kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,177
- 17,512
Inatia mashaka na aibu kama Bwakwata (kundi dogo) la waislam nchini linapowapotosha waislam na wananchi wote wa Tanzania kuhusu lini iwe sikukuu za kiislam na lini isiwe kwa kutumia kifungu kwenye maandiko ya quran yanayosema "fungeni kwa kuuona mwezi"
Nasikitika kuona BAKWATA kwa kutumia watendaji wake wanawapotosha na kuwaletea usumbufu wananchi wenzao bila sababu za maana. Wanatumia maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano kwa kuwapotosha na kuwatenganisha waisilam wa Tanzania badala ya kuwaunganisha na waislamu wenzao duniani. Nilimuona Sheikh Mataka BBC akiongea na mtangazaji wa BBC Salim Kikeke juu ya tofauti za tarehe kati ya "Tanzania" na Saud-Arabia, kwamba sio vizuri kuwafuata watu wa Saudi katika tarehe za kiislam ila tufuate kuuona mwandamo wa mwezi katika kila Taifa. Hoja ya Mataka na wenzie inatia mashaka kwasababu zifuatazo
1. Dini ya Kiisalam ilishushwa Saudi Arabia (Uarabuni), hivyo kuna utukufu fulani katika uislam
2. Watu wa Saudi Arabia ndio waliomzaa, kumlea, kumlinda na kumpokea Mtume Mohamad SAW, hivyo ni waaminifu sana katika uislam. Hivyo hatuna sababu ya kuwa na mashaka nao wanaposema na kudhibitisha kuwa wameuona mwezi.
3. Kaabar, Arafa ni moja tu na iko Saud
4. Wakati wa Mtume mawasiliano na usafiri vilikuwa duni (ngamia, punda, mitumbwi, na miguu tu basi), hivyo bila ya elimu za Uchina watu wengi wangeshindwa kukamilisha nguzo ya tano ya kwenda kuhij
5. Wakoloni ndio waliofanya Dar es Salaam, Kigoma, Mtwara, Mwanza, n.k iwe nchi moja (Tanganyika) na sio mwenyezimungu wala waislam. hiivyo kwa kufuata falsafa ya kufunga kwa kuuona mwezi bila kuweko kwa teknologia ya habari na mawasiliano hata waislam wa Tanzania wasingefunga na kufungua siku mmoja maana wakigoma wangeuona mwezi siku tofauti na wale wa Mtwara na Tanga. Sayansi ndiyo iliyoipa DSM na Kigoma muda unaofanana sio Mwenyezimungu. Mwenyezimungu ana taifa moja tu la waislamu vilivyobakia ni vitongoji na vijiji tu.
6. Tofauti ya Tanzania na Saudi Arabia sio masaa 24. Hivyo kutofautiana kiibada na Saud kwa masaa 24 sio sahihi
7. Ugunduzi katika teknolojia ya habari, mawasiliano na uchukuzi ni mpango mahsusi wa MwenyeziMungu katika kuwaunganisha waislam wote duniani. Ndiyo maana Mtume aliwaambia waislam watafute elimu hata ikibidi kwenda Uchina ambako alijua kuwa kwa enzi hizo kulikuwa mbali sana kufika na hakukuwa na muislam hata mmoja huko Uchina. Alifahamu kuwa elimu ya wachina itasaidia katika kuimarisha uislam hata baada ya yeye kufa. Kwa elimu kutoka uchina (isiyo ya kiislam) ndio maana leo hii tuna simu, redio, TV, vipasa sauti, umeme, kanzu nzuri, magari, ndege, computer, bunduki, n.k, na kuyafanya makundi ya waislamu wafike Saudi kwa ibada ya Hijja
8. Kama muislam huna elimu kutoka uchina (hata kama uko Saudi kwenyewe) hupaswi kuwa msemaji wa waislam kwasababu utakuwa na mapungufu mengi ambayo Mtume aliyaona kabla. Mtume alijua kuwa elimu ya Uchina itakuja kuwa lulu kwa uislam katika miaka ijayo baada ya yeye kuondoka na ndiyo maana iliwahimiza waislam waitafute kwa juhudi.
9. Hata Bw. Mtume Mohamad S.A.W aliwahi kufunga na kufungua kwa kusikia tu habari za mwezi, iweje leo Tanzania tusiwaamini hata wale watu wanaoilinda Kaabar kuwa wameuona na kuthibitisha kuwa wameuona mwezi? Hii ni hujuma kwa waislam na uislam. Kama haiwekekani kuwaamini watu wa Saudi basi isiwezekane hata kwa watu wa Mwanza na wa DSM kuswali siku moja, maana hata masaa yetu ni tofauti pia, Saa moja usiku hapa DSM kule Mwanza na Kigoma bado jua linawaka (ni mchana).
Ushauri wangu ni kwamba Saudi ni muhimu sana katika dini ya kiislam na uislam. Kila nchi ikisema ifunge kwa kuuona mwezi sio sahihi, maana Mtume hakuacha nchi inayoitwa Tanzania wala Kenya, bali kulikuwa na miji kama Lamu, Mombasa, Liwale, Mikindani, na makabila ya Wazaramo, warangi, wazigua, wagogo, waha, wasukuma, Wakwere, n.k, ambayo kwa kigezo cha "fungeni kwa kuuona mwezi" isingewezekana hata hapa Tanzania kabla ya kuja wakoloni waliyoifanya Dar es Salaam na Kigoma kuwa Tanganyika na bila ya kuweko kwa maendeleo ya mawasiliano. Hivyo, wanaofunga na kufungua kwa kufuata tarehe za Saudi wako sahihi na waungwe mkono kwa kukuwa wanafuata hekima za Mtume ya elimu ya Uchina iliyozaa teknologia ya habari na mawasiliano inayotumika kupashana habari leo juu ya kuandama kwa mwezi huko Saudi. Viongozi wa BAKWATA lazima wawe wale waliotimiza maneno ya Mtume ya kutafuta elimu hata ikibidi uchina. Mwenyezimungu bado anaendelea kuiumba dunia na watu wake, tusibaki palepale pa fungeni kwa kuuona mwezi, ukifanya hivyo ni sawa na mtu anayekataa kutumia usafiri wa gari na ndege kwakuwa Mtume hajasema wala kuutumia usafiri huo. AIBU
Ni mawazo yangu