidhalilisha na kukidharaulisha chama.
Njia ya pili ya kukabiliana na watuhumiwa wa ufisadi ndani ya CCM inaweza kulenga kuzuia wabunge wake kugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC).

Hili linaweza kufanyika kwa njia mbili: Kuondoa utaratibu wa kuwa na wajumbe wanaotokea mkoani na badala yake watokee wilayani tu.
Njia nyingine ambayo sharti itokane na mabadiliko ya katiba, ni kuzuia wabunge kugombea ujumbe wa NEC wilayani; badala yake wasubiri uteuzi kupitia nafasi za wajumbe ndani ya kamati ya bunge ya CCM.

Kwa miezi sita sasa, viongozi ndani ya CCM, Edward Lowassa, Andrew Chenge na Rostam Aziz wamekuwa wakishinikizwa, angalau kwa kauli, wajiuzulu uongozi ili "kusafisha" chama, kutokana na wao kutuhumiwa ufisadi katika nyanja mbalimbali.
Ni Rostam peke yake, miongoni mwao aliyehiari au aliyeshinikizwa kwa siri, kujiuzulu ubunge na ujumbe wa NEC. Hata hivyo, Rostam ameonekana waziwazi jimboni Igunga, akimbeba rais mstaafu Benjamin Mkapa kwenye kampeni za uchaguzi mdogo kuziba pengo aliloacha.

"Unajua, CCM inahitaji mabadiliko makubwa ya katiba, ambapo moja ya mapendekezo sharti iwe kuzuia wabunge kugombea ujumbe wa NEC kupitia wilayani," ameeleza kada mmoja na kuongeza, "…pendekezo hilo likipita, basi Kikwete atakuwa amefanikiwa kuwadondosha kina Lowassa."
Umuhimu wa mabadiliko haya umeonekana kufuatia taarifa kuwa kuna njama za kumwengua Rais Kikwete kutoka uenyekiti wa chama chake.

Ilikuwa MwanaHALISI ambayo miaka mitatu iliyopita iliripoti taarifa za kumwondoa Kikwete kwenye uongozi. Licha ya gazeti kubezwa na wanachana na viongozi wa chama hicho, lilikemewa pia na msajili wa magazeti nchini na kufungiwa kwa siku 90.

Miezi miwili iliyopita, viongozi wastaafu wa chama hicho mkoani Morogoro, walikariri taarifa hizohizo wakisema kuna wanaopita wilayani na makao makuu ya mikoa wakishawishi Kikwete atoswe.
Hivi karibuni, waziri wa mambo ya nje, Benard Membe alikaririwa akisema wateule wa Kikwete wanamsaliti; akifuatiwa na katibu wa uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliyekaririwa akisema kuna njama za kumng'oa Kikwete.

Kinachoelezwa na wapinzani wa Kikwete ni kwamba amekifanya chama kudhoofika na kuwa kwenye wakati mgumu hadi kuonekana kuwa hakiwezi kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Habari zinasema baadhi ya wanachama wanaotaka Kikwete ang'oke kwenye uongozi tayari wamejiadaa kuwasilisha hoja hiyo kwenye mkutano wa NEC uliopangwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi ujao.

Hata hivyo, MwanaHALISI limeelezwa na mtoa taarifa wake kwamba mkakati wa kutaka wajumbe wa NEC watoke wilayani umeanza kukigawa chama hicho.
Habari zinasema wapo wanaoona hatua hiyo ya kupeleka nafasi za NEC wilayani imelenga kuwaengua watuhumiwa wawili wa ufisadi ambao hawajaamua kuchukua njia ya Rostam.

Kwa njia hii na kama mapendekezo ya mabadiliko ya katiba yatapitishwa, Lowassa na Chenge waweza kushindwa kuingia NEC kwa kuwa uchaguzi wa nafasi hiyo kupitia kamati ya Bunge ya CCM, tayari umefanyika. Uchaguzi mwingine utafanyika baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Hoja ya kuzuia wabunge kugombea wilayani inaondoa uwezekano wa kukuta NEC yote ikiongozwa na wabunge ambapo, kwa vyovyote vile, wanachama wa kawaida hawawezi kushindana nao," anasema kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya CCM.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa CCM kufanya mabadiliko ambayo yanauma kwa baadhi ya wanachama wake. Iliwahi kutengeneza kanuni ya kuondoa utaratibu wa kupiga kura tatu kumpata mgombea urais mwaka 2005. Iliwahi pia kuweka sharti la kuwa na digrii ili ugombee urais.

Wakati hayo yakitendeka, mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UV-CCM), mkoa wa Arusha, James Millya ameendelea kumshindilia Kikwete kwa kukaa kimya kuhusu kauli ya Baraza la Vijana mkoa wa Pwani, kuwa rais ajaye hawezi kuwa "mtu kutoka Kaskazini" mwa nchi hii.

Sehemu ya uongozi wa UV-CCM hivi sasa inadai kuwa, kwa vile mtoto wa rais, Ridhiwan alikuwa kwenye baraza hilo, basi anajua vema chanzo cha kauli hiyo.
Katika waraka wake ambao alipanga kuusoma kwa wananchi, juzi Jumatatu, mjini Arusha (haukusomwa), Millya anatuhumu UV-CCM mkoa wa Pwani kwa kupanga "safu ya uongozi ndani ya nchi" kabla ya uchaguzi.

"Mapema mwaka huu, baraza la vijana mkoa wa Pwani walitamka wazi kwamba, ‘rais wa 2015 kamwe hawezi kutokea kanda ya Kaskazini na anayemjua Rais wa 2015, ni Rais Jakaya M. Kikwete…' " amelalamika Millya.

Amesema, "Mbali na kwamba hili ni tusi kubwa kwa watu wa Kaskazini wenye haki yao kikatiba kuwania nafasi ya uongozi wa juu wa nchi yetu, ni tusi pia kwa wapiga kura wa Tanzania…ni dhahiri kuwa rais ameshapangwa na kikundi kidogo cha watu na upigaji kura wa 2015 utakuwa ni usanii mtupu."

Millya anaituhumu ikulu kushindwa kukanusha kwamba Rais Kikwete hayumo "au hatarajii kushinikiza kwa mabavu mtu wa kuongoza taifa hili baada ya kumaliza kipindi chake cha urais" Novemba 2015.
Ameandika katika waraka wake na kuuliza, kama rais ameshapatikana, demokrasia iko wapi?
 
Mene: Mungu na Watanzania wamezihesabu siku za utawala wa CCM na kuzihitimisha. Tekel: CCM imepimwa kwenye mzani na kukutwa kwamba imepungua. Peres: Ufalme wa CCM umegawanywa na kupewa CHADEMA. by Samson Mwigamba
Kwa heri CCM!
 
Back
Top Bottom