BAKWATA, Clouds FM huko mwendako siko!As-Salamu Alaykum

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,271
669
HISTORIA ya dunia hii imesheheni ushahidi wa kutosha kabisa kutuonyesha kwamba mambo makubwa makubwa ya kutisha chni ya jua yameanza kama masihara na katika vitu vidogo vidogo tu ambavyo watu wangeweza kudhani kwamba havina maana wala msingi wowote.

Ndiyo maana watu makini na viongozi mahiri duniani kote hawapuuzi mambo yanayodhaniwa na wengi kuwa ni madogo au ni ya kupuuzwa, hii ni kwa sababu mambo madogo yasipoangaliwa kwa makini yanaweza kutumiwa na watu wachache yakakuzwa na hata kuwa balaa kwa taifa na jamii husika.
Ninazungumzia kile kilichotokea kwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Mama Fatma Kimario na wafuasi wanaodhaniwa kuwa ni wa CHADEMA. Wakati hakuna mtu mwenye akili zake timamu, ikiwemo safu hii, anaweza kuunga mkono vurugu za aina yeyote ile au matumizi ya aina yoyote ile ya nguvu katika kutatua tatizo, wako watu wanaonyesha kila dalili za kulishadidia suala hili kwa maslahi ya kisiasa.

Na kwa muktadha huo, safu hii inajikita katika kujadili masuala mawili yatokanayo na sakata hilo, kwanza ni taarifa ya BAKWATA na BASUTA kutaka CHADEMA iombe radhi Waislamu kwa kuwa wamemdhalilisha mama huyo kwa kumvua hijabu (au mtandio aliokuwa amejitanda kichwani kama maadili ya Kiislamu yanavyowataka wanawake wa Kiislamu wawe).

Kama ambavyo mchangiaji mmoja katika mtandao wa Jamii Forum alivyochangia kuwa “Ndugu zangu Waislamu kwa hili mnapotoka sana. Padri aliyebaka hawezi kusubiriwa avue kanzu yake ndio akamatwe, vazi ni nini kwani? Vazi si alama ya imani ya Uisilamu bali ni utambulisho ambao hata shetani anaweza kujigubika humu. Uisilamu ni upendo, ni moyo wa kujali haki na kuzingatia uadilifu tunapopewa majukumu ya kusimamia haki vitu ambavyo DC yule kwa siku ile alivikosa. Chonde sana viongozi wa BAKWATA na BASUTA tuepuka kuingia kwenye siasa kwa kuwagawa Watanzania kwa kutumia imani zetu hata pale ambapo hakuna uhusiano”Ninaamini Clouds FM wanalijua hili, lakini katika moja ya vipindi vyao, mtangazaji wao( Epharim Kibonde) akizunguza kuhusu sakata hili la Mkuu wa Wilaya wa Igunga, amenishtua na kwa hakika nimeogopa. Mtangazaji huyo katika moja ya vipindi anapolivisha suala hili sura ya kidini kwa kiwango kile, huku akijua kuwa wasikilizaji wake wana viwango tofauti sana vya uelewa sijui alikuwa anadhamiria kuiambia nini jamii.

Mtangazji huyu amekwenda mbali (mbali sana) kupandikiza hisia za udini wa hali ya juu kwenye suala hili, anapozungumzia habari za kwamba eti Waislamu nao wakifikia hatua ya kuwavua watawa Wakatoliki vilemba vyao kama alivyofanywa mkuu wa wilaya, kwa hakika hii ni hatari sana kwa umoja na mshikamano wa taifa hili.

Maadili ya taaluma hii yanatutaka tusema ukweli tu na ukweli mtupu kwa manufaa ya ustawi na mshikamano wa jamii tuliyomo.
Tukifika mahali tukaanza kuwianisha hisia zetu au ushabiki wetu katika mambo tete na nyeti kama imani za dini tunakuwa hatuitendei haki nchi yetu wala sisi wenyewe.

Kwa sababu, hebu tufikiri pamoja kwa sauti, hivi katika hili Ukatoliki au watawa Wakatoliki wamehusika vipi, Je, mtangazaji huyu anaweza kusema kwa uhakika aliyosema anawasemea Waislamu, amefanya utafiti kiasi gani au akajiridhisha kwa kiwango gani suala hili linahusu Ukristo na Uislamu?

Hapana, tusilifikishe taifa hili mahali ambapo halitakuwa tena taifa moja tunalojivunia sasa kwa ajili tu ya kuwanufaisha watu wachache au kwa maslahi ya nani sijui. Hatimaye Tanzania kwa Watazania ni juu ya kila kitu, utaifa wetu unakuja kwanza na mengine yatakuja baadae, tutumie nafasi zetu na mamlaka tuliyo nayo katika jamii kuhakikisha tunahamasisha umoja zaidi kuliko kupandikiza mbegu za kutugawa, tunaweza kudhani ni mbegu ndogo sana, lakini madhara yake ni makubwa kuliko tunvyoweza kufikiri.
Wapo miongoni mwetu, wanachukulia kitu wanachosikia redioni, runigani, au kwenye gazeti kama ni ukweli halisi wa kila jambo, kwa hiyo hata kama tunafanya masihara tusifanye masihara ya hatari namna hiyo, historia ya taifa hili isije ikatuandika kwenye kitabu cheusi.
Mungu ibariki Tanzania

Sosi: Tanzania Daima
 
Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,271
669
Kwa kueneza udini ndo maana wanakuja na kipindi cha As-Salamu Alaykum
hii yote ni kuubili udini udini
isipokomeshwa akianane zogo la udini likianza watu wataanzaia clouds fm
 
The Dude

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
1,029
444
Hakuna siku nlikereka kama siku ile naskiza kipindi cha kibonde..nina mashaka na utashi na upeo wa kibonde ktk masuala mtambuka yagusayo kijamii..yeye huropoka ropoka tu bila kujali as long as he‘s certain some ccm guys r pleased!
 
Bornvilla

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
924
267
Kwa kueneza udini ndo maana wanakuja na kipindi cha As-Salamu Alaykum
hii yote ni kuubili udini udini
isipokomeshwa akianane zogo la udini likianza watu wataanzaia clouds fm

Ubongo wako haufiri vyema! Assalaam-aleykum=amani iwe juu yenu/yako. Hiyo ni lugha tu. Haimaanishi kuwa ndio uislam,sasa nikuulize! Waarabu wakristo wanasalimianaje? Acha fikra za kitoto. Kuhusu Kibonde ni kuwa yuko sawa kwa alichokisema! Hivi ikidhibitika mtawa amevuliwa kilemba ninyi mtaichukuliaje? Hata kama kweli amekosea kwanini usimhukumu kwa busara? Jamani tuheshimiane kama twaipenda amani la sivyo mambo yatachafuka tukose pa kukimbilia.Mzarau mwiba mguu huota tende.
 
Ngofilo

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
220
65
Acheni ujinga wa kufikiri Watawa ni wakatoriki wamehusika vipi na huyo kada wa ccm aliyevuliwa hijab,,cku zote ukiongelewa ukristo hawa waislam lazima waongelee kanisa katoriki kwa nini.kwanini huyo kibonde asiseme mlokole anatolea mfano wa masista wa katoriki..KIBONDE anafikiri kwa kutumia makalio cku zote kwani hamumujui tokea yuko CTN,nini kilimtoa huko au anataka tuseme ukweli wake...Ulizeni elimu yake mtamsamehe.
 
The Dude

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
1,029
444
Binafsi sitetei dini yoyote kuwa attacked imani zake. Isipokuwa nakemea uozo wa kibonde..ana upeo duni sana kiasi kwamba kumruhusu azungumzie mada sensitive inayogusa imani za watu namna hiyo ni kuhamasisha uchochezi..oneni yule mtangazaji wa kenya saivi ana kesi ICC ya international crimes
 
Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,271
669
Ubongo wako haufiri vyema! Assalaam-aleykum=amani iwe juu yenu/yako. Hiyo ni lugha tu. Haimaanishi kuwa ndio uislam,sasa nikuulize! Waarabu wakristo wanasalimianaje? Acha fikra za kitoto. Kuhusu Kibonde ni kuwa yuko sawa kwa alichokisema! Hivi ikidhibitika mtawa amevuliwa kilemba ninyi mtaichukuliaje? Hata kama kweli amekosea kwanini usimhukumu kwa busara? Jamani tuheshimiane kama twaipenda amani la sivyo mambo yatachafuka tukose pa kukimbilia.Mzarau mwiba mguu huota tende.

ili kubalance story kwanini asiweke maneno kama tumsifu yesu...... bwana asifiwe.... sharom........etc
hii inaonesha kuwa Radio unaegemea upande wa dini fulani
 
It is Sur_Plus

Senior Member
Sep 28, 2010
167
7
HISTORIA ya dunia hii imesheheni ushahidi wa kutosha kabisa kutuonyesha kwamba mambo makubwa makubwa ya kutisha chni ya jua yameanza kama masihara na katika vitu vidogo vidogo tu ambavyo watu wangeweza kudhani kwamba havina maana wala msingi wowote.

Ndiyo maana watu makini na viongozi mahiri duniani kote hawapuuzi mambo yanayodhaniwa na wengi kuwa ni madogo au ni ya kupuuzwa, hii ni kwa sababu mambo madogo yasipoangaliwa kwa makini yanaweza kutumiwa na watu wachache yakakuzwa na hata kuwa balaa kwa taifa na jamii husika.
Ninazungumzia kile kilichotokea kwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Mama Fatma Kimario na wafuasi wanaodhaniwa kuwa ni wa CHADEMA. Wakati hakuna mtu mwenye akili zake timamu, ikiwemo safu hii, anaweza kuunga mkono vurugu za aina yeyote ile au matumizi ya aina yoyote ile ya nguvu katika kutatua tatizo, wako watu wanaonyesha kila dalili za kulishadidia suala hili kwa maslahi ya kisiasa.

Na kwa muktadha huo, safu hii inajikita katika kujadili masuala mawili yatokanayo na sakata hilo, kwanza ni taarifa ya BAKWATA na BASUTA kutaka CHADEMA iombe radhi Waislamu kwa kuwa wamemdhalilisha mama huyo kwa kumvua hijabu (au mtandio aliokuwa amejitanda kichwani kama maadili ya Kiislamu yanavyowataka wanawake wa Kiislamu wawe).

Kama ambavyo mchangiaji mmoja katika mtandao wa Jamii Forum alivyochangia kuwa "Ndugu zangu Waislamu kwa hili mnapotoka sana. Padri aliyebaka hawezi kusubiriwa avue kanzu yake ndio akamatwe, vazi ni nini kwani? Vazi si alama ya imani ya Uisilamu bali ni utambulisho ambao hata shetani anaweza kujigubika humu. Uisilamu ni upendo, ni moyo wa kujali haki na kuzingatia uadilifu tunapopewa majukumu ya kusimamia haki vitu ambavyo DC yule kwa siku ile alivikosa. Chonde sana viongozi wa BAKWATA na BASUTA tuepuka kuingia kwenye siasa kwa kuwagawa Watanzania kwa kutumia imani zetu hata pale ambapo hakuna uhusiamkuu naomba ufanye kuhusisha hizo sentensi mbili zenye red colour.Nadhani utakua umeshajua ni kwanamna gani unajichanganya katika mada yako na kwamba unatolea hukumu jambo ambalo hujalielewa TAMBUA KWAMBA UISLAMU SI KUJIONYESHA KAMAULIVYO SEMA KWAMBA HIJJAB NI ISHALA TU KATIKA JAMII JAMBO LISILO LA KWELI HATA KIDOGO UISLAM UNAHUKUMU ZAKE AMBAZO MWANADAMU YEYOTE HAWEZI KUZIBADIRISHA NA KUWEKA KTK FIKRA ZAKE NA NAIKAKUBARIWA KATIKA UISLAMU.KITENDO CHAKUSEMA HIJJAB NI ALAMA AU UTAMBULISHO WA UISLAMU SIKWELI BALI HIJJAB NI STARA AMBAYO MWISLAMU KAAMRISHWA AIVAE SO NI NILAZIMA AWE KATIKA MAZINGIRA HAYO MUDA WOTE. Mimi binafsi siungi mkono jambo ambalo KIBONDE amelifany BUT ninacho kupinga ni wewe kuchanganya kauli ya kibonde kanakwamba katumwa na bakwata. Bakwata take yao ilikua ni kwenye hijjab suala ambalo lilitokea
 
Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,271
669
Hii Redio isipokemewa kwa kupandikiza udini
siku zinazokuja hali itakuwa mbaya Tanzania
 
Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,271
669
mkuu naomba ufanye kuhusisha hizo sentensi mbili zenye red colour.Nadhani utakua umeshajua ni kwanamna gani unajichanganya katika mada yako na kwamba unatolea hukumu jambo ambalo hujalielewa TAMBUA KWAMBA UISLAMU SI KUJIONYESHA KAMAULIVYO SEMA KWAMBA HIJJAB NI ISHALA TU KATIKA JAMII JAMBO LISILO LA KWELI HATA KIDOGO UISLAM UNAHUKUMU ZAKE AMBAZO MWANADAMU YEYOTE HAWEZI KUZIBADIRISHA NA KUWEKA KTK FIKRA ZAKE NA NAIKAKUBARIWA KATIKA UISLAMU.KITENDO CHAKUSEMA HIJJAB NI ALAMA AU UTAMBULISHO WA UISLAMU SIKWELI BALI HIJJAB NI STARA AMBAYO MWISLAMU KAAMRISHWA AIVAE SO NI NILAZIMA AWE KATIKA MAZINGIRA HAYO MUDA WOTE. Mimi binafsi siungi mkono jambo ambalo KIBONDE amelifany BUT ninacho kupinga ni wewe kuchanganya kauli ya kibonde kanakwamba katumwa na bakwata. Bakwata take yao ilikua ni kwenye hijjab suala ambalo lilitokea

mkuu kama ulisikiliza vizuri hayo maneno yalisemwa na kibonde
kukandamiza dini za watu wengine
 
mustiss

Member
Jul 5, 2011
15
5
kiukwel jamaa alitumia sana ukada wa ccm kuendesha kipind, pia ajitahid kufanya tafiti za kutosha kabla ya kuropoka upuuz wake.
 
Memo

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
2,157
759
Hii inaitwa warming up for the dark ahead of us.
Kibonde anarusha ngumi kwenye mwanga, akijifanya hajui anayempiga.....ngoja giza litakapotua 2015 ndio kitajulikana!
Haya mambo ni mabaya sana!
Hii Redio isipokemewa kwa kupandikiza udini
siku zinazokuja hali itakuwa mbaya Tanzania
 
BPM

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,761
572
huyu bwana kibonde huwa ana mada nzuri lakini hutaka kuendesha kutokana na utashi wake yeye kama yeye na si uelewa kwa ujumla
 
Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
47,133
17,103
historia ya dunia hii imesheheni ushahidi wa kutosha kabisa kutuonyesha kwamba mambo makubwa makubwa ya kutisha chni ya jua yameanza kama masihara na katika vitu vidogo vidogo tu ambavyo watu wangeweza kudhani kwamba havina maana wala msingi wowote.

Ndiyo maana watu makini na viongozi mahiri duniani kote hawapuuzi mambo yanayodhaniwa na wengi kuwa ni madogo au ni ya kupuuzwa, hii ni kwa sababu mambo madogo yasipoangaliwa kwa makini yanaweza kutumiwa na watu wachache yakakuzwa na hata kuwa balaa kwa taifa na jamii husika.
Ninazungumzia kile kilichotokea kwa mkuu wa wilaya ya igunga, mama fatma kimario na wafuasi wanaodhaniwa kuwa ni wa chadema. Wakati hakuna mtu mwenye akili zake timamu, ikiwemo safu hii, anaweza kuunga mkono vurugu za aina yeyote ile au matumizi ya aina yoyote ile ya nguvu katika kutatua tatizo, wako watu wanaonyesha kila dalili za kulishadidia suala hili kwa maslahi ya kisiasa.

Na kwa muktadha huo, safu hii inajikita katika kujadili masuala mawili yatokanayo na sakata hilo, kwanza ni taarifa ya bakwata na basuta kutaka chadema iombe radhi waislamu kwa kuwa wamemdhalilisha mama huyo kwa kumvua hijabu (au mtandio aliokuwa amejitanda kichwani kama maadili ya kiislamu yanavyowataka wanawake wa kiislamu wawe).

kama ambavyo mchangiaji mmoja katika mtandao wa jamii forum alivyochangia kuwa "ndugu zangu waislamu kwa hili mnapotoka sana. Padri aliyebaka hawezi kusubiriwa avue kanzu yake ndio akamatwe, vazi ni nini kwani? Vazi si alama ya imani ya uisilamu bali ni utambulisho ambao hata shetani anaweza kujigubika humu. Uisilamu ni upendo, ni moyo wa kujali haki na kuzingatia uadilifu tunapopewa majukumu ya kusimamia haki vitu ambavyo dc yule kwa siku ile alivikosa. Chonde sana viongozi wa bakwata na basuta tuepuka kuingia kwenye siasa kwa kuwagawa watanzania kwa kutumia imani zetu hata pale ambapo hakuna uhusiano"ninaamini clouds fm wanalijua hili, lakini katika moja ya vipindi vyao, mtangazaji wao( epharim kibonde) akizunguza kuhusu sakata hili la mkuu wa wilaya wa igunga, amenishtua na kwa hakika nimeogopa. Mtangazaji huyo katika moja ya vipindi anapolivisha suala hili sura ya kidini kwa kiwango kile, huku akijua kuwa wasikilizaji wake wana viwango tofauti sana vya uelewa sijui alikuwa anadhamiria kuiambia nini jamii.

mtangazji huyu amekwenda mbali (mbali sana) kupandikiza hisia za udini wa hali ya juu kwenye suala hili, anapozungumzia habari za kwamba eti waislamu nao wakifikia hatua ya kuwavua watawa wakatoliki vilemba vyao kama alivyofanywa mkuu wa wilaya, kwa hakika hii ni hatari sana kwa umoja na mshikamano wa taifa hili.

Maadili ya taaluma hii yanatutaka tusema ukweli tu na ukweli mtupu kwa manufaa ya ustawi na mshikamano wa jamii tuliyomo.
Tukifika mahali tukaanza kuwianisha hisia zetu au ushabiki wetu katika mambo tete na nyeti kama imani za dini tunakuwa hatuitendei haki nchi yetu wala sisi wenyewe.

Kwa sababu, hebu tufikiri pamoja kwa sauti, hivi katika hili ukatoliki au watawa wakatoliki wamehusika vipi, je, mtangazaji huyu anaweza kusema kwa uhakika aliyosema anawasemea waislamu, amefanya utafiti kiasi gani au akajiridhisha kwa kiwango gani suala hili linahusu ukristo na uislamu?

Hapana, tusilifikishe taifa hili mahali ambapo halitakuwa tena taifa moja tunalojivunia sasa kwa ajili tu ya kuwanufaisha watu wachache au kwa maslahi ya nani sijui. Hatimaye tanzania kwa watazania ni juu ya kila kitu, utaifa wetu unakuja kwanza na mengine yatakuja baadae, tutumie nafasi zetu na mamlaka tuliyo nayo katika jamii kuhakikisha tunahamasisha umoja zaidi kuliko kupandikiza mbegu za kutugawa, tunaweza kudhani ni mbegu ndogo sana, lakini madhara yake ni makubwa kuliko tunvyoweza kufikiri.
Wapo miongoni mwetu, wanachukulia kitu wanachosikia redioni, runigani, au kwenye gazeti kama ni ukweli halisi wa kila jambo, kwa hiyo hata kama tunafanya masihara tusifanye masihara ya hatari namna hiyo, historia ya taifa hili isije ikatuandika kwenye kitabu cheusi.
Mungu ibariki tanzania

sosi: Tanzania daima

mkuu huyo shetwani kibonde asikuumize kichwa atiiiiiiiiii
anasubiri the hague 2015...hana tofauti na yule mtangazaji wa kenya ....huyu naogopa kama si kuona aibu wazazi wamkewe wakati wakimpa mke kama walikuwa wametoka skatriki ama lah...sidhani mwenye akili za kawaida waweza kumpa mtoto waako kama ephraimu kibonde ...anapoelekea hana tofauti na freemassons huyu
 
Guyton

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
263
78
hivi kuna members wa jf huwa mnasikiliza cloud fm?? au siku hiyo mlipitiwa??
 
Guyton

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
263
78
mkuu huyo shetwani kibonde asikuumize kichwa atiiiiiiiiii
anasubiri the hague 2015...hana tofauti na yule mtangazaji wa kenya ....huyu naogopa kama si kuona aibu wazazi wamkewe wakati wakimpa mke kama walikuwa wametoka skatriki ama lah...sidhani mwenye akili za kawaida waweza kumpa mtoto waako kama ephraimu kibonde ...anapoelekea hana tofauti na freemassons huyu

freemasons they are elite and very intelligent, huyo jamaa mtafutie size yake ya kumfananisha.
 
KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,601
11,849
Kwa kueneza udini ndo maana wanakuja na kipindi cha As-Salamu Alaykum
hii yote ni kuubili udini udini
isipokomeshwa akianane zogo la udini likianza watu wataanzaia clouds fm

Angekua anatoa salaam ya 'Bwana Yesu Asifiwe" waislam wangetishia kuandamana kupinga hiyo salaam.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom