BAKWATA ni taasisi ya Serikali?

Mwenye picha ya ofisi za bakwata za sasa na officially ofisi ya Mufti kwa sasa aiweke tunaweza kupata jibu kwa nn wanajengewa.
 
Wasomaji wa ilani ya ccm wangejibu hili huwenda ipo kwenye ilani ya ccm, kwa kuwa makamba alidai kila kinachofanywa na magufuli kipo kwenye Ilana.
 
Ndio maana nimekuambia umem-quote kumbe hilujamuelewa....Ungerudia kusoma kwa makini ungegindua wala alikuwa hana upande wowote wa dini...

Jinga kabisa..
Anaweza kuwa hana upande wowote, sijakataa, ila kitendo cha yeye kuita dini zingine majina ya ajabu katika maandishi yake kunamfanya kuwa mmoja wa wale ambao hawajapevuka.

Ana hoja nzuri na anaeleweka, lakini alishindwaje kufikisha hoja zake bila kuita wengine 'makafiri' na 'wapagani' ?? na kuita dini nyingine kuwa ni 'deen ya haki'??

Walimu wana kazi sana kuelewesha 'slow learners' kama wewe.
 

Haya mambo hayajaanza leo. Ndio maana kuna baadhi ya waislamu hawaridhishwi na BAKWATA, wanakiona ni kama chombo cha serikali. Na hasa kipindi hiki ambacho wapinzani wanaonekana kuwa na nguvu tutaiona hiyo "misaada" kwa wingi zaidi.
 
Mimi kwanza ningehoji hii tabia ya viongozi wetu kuchangia au kusaidia mamilioni au bilioni za shilingi pasipo kusema wamezitoa wapi? Sijapata kusikia rais wa nchi zilizoendelea akichangia jambo kwa kiasi zaidi ya mshahara wake!

Hili la Bakwata kwa kweli halijakaa sawa maana LINAACHA MASWALI MENGI na linagawa waislam kwa waislam na wakristo kwa waislam. Tunarudi pale pale, kiongozi ni nani na mtu binafsi ni nani? Makonda kama kiongozi wa serikali isiyo na dini anashiriki vipi ujenzi wa jengo la taasisi ya kidini? Waislam kwa muda mwingi wamekuwa na mtazamo tofauti juu ya Bakwata, je ujenzi wake unahaashiria nini kwenye mahusiano yao wao kwa wao na mahusiano ya baadhi yao kwa serikali? Waislam wasio na imani na Bakwata wananufaikaje na ujenzi wa jengo hili?

Je wakristo ambao wapo katika madhehebu mengi tofauti wakidai ujenzi wa kitu chochote watapata ushirikiano na serikali? Wapagani? Wahindi au wahindu? Je kwa hili la Bakwata hivi ni kweli serikali haina dini?

Ngumu kwa wananchi wakawaida kujuwa ni nani anajenga jengo hili na ushiriki wa Makonda kama serikali unaanza wapi na unaishia wapi?
 
Rejea mkataba kati ya serikali na umoja wa makanisa. Serikali hutoa ruzuku na mishahara kwenye taasisi za makanisa. Serikali ilitaifisha shule wakawarejeshea madhehebu ya kikistu huku zile za waarabu hazikurejeshwa kwa waislam. Acha tu nchii itafika mda tutafahamiana tu.
 
Jee anapokwenda kanisani na brief kama hiyo na akatoa mchango inakuwaje????
 
BAKWATA ni taasisi ya chama tawala kinachoongoza Serikali
 
Bakwata, Tec na CCT ni taasisi zenye msingi wa kiserikali na hii ilifanywa kwa NIA njema kabisa na hata TAG ina msingi huohuo.Zenyewe hazipewi ruzuku kama vyama vya siasa lakini inkind vinabenefit kupitia misamaha ya kodi.Ndio maana tuna Amani hata sasa fikiria kama hao wote wangeachwa kama siye mitume na manabii sijui kama pangetosha,so Makonda kuwafadhili Bakwata kama ana uwezo HUO halitakuwa jambo JIPYA
 
Mkuu bakwata ni taasisi ya serikali mbona inaeleweka tangu siku nyingi,ila kwa sasa ndio wameamua kuweka wazi kabisaa
 
Kwa namna ulivomalizia na wewe ni mdini namba moja, eti raisi "mdini", kweli???
Mkuu mimi sio midini, ndio maana nikiona mtu, kundi au jamii fulani wanajiona wao ni bora kuliko wengine, hawaheshimu na kuthamini wenzao, hawapendi wenzao, wanaita wenzao majina ya ajabu, hawatoi fursa sawa kwa wote n.k kwa sababu tu ya tofauti ya kidini huwa naona ni udumavu wa fikra.
 
Misikiti aliyojenga lowassa ni mali ya lowassa au ya Chadema? Au nayo ni matawi ya Chadema?

Unalalamika watu kujengewa msikiti, tatizo pande zote mnawafanya waislamu hamnazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…