Jamani kwa wale wa enzi hizo kulikuwa na posts za kisiasa zenye mtiririko wa kiufundi zilizokuwa zinapostiwa kama sikosei kwenye gazeti la Majira. Huyu jamaa alikuwa ni mzungu aliyeoa usukumani kama sikosei na alikuwa anajulikana kama Bala wa mabalaa baada ya makala yake moja kubeba jina hilo lakini alikuwa na mchango mkubwa sana katika kuamsha hisia za watanzania dhidi ubabaishaji wa serikali wakati huo. Nakumbuka nilikuwa sikosi kununua gazeti ili nisome makala zake na nilikuwa nikicheka mpaka mbavu zinaniuma jinsi alivyokuwa anayapangilia madongo yake. Nakumbuka makala yake moja ilikuwa inaitwa Bangi ya Bunge na ukiismoma utacheka mpaka mbavu zikuume. Kama sikosei walimpa kibano akaachana na mambo ya kutunga makala zake na akaendelea na shughuli zingine.
Kwa wenye makala zake au kama yeye mwenyewe yupo humu basi naomba azipost zile makala zake ili ziwakumbushe vijana wetu tulipotokea katika mapambano ya kudhibiti serikali zetu za ubabaishaji.
Nawakilisha