hao wameibuka baada ya kuona wenye madaraka na BAKWATA wana tumia vibaya rasmali za baraza ndio maana wakaanza kusema ukweli na hapo sioni kama ni tatizo,

mkuu kwa nini ponda asikemee huo ubadhirifu kwa kupitia vikao rasmi vya bakwata, je atafanikiwa vipi kwa kukemea ubadhirifu akiwa nje ya mfumo wa uongozi tena kwenye mihadhara isiyo na vibali?
 
....kwa wingi wanaoikubali TAASISI NA kwa wingi wao wanaoikataa.....BAKWATA ilianza kupingwa toka kipindi cha kuundwa kwake soma historia mzee watu walienda jela kwa kutoikubali bakwata swala la kupingwa kwa bakwata halijaanzia leo,na nikwambie kitu wanaoikubali BAKWATA ni wale wasio jua BAKWATA ILIUNDWAJE,NA HAWANA LOLOTE wanalojua juu bakwata na historia yake na ndio maana yyt atakae zungumza historia ya bakwata atakuwa muharifu,na hao viongozi wako unao waona wanauma na kupuliza na kingine wanaheshimu familia zao na matumbo yao.
 
mkuu kwa nini ponda asikemee huo ubadhirifu kwa kupitia vikao rasmi vya bakwata, je atafanikiwa vipi kwa kukemea ubadhirifu akiwa nje ya mfumo wa uongozi tena kwenye mihadhara isiyo na vibali?

sijamzungumzia ponda hapa,ila kuna tofauti gani kati ya chama tawala na chama pinzani....wakina ponda's wamekuwa ni kama upinzani kwa BAKWATA kwa kujua kwao madudu ya BAKWATA.....WEWE UNADHANI KWANINI SERIKALI BADO WANAIKUMBATIA BAKWATA???
 
MUANZISHA MADA HONGERA SANA NDG ZETU WABUBUJIKE ILI KUPATA SULUHISHO SAHIHI LA "BAKWATA" WAITAKAYO ili tupuzike na ghasia zinazolipukalika hovyohovyo
 
Waisilamu wanalaumu kwamba BAKWATA ilianzishwa na serikali. Waisilamu hao hao wanailazimisha serikali iuwaanzishie mahakama ya kadhi. Kwa ufupi waisilamu ni watu wa ajabu sana hapa duniani, ni majanga!
 
mods ondoa huu Uzi, kama ni mambo ya dini mkajadiliane huko msikitini.Siku hizi watu wanajadili mambo ya maendeleo bwana.Kila kukicha dini, dini, dini.
 
MUANZISHA MADA HONGERA SANA NDG ZETU WABUBUJIKE ILI KUPATA SULUHISHO SAHIHI LA "BAKWATA" WAITAKAYO ili tupuzike na ghasia zinazolipukalika hovyohovyo

Ifike wakati serikali iwe na AIBU kwa hili,historia yaonyesha wao kama serikali ndio waliocheza rafu kwa kuwatumia hawa jamaa,Adam Nasibu, Sheikh Kassim Juma na Abdallah Chaurembo.
 
Waisilamu wanalaumu kwamba BAKWATA ilianzishwa na serikali. Waisilamu hao hao wanailazimisha serikali iuwaanzishie mahakama ya kadhi. Kwa ufupi waisilamu ni watu wa ajabu sana hapa duniani, ni majanga!

kama serikali iliweza kuanzisha BAKWATA kwanini ishindwe MAHAKAMA YA KADHI,bakwata ikitoka mikononi mwa serikali wataweza kuanzisha mahakama yao na serikali kuwa na mwakilishi tu katika mchakato mzima na kutoa ushauri.
 
mods ondoa huu Uzi, kama ni mambo ya dini mkajadiliane huko msikitini.Siku hizi watu wanajadili mambo ya maendeleo bwana.Kila kukicha dini, dini, dini.

kama unaona kwako upuuzi kuna majukwaa mengi NENDA,hii nchii haina utawala wa AMRI
 
kama serikali iliweza kuanzisha BAKWATA kwanini ishindwe MAHAKAMA YA KADHI,bakwata ikitoka mikononi mwa serikali wataweza kuanzisha mahakama yao na serikali kuwa na mwakilishi tu katika mchakato mzima na kutoa ushauri.
Serikali imejifunza; inaogopa kuwa kwa suala la mahakama ya kadhi itakuja kulaumiwa kama inavyolaumiwa kwa suala la BAKWATA, kwa hiyo heri wawaachie walalamikaji waianzishe wenyewe!
 
Bakwata ilianzishwa na Nyerere kule iringa baada ya mwl kutoka tabora kuzungumza na wazee wa kikatoliki.

Bakwata haikuanzishwa kwa nia ya kuwasaidia waislam kwa namna yeyote, hata mzee ruksa analijua hilo.

Kwani waislamu wanataka kusaidiwa na BAKWATA kutatuta matatizo gani?
 
Serikali imejifunza; inaogopa kuwa kwa suala la mahakama ya kadhi itakuja kulaumiwa kama inavyolaumiwa kwa suala la BAKWATA, kwa hiyo heri wawaachie walalamikaji waianzishe wenyewe!

sasa kama ni hivyo serikali iache bakwata ifanye mambo yake,na kama baadhi ya watumishi wake hawakuhusika kula njama za kuuza mali za bakwata hakuna ulazima wa kuendelea kuikumbatia,wa plant watu kama wanavyofanya kwa madhehebu mengine,lakini si kila kitu kufanya wao.WAICHE BAKWATA SASA ili ipate viongozi wenye nidhamu na utii wa imani yao.
 
kwani waislamu wanataka kusaidiwa na bakwata kutatuta matatizo gani?

waislamu wanataka bakwata safi isiyo na mkono wa serikali,bakwata itakayo heshimu mali za taasisi hizo ili zilete manufaa kwao na kwa wengine,
 
Waisilamu wanalaumu kwamba BAKWATA ilianzishwa na serikali. Waisilamu hao hao wanailazimisha serikali iuwaanzishie mahakama ya kadhi. Kwa ufupi waisilamu ni watu wa ajabu sana hapa duniani, ni majanga!
Wakristo wanakataa Mahakama ya Kadhi kugharamiwa na serikali lakini hawaoni tabu yoyote BAKWATA kugharamiwa kwa pesa za serikali!

Serkali nayo haitaki kuigharamia Mahakama ya kadhi lakini haioni ubaya wowote kuigharamia BAKWATA.

Kanisa na serikali nani ni nani?
 
ukweli ndio huo ni ubwabwa mbele wala sio ibada, kikubwa ni commercialization of islam kama unafikiri duniani kuna siku utaiona amani basi we ni chizi, ni kaburini tu ndiko kuliko na amani, zoea vurugu kama uko hai usiwe mwanamke mkubwa.

tatizo lako nini....??? kama hauna cha kuchangia unakaa kimya tu,
 
Mkuu SP mimi nakubaliana na wewe kabisa. Umefika wakati wa watu kuacha kulalamika kama ambavyo wamekuwa wanafanya kwa miaka zaidi ya 40 iliyopita. Pamoja na kuangalia re-oragisation ya BAKWATA, lakini pia waislamu wanatakiwa kujipanga.

Tunapoona wachanga, wahaya na wanyakuyusa wameshika naafasi za juu katika ofisini za serikali na mashirika ya umma, hata kwa watu binafsi, it did not happen out of the blue. Mzee ruksa alikuwa Raisi wa nchi hii kuanzia mwaka 1985 na hadi sasa Raisi a;pyeko madarakani ni mwislamu.

Adolf Hitler alijaribu sana kuwateketeza Jews, na wao walipojua fate yao walijipanga. leo hii tunalijua vema taifa hilo na makeke yake,

Mimi nadhani kama waislamu wangejipanga vizuri tokea wakati mwa Utawala wa Myinyi, hali ingekuwa tofauti sana. Moja kati ya mikakati ya mzeee Ruksa ni kumfanya kighoma Malima (RIP) kuwa waziri wa elimu. Alikifanya wizarani pale kinafahamika. Ni zaidi ya miaka 30, wafadhili wangejikiza zaidi kwenye kujenga shule na institutions za elimu ili kupunguza gap linalolalamikiwa (kati ya waislamu na wakristo). Tokea 1985, kama wangekuwa wamejipanga, hadi sasa wamekuwa na vijana ambao wamemaliza shahada ya pili na wengine wanafanya shahada ya tatu. Kwa njia hiyo, utashangaa haya malamiko yote ya kuonewa yashingekuwepo.

Shida, watu wamebaki kulalamika tu na hakuna mikakati madhubuti ya kuondoka tofauti hiyo miaka ya baadaye

mkuu umeongea kweli lakini hapa tujadiri bakwata na serikali,
 
ndio maana watu husema serikali ina mkono mrefu .....isue si kulalama isue hapa srikali ikae pembeni iache bakwata waamue mambo yao,BAKWATA ndio mmiliki wa mali za waislamu wao ndio wanaotambulika zaidi,ndio wasemaji wa waislamu TZ nzima sasa watakapo kuwa na maamuzi yao binafsi wataendesha miladi yao bila kuingiliwa na serikali na mpk kusomesha watu wao,kama walikosea basi walikosea mwanzo si leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…