Balaa: Kuna ajali kubwa huko Iwambi

Balaa: Kuna ajali kubwa huko Iwambi

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,676
Reaction score
59,166
Kulikoni? Naambiwa Huko Iwambi Mbeya kuna ajali kubwa. Pigia simu ndugu na jamaa..

Sijajua zaidi hadi sasa sababu ni taharuki tupu..

Tusubiri Polisi waseme

=====

UPDATES: 1200HRS

=====

Watu 28 wamefariki dunia na wengine wanane kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu ikiwamo lori katika mlima Iwambi jijini Mbeya.

Akithibitisha ajali hiyo, Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema ajali hiyo imetokea jana Jumamosi, Juni 6, ambapo watu 27 walifariki papo hapo na majeruhi kuwahishwa Hospitali teule Ifisi iliyopo Mbalizi.

Amesema katika barabara kuu ya Tanzam, kutokea Mbeya kwenda Tunduma, gari aina ya lori likiwa na tela likiendeshwa na dereva Philip Mwashibanda (33) liligonga magari mengine mawili.

Amesema katika magari hayo yaliyokuwa na abiria yaligongwa na lori hilo, kisha kutumbukia kwenye korongo ulipo Mto Mbalizi na kusababisha vifo na majeruhi hao.
"Baada ya kugonga magari hayo yalitumbukia korongoni na kukita kwenye gema na kingo za mto, jana hiyo walifariki watu 27 na leo asubuhi tumepata taarifa ya majeruhi mmoja kufariki na kufikia idadi hiyo" amesema Kamanda Kuzaga.

IMG-20250608-WA0004.jpg


IMG-20250608-WA0037.jpg
IMG-20250608-WA0038.jpg
 
Ile iwambi imekaa vibaya sana..... serikali ifanye jambo pale sio mpaka tusubirie apate ajali yule kijana AUBUDULI......hata sisi wanyonge tunapenda kuishi

Nyie si mnapita na msafara na mnakuta kweupe Sisi wanyonge tunaongozana na maroli ambayo wakati mwingine yanafeli breki na kuleta maafa
 
Road Accident is about Man made
Pole Sana .

Serikali imelala Sana hiyo barabara inahitaji kuwekwa sawa.

Hizo mbeya marathon kwanini msiachane nazo mkajenga barabara
Wanapenda mbio hao watu ni balaa.....na kila ziku zinawalaza chini.

Na hili nalo mpaka No reform no election?
 
Hizo kenge zilizojaa hapo zikalale sasa usiku
Waache vyombo vya uokoaji viwe na nafasi na eneo la kufanyia kazi....
 
Back
Top Bottom