Vita CCM yamgusa mtoto wa JK, Ikulu; MAKUNDI MAWILI YATUNISHIANA MISULI URAIS 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita CCM yamgusa mtoto wa JK, Ikulu; MAKUNDI MAWILI YATUNISHIANA MISULI URAIS 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 23, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Saturday, 22 October 2011 22:25[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]


  [​IMG]

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete

  MAKUNDI MAWILI YATUNISHIANA MISULI URAIS 2015

  Na Waandishi Wetu

  MINYUKANO inayohusisha makundi mawili ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), sasa imeanza kugusa taasisi ya Urais baada ya jina la Rais Jakaya Kikwete, mwanawe, Ridhwan na Ikulu kuanza kuhusishwa katika malumbano yanayoendelea.Jina la Rais na Ikulu limeanza kutajwa hivi karibuni katika mgogoro ulioanza baada ya moja ya kundi la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa chama hicho, (UVCCM), likiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wake wa taifa, Benno Malisa na baadhi ya wenyeviti wa mikoa wa umoja huo, kuzuiwa na Jeshi la Polisi kufugua matawi mkoani Arusha, kwa kile kilichodaiwa maelekezo ya mtoto wa kigogo.

  Ingawa Malisa na wenzake hawakutaja jina la mtoto huyo wa kigogo
  walipohutubia mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Hospitali ya St. Thomas mjini Arusha, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James Ole Millya alimtaja,Ridhwani Kikwete kuhusika na njama za kuzuia shughuli hiyo alipozungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Lash Garden, walikofikia viongozi hao.

  "Ingawa polisi wanadai kutunyima kibali cha maandamano ya kufungua mashina ya Umoja wa Vijana na mkutano wa hadhara kwa kile wanachodai taarifa za kiintelijensia kugundua kutatokea uvunjifu wa amani, tumepata habari kuwa Ridhwan ndiye kapiga simu kuelekeza tunyimwe.Sisi tutaendelea na shughuli yetu liwalo na liwe, wacha watupige mabomu kama Chadema," alisema Millya.

  Millya pia alimshambulia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauye na kumtaja kama ugonjwa wa saratani kwa chama hicho na kuonya kwamba kama hatadhibitiwa, atasababisha anguko la chama.

  Millya alizungumzia pia tamko la Baraza la UVCCM Mkoa wa Pwani lilotolewa mapema mwaka huu na kuzua mtafaruku miongoni mwa wanaCCM kuwa rais ajaye hawezi kutoka Kanda ya Kaskazini na kwamba ni Rais Kikwete pekee ndiye anayemjua mrithi wake.

  Mwenyekiti huyo alisema kauli hiyo ni tata, kandamizi na yenye kuonyesha dharau kwa watu wa Kanda ya Kaskazini na demokrasia nchini na kuongeza kuwa Ikulu na Rais Kikwete, ilipaswa kutolea kauli ya kuthibitisha au kukanusha maneno hayo ya vijana wa Mkoa wa Pwani yaliyotamkwa mbele ya Ridhwan lakini hadi sasa hakuna ufafanuzi uliotolewa, hivyo kuzua hofu kuwa pengine vijana hao walielekezwa kutoa ujumbe huo na mamlaka za juu za nchi (Rais na Ikulu).

  Kiongozi mwingine wa CCM ambaye wiki hii alimrushia kombora Nape, ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole aliyedai kuwa Katibu huyo kwa sasa hafanyi kazi ya kueneza na kujenga chama badala yake anakibomoa kwa kung'ang'ania hoja ya kujivua gamba, akilenga watu binafsi hivyo kupotosha nia njema ya Rais Kikwete iliyeanisha falsafa hiyo, akilenga marekebisho ya mfumo mzima wa uongozi, uanachama na chaguzi ndani ya chama.

  Ole Nangole ambaye pia alizungumza na waandishi mjini Arusha, alienda mbali zaidi kwa kumuita Nape kuwa ‘muasi namba moja' ndani ya CCM baada ya kutajwa kuwa miongoni mwa waasisi wa Chama Cha Jamii (CCJ), kilichokwama kupata usajili baada ya kushindwa kutimiza masharti.

  Mtu mwingine aliyemshambulia hadharani Nape ni Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM taifa, Malisa aliyedai Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi, anapotosha nia na kauli ya Rais Kikwete kuhusu dhana ya kujivua gamba kwa kung'ang'ania kutaja majina ya viongozi wachache ndani ya chama kuwa ndio walengwa wa falsafa hiyo.

  Akijibu tuhuma hizo Nape, alisema kuna kundi dogo la watu ndani ya chama hicho wenye nguvu ya pesa, wanaotaka kufanya njama za kumng'oa mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete, kwa kigezo cha kutenganisha kofia mbili, urais na uenyekiti.

  Matukio makubwa yaliyotokea wiki hii ya Makamu Mwenyekiti wa UVCCM taifa, Malisa kutoa matamshi mazito ya kumshutumu Mwenyekiti wa Kamati ya Miradi na Uchumi ya Umoja huo Ridhwan hadharani, yameibua sura mpya ya mvutano huo.

  Malisa ambaye awali alikuwa swahiba mkubwa wa Ridhiwan ambaye ni mtoto wa Mwenyekiti wa taifa wa CCM Rais Kikwete, wakati wa kampeni za kuwania Uenyekiti wa Umoja huo mjini Dodoma, walikuwa kambi moja wakipigana kushawishi wajumbe, sasa hawako pamoja tena.

  Nguvu za makundi ikoje?

  Kundi la watuhumiwa wa ufisadi
  Nguvu kubwa ya kundi hili linalodaiwa kuongozwa na makada wanaohumiwa kwa ufisadi ndani ya chama hicho ni;
  1. Kuwa na mtandao mkubwa ndani ya chama ambao ulitumika kumwingiza Rais Jakaya Kikwete madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.

  2. Jumuia zote za chama ukiwemo Umoja wa Vijana (UVCCM), Umoja wa Wanawake (UWT) na Jumuiya ya Wazazi ambazo zina wanachama hadi ngazi ya shina.

  3. Kundi hili linaungwa mkono pia na wenyeviti wa mikoa
  19 wa CCM kutoka bara na visiwani

  4. Lina nusu ya wajumbe wa Halmashuari Kuu ya Taifa
  (NEC) wanaoweza kushinikiza maamuzi magumu
  yakapitishwa na chama.

  5. Kundi hili pia lina nguvu kubwa ndani ya bunge likiwa
  na wabunge wengi wa CCM wanaoliunga mkono.

  6. Lina nguvu kubwa ya fedha inayolifanya kutumia
  kuwashawishi wana CCM wengi kuliunga mkono.

  Nguvu ya kundi la Mwenyekiti Kikwete
  Kundi hili ni lile la wana CCM wanaounga mkono maamuzi ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Kikwete ya chama kujivua gamba.

  1. Kundi hili linaungwa mkono na viongozi ndani ya CCM ambao wanapambana na ufisadi wakiwamo baadhi ya wabunge, mawaziri, makada na wanachama wa kawaida wa chama hicho.

  2. Nguvu nyingine ya kundi hili, ni kwamba linaongozwa na Mwenyekiti ambaye ana dola, ana uwezo wa kuteua viongozi mbalimbali hususan makatibu wa CCM wa mikoa na wilaya.

  3. Mwenyekiti ana nguvu kwenye vikao, anaweza kunishikiza jambo ambalo analitaka na likafanyika kama anataka.

  4. Mwenyekiti anaungwa mkono na wanachama wa kawaida wa CCM ambao wengi wao wapo katika ngazi ya matawi.

  5. Raslimali zote za chama zipo chini ya Mwenyekiti.

  6. Nguvu ya kundi hili pia inatokana na kuungwa mkono na kundi la viongozi wastaafu wa chama wakiwamo baadhi ya mawaziri wakuu.

  Kauli za makada wa CCM
  Kada wa CCM Mwanza

  KADA wa CCM na Diwani wa Kata ya Lugata Kome wilayani Sengerema, Adrian Tizeba amesema falsafa ya chama chake ya kujivua gamba haina lolote kwani haina nia ya kukinusuru bali kuongeza minyukano ya makundi ambayo alisema yatasababisha kifo cha chama hicho.

  Aliiambia Mwananchi Jumapili kuwa kutokana na hali ilivyo na jinsi anavyoona mambo ndani ya CCM, chama hicho hivi sasa kimegawanyika katika sura mbili kwa wakati mmoja, hivyo kinaweza kufa.

  "Ninachoweza kutabiri juu ya chama changu ni jambo ambalo liko wazi, kutokana na kuwa na makundi mawili moja linalomtii na kuamini misingi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, na lingine linaloamini katika kujilimbikizia mali basi, kutaibua fujo kubwa ndani ya chama na kitavunjika," alieleza.

  Alisema kwa upande mwingine wananchi wameanza kuonekana kukichoka kutokana na kutupa misingi ya Baba wa Taifa, hatua ambayo imesababisha chama kutekwa na kundi la wafanyabiashara wanaotaka kujinufaisha.

  Mwenyekiti CCM Shinyanga
  Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, alisema wana CCM wanapaswa kurudi kwenye kanuni na kutoa matatizo yao kwa njia za vikao na kubainisha kuwa kuyasema majukwaani ama hadharani kunakifanya chama kuonekana kama kina matatizo makubwa.

  Mgeja alisema hali inavyoonekana sasa siyo nzuri, hii inatokana na baadhi ya wanachama kukiuka utaratibu wa vikao na kuwa wazungumzaji nje ya vikao.Alionya kwamba iwapo jambo hilo litaendelea basi upo uwezekano wa CCM kupoteza mwelekeo.

  "Ninavyoona mwelekeo wa sasa siyo mzuri, chama kinaoutaratibu wa kutumia vikao, lakini kama watu wanazungumza nje ya vikao ni tatizo, cha muhimu ni kuwaomba wanaCCM kurejea kwenye utaribu wa vikao. Tukiendelea kuzungumza nje ya vikao, chama kitaonekana kina matatizo makubwa sana," alieleza Mgeja.


  Ole Millya
  Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, Millya anasema kimsingi mgongano wa kimawazo unaoibuka sasa haulengi kukidhoofisha chama hicho bali ni kuboresha.

  "Hiki ni kipindi cha mpito isionekane watu kutoa mawazo kuwa, wanatumiwa au wana njaa, hali kama hii iliwahi kuvikuta vyama vya Labour nchini Uingereza na Democrat nchini Marekani na walikaa na kufikia maamuzi ambayo yamewafanya kuendelea kushika dola,"alisema Millya.

  Alisema suala la kusikilizwa maoni ya vijana linapaswa kupewa uzito kwani wao ndio wapigakura wengi kwa sasa na wanaweza kuwa na mawazo chanya ya kukiboresha chama kuelekea uchaguzi mkuu.

  "Haya ambayo yanatokea isionekane kuna mpasuko, hapana sote tunataka kujenga chama chetu hivyo maoni na ushauri ufanyiwe kazi na sio kundi moja kudharau lingine,"alisema Millya.

  Akizungumzia kauli yake ya mtoto mmoja wa kigogo kuyumbisha chama hicho mkoani Arusha, alisisitiza ni jambo lililowazi na ana ushahidi nalo kama atahitajika kusema.

  "Sisi sio vichaa kuibuka majukwaani na kulalamikia hili, tuna ushahidi na nia yetu sio kulumbana ni kutaka mambo yaende vizuri na CCM iendelee kushika dola,"alisema Millya.

  Kanda mwingine wa CCM, Julius Mollel alisema katika kila chama ni busara kuzingatia maoni ya pande zote na kufikia maamuzi sahihi badala ya kudharauliana.

  "Mimi ninachoona hali ndani ya CCM ni nzuri tu kwani watu wanasema na kuna marekebisho yanafanyika,"alisema Mollel.

  Hata hivyo, wanaCCM wengine, Jeremiah Nkya na Solomon Singu, kwa nyakati tofauti walisema kuumbuana hadharani kwa vigogo wa CCM ni mwelekeo wa chama hicho kopoteza heshima na nguvu ya kushika dola.

  Nkya alisema ni aibu chama chenye dola, viongozi wake waanze kulaumiana hadharani na kushutumiana kuwa wanataka kuuana halafu waseme ni uhuru wa mawazo.

  "Kuna matatizo ndani ya CCM, la muhimu ni kumaliza malalamiko kupitia vikao sahihi," alisema Nkya.

  Kwa upande wake, Singu alifafanua zaidi na kusema makundi ndani ya chama hicho, yamekifikisha pabaya na sasa viongozi wake wameshindwa kuheshimiana.

  "Leo Nape (Katibu wa Itikadi na Uenezi) anasema hivi, kesho anaibuka Mwenyekiti wa UVCCM anasema vile, hivyo hivyo hata kwa mawaziri hapa hakuna chama tena kila mtu anafanyakazi kivyake"alisema Singu.

  Kauli ya Nape
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape alipotafutwa na Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu jana, alijibu kwa kifupi kuwa masuala yote hayo yatazungumzwa kwenye vikao vya chama.

  "Masuala yote haya yatajadiliwa kwenye vikao vya chama vitakavyokuja," alisema Nape bila kutaja ni kikao gani ambacho kitajadili mvutano huo.

  "Uamuzi wa kikao gani tutazungumza ni wetu sio wenu, kikao kitakachokuwa na hadhi ya kujadili jambo hili basi litajadiliwa," aliongeza Nape.

  Ridhiwan Kikwete
  Ridhwan alipotafutwa kwa njia ya simu kuzungumzia hali hiyo hakupatikana na hata alipoandikiwa ujumbe mfupi wa simu, hakujibu.

  Katika kuonyesha kuongezeka kwa fukuto la kisiasa ndani ya chama hicho, kada wa maarufu wa chama hicho, aliyekuwa pia Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, Juni mwaka huu alitangaza kujivua nyadhifa zote ndani ya chama, huku akiweka wazi kwamba amechoshwa na siasa uchwara zinazoendeshwa na baadhi ya wanasiasa ndani ya chama hicho.


  Edward Lowassa
  Wiki hii Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa naye alivunja ukimya kwa kuzungumzia tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa kwake, huku akisisitiza kuwa amechoka kukashifiwa na sasa kamwe hatawavumilia wanaomzulia mambo.

  Alisema kuanzia sasa hatakubali kuchafuliwa jina na mtu yeyote au chombo chochote cha habari na atakayefanya hivyo, ajiandae kukabiliana na mkono wa sheria.

  Alisisitiza kuwa ni jambo lisiloingia akilini kumhusisha yeye na kile kinachodaiwa mkakati wa kumhujumu Rais Kikwete au CCM, wakati yeye ni mbunge anayetokana na chama hicho na kiongozi wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nje, Ulinzi na Usalama .
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. k

  kuzou JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ccm inasuprise mpya kila kukicha hivyo ataibuka mtu asiyetegemewa na kuwa kidedea.
  ewe jk huna cha kupoteza sasa achana na makundi fanya kazi,hugombei huhitaji kupendwa kuwa mkali
   
 3. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #3
  Oct 23, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  KUVUNJIKA KWA CCM NDIYO ZAWADI PEKEE KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 50 YA UHURU:hatari:
   
 4. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  M.k.w.e.r.e ameshika hatamu!!! haangalii nyuma wala mbele, anayesikilizwa ni alshaab mbeba bunduki kiunoni
   
 5. m

  mbosia Senior Member

  #5
  Oct 23, 2011
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  mh !!!!!!! mbona maneno mazito namna hiiiiiiiiiiiiiiiiiii ??????????????
   
 6. p

  plawala JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watajiju,miaka 50 waliyotawala yametosha,hakuna marefu yasiyo na kikomo,tunataka watu tofauti wenye fikra mbadala
   
 7. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  yaani kujilimbikizia mali kote huko bado hujatosheka tu? Nalog off
   
 8. king'amuzi

  king'amuzi JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kufa kwa ccm ni faraja kwa watanzania. die quickly magamba
   
 9. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,032
  Likes Received: 3,056
  Trophy Points: 280
  Tunataka watajane kwanza mmoja mmoja kwa kila nukta kabla hawajafa na magamba yao make wengine walishasema magamba yanaishia kiunoni tu vinginevyo kichwa kitenganishwe na kiwiliwili...hii nayo kali
   
 10. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 1,522
  Trophy Points: 280
  ......nyimwa vingine lakini sio uwezo wa kufikiri, hebu angalia hawa, GADDAF, SADDAM, MUBARAK, AL SAAD (kwa uchache) yaliwadodea/yanawadodea mambo kwa ajili tu ya aidha kuanda wanao ama wao waliandaliwa na baba zao, watu hawataki tena kusikia baba mara mtoto mara mjukuu, kwa vuguvugu la sasa hivi mimi ningekuwa riz, wala nisingesema kitu kuhusu hizi siasa uchwara (according to Rostam).....
   
 11. O

  Omr JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nyie vilaza wa CDM subirini kufa kwa chama chenu 2015.
   
 12. z

  zakaria Member

  #12
  Oct 23, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  wamejifichaficha vya kutosha sasa ni wakati Watanzania kuona yaliyomo mioyoni mwao: unafiki na uroho wa madaraka. Wanagombania kwend Ikulu! Ajabu sana hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
Loading...