BAKWATA, Clouds FM huko mwendako siko!As-Salamu Alaykum

clouds fm radio ya??????? malizia mwenyewe hivo sioni haja ya kuilamu kwani taaluma za watangazaji wake ni vilaza,tasnia ya uandishi wa habari inavamiwa na wanaofeli form 4 na form 6 wanaingia vyuo utitiri vya uandishi wa habari mnategemea nini? kama amefeli somo la uraia,kiswahili,historia,kiingereza masomo haya ndio yanapandisha credit za watu wengi wasiojua hesabu mitihani ya form 4 sasa na hayo kafeli atakuwa na upeo gani? bora msikize radio zingine sio clouds,
 
HISTORIA ya dunia hii imesheheni ushahidi wa kutosha kabisa kutuonyesha kwamba mambo makubwa makubwa ya kutisha chni ya jua yameanza kama masihara na katika vitu vidogo vidogo tu ambavyo watu wangeweza kudhani kwamba havina maana wala msingi wowote.

Ndiyo maana watu makini na viongozi mahiri duniani kote hawapuuzi mambo yanayodhaniwa na wengi kuwa ni madogo au ni ya kupuuzwa, hii ni kwa sababu mambo madogo yasipoangaliwa kwa makini yanaweza kutumiwa na watu wachache yakakuzwa na hata kuwa balaa kwa taifa na jamii husika.
Ninazungumzia kile kilichotokea kwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Mama Fatma Kimario na wafuasi wanaodhaniwa kuwa ni wa CHADEMA. Wakati hakuna mtu mwenye akili zake timamu, ikiwemo safu hii, anaweza kuunga mkono vurugu za aina yeyote ile au matumizi ya aina yoyote ile ya nguvu katika kutatua tatizo, wako watu wanaonyesha kila dalili za kulishadidia suala hili kwa maslahi ya kisiasa.

Na kwa muktadha huo, safu hii inajikita katika kujadili masuala mawili yatokanayo na sakata hilo, kwanza ni taarifa ya BAKWATA na BASUTA kutaka CHADEMA iombe radhi Waislamu kwa kuwa wamemdhalilisha mama huyo kwa kumvua hijabu (au mtandio aliokuwa amejitanda kichwani kama maadili ya Kiislamu yanavyowataka wanawake wa Kiislamu wawe).

Kama ambavyo mchangiaji mmoja katika mtandao wa Jamii Forum alivyochangia kuwa “Ndugu zangu Waislamu kwa hili mnapotoka sana. Padri aliyebaka hawezi kusubiriwa avue kanzu yake ndio akamatwe, vazi ni nini kwani? Vazi si alama ya imani ya Uisilamu bali ni utambulisho ambao hata shetani anaweza kujigubika humu. Uisilamu ni upendo, ni moyo wa kujali haki na kuzingatia uadilifu tunapopewa majukumu ya kusimamia haki vitu ambavyo DC yule kwa siku ile alivikosa. Chonde sana viongozi wa BAKWATA na BASUTA tuepuka kuingia kwenye siasa kwa kuwagawa Watanzania kwa kutumia imani zetu hata pale ambapo hakuna uhusiano”



Ninaamini Clouds FM wanalijua hili, lakini katika moja ya vipindi vyao, mtangazaji wao( Epharim Kibonde) akizunguza kuhusu sakata hili la Mkuu wa Wilaya wa Igunga, amenishtua na kwa hakika nimeogopa. Mtangazaji huyo katika moja ya vipindi anapolivisha suala hili sura ya kidini kwa kiwango kile, huku akijua kuwa wasikilizaji wake wana viwango tofauti sana vya uelewa sijui alikuwa anadhamiria kuiambia nini jamii.

Mtangazji huyu amekwenda mbali (mbali sana) kupandikiza hisia za udini wa hali ya juu kwenye suala hili, anapozungumzia habari za kwamba eti Waislamu nao wakifikia hatua ya kuwavua watawa Wakatoliki vilemba vyao kama alivyofanywa mkuu wa wilaya, kwa hakika hii ni hatari sana kwa umoja na mshikamano wa taifa hili.

Maadili ya taaluma hii yanatutaka tusema ukweli tu na ukweli mtupu kwa manufaa ya ustawi na mshikamano wa jamii tuliyomo.
Tukifika mahali tukaanza kuwianisha hisia zetu au ushabiki wetu katika mambo tete na nyeti kama imani za dini tunakuwa hatuitendei haki nchi yetgwu wala sisi wenyewe.

Kwa sababu, hebu tufikiri pamoja kwa sauti, hivi katika hili Ukatoliki au watawa Wakatoliki wamehusika vipi, Je, mtangazaji huyu anaweza kusema kwa uhakika aliyosema anawasemea Waislamu, amefanya utafiti kiasi gani au akajiridhisha kwa kiwango gani suala hili linahusu Ukristo na Uislamu?

Hapana, tusilifikishe taifa hili mahali ambapo halitakuwa tena taifa moja tunalojivunia sasa kwa ajili tu ya kuwanufaisha watu wachache au kwa maslahi ya nani sijui. Hatimaye Tanzania kwa Watazania ni juu ya kila kitu, utaifa wetu unakuja kwanza na mengine yatakuja baadae, tutumie nafasi zetu na mamlaka tuliyo nayo katika jamii kuhakikisha tunahamasisha umoja zaidi kuliko kupandikiza mbegu za kutugawa, tunaweza kudhani ni mbegu ndogo sana, lakini madhara yake ni makubwa kuliko tunvyoweza kufikiri.
Wapo miongoni mwetu, wanachukulia kitu wanachosikia redioni, runigani, au kwenye gazeti kama ni ukweli halisi wa kila jambo, kwa hiyo hata kama tunafanya masihara tusifanye masihara ya hatari namna hiyo, historia ya taifa hili isije ikatuandika kwenye kitabu cheusi.
Mungu ibariki Tanzania

Sosi: Tanzania Daima





Huyu mdudu anayeitwa Kibonde, mimi simwelewi kabisa uwezo wake na namna anavyotumia Clouds FM kwa kueneza ujinga wake. Sijui hata mwajiri wake anawaza nini? Siku zote anaendelea kumwangalia anaivunjia heshima Clouds FM? Nadhani ifike wakati kwa mwajiri wake amwangalie upya kama anazo sifa za kufanya kazi hii anayoifanya ama la. Ni wazi kwamba uwezo wake wa kuchambua mambo ni mdogo sana hivyo kazi anayoifanya ipo juu ya uwezo wake.
 
Hivi yule mkuu wa wilaya alikuwa amevaa Hijab au mtandio? Hiajab na mtandio, vyote ni sawa?
 
Naomba ni kiri kuwa hii thread ni nzuri sana na imelenga kustawisha jamii yetu ya Tanzania..naomba ni declare interest..mimi sio muumini wa dini yeyote ile kwa wenzetu ninaweza kujitanabahisha kama "atheist" ila mimihakuna kitu kina nichukiza sana kama watanznia tukigawanyika eti kwa sababu ya tofauti zetu za kiimani. Na hapa tatizo kubwa linalo ni kabili ni kuwa hizi dini sasa zinafundisha nini? kama kweli zinafundisha upendo mbona tusiishi pamoja kwa Upendo??? Hizi dini zote zimejaa ubinafsi, uchoyo na kutawaliwa na maamuzi ya watu binafsi kuamua kama wanavyo jisikia. la pili ni hili la vyombo vya habari navyo vimekuwa mwiba mbaya kwa ustawi wa taifa letu..tuna ushahidi wa redio kadhaa hapa Afrika kutumika kama kichocheo cha vurugo, Rwanda na Kenya imekuwa mifano iliyo waadhi wa habari za upotoshaji na uchchezu hadi machafuko yakatokea kwenye nchi husika, sasa Kibonde na Clouds Fm naona wanatupeleka huko> Binafsi kibonde nilikua nikimkubali ila sasa naona sifa zimemzidi na anapo elekea sipo
 
I was once a fan of Jahazi la Clouds FM, but now I don't bother if I have tuned it or not. Kibonde, akumbuke kuwa kuna mtangazaji huko Kenya, anaitwa Arap Sang, yuko mbele ya Ocampo huko Hague kwa mizaha na upuuzi wa namna hiyo. Anaweza kudhani kuwa ni jokes na kufurahisha barza lakini kumbe kuna Wapumbavu walio tayari kufanyia kazi mizaha yake.

Amani kwako Kibonde, fanya mizaha mambo mengine lakini si kuchakachua siasa na dini.
 
Back
Top Bottom