Balozi Herbert Mrango lete majibu kamili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balozi Herbert Mrango lete majibu kamili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Divele Dikalame, Feb 7, 2012.

 1. D

  Divele Dikalame Member

  #1
  Feb 7, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika gazeti la Habari leo la februali 4,2012 uk wa 5 kuna taarifa kwa umma iliyotolewa na wizara ya ujenzi na kusainiwa na katibu mkuu wake bwana Mrango kukanusha habari zilizochapishwa katika gazeti la Raia mwema toleo la februali 1,2012 lililofichua malipo hewa ya zaidi ya bilioni 10 kwa kampuni ya CHICO-CRSG JV inayojenga barabara ya KAGOMA-LUSAHUNGA1.

  Balozi Mrango hana alichojibu zaidi ya kutapata na ameshindwa kukanusha tuhuma hizo dhidi ya mpango wao mchafu wa kutaka kukwapua bilioni 10, sijui balozi Mrango anadhani watanzania ni mambumbu kiasi cha kuwalaghai wakubale hoja zake dhaifu mno kuliko hata utando wa buibui.

  katika barua tarehe 1 Desemba yenye kumbukumbu na TRD/D/GEN/P.99/01/XVIII/A iliyosainiwa na mtendaji mkuu wa TANROADS bwana Mfugale amekiri kwamba kiasi kilichotakiwa kulipwa kwa kampuni CHICO-CRSG JV toka hazina ni bilioni 27 lakini akadai makosa yamefanyika hesabu iliyopelekwa hazina ni bilioni 37 badala ya 27!!? kwa mantiki hiyo bilioni 10 zimezidi na ukadai mkandarasi aliyekosea hilo [bwana Kisandu] amechukuliwa hatuwa wakati si kweli bali mlichofanya ni kumuhamisha na kumpeleka CML na bwana Kisandu anasema wazi aliambiwa achakachue hivyo wala hakuandika kwa makosa.

  pia Balozi Mrango ameshindwa kutoa ufafanuzi wa malipo hewa ya milioni 800 badala ya milioni 60 kule TEMESA
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 12,863
  Likes Received: 1,640
  Trophy Points: 280
  Duh Mkuu kumbe ngoma bado mbichi. Tuwekeeni basi na hizo barua na hiyo taarifa ya umma ili nasi tujisomee
   
Loading...