Makamu mweyekiti wa BAKITA ( Omari Kiputiputi), amesema neno "king`amuzi" halijasanifiwa na linatumika kwa makosa katika kifaa cha televisheni. Amesema, "king`amuzi ni kile kitu ambacho huwezi kukiona kwa macho kwa mfano, mashine maalumu ya kugundua mabomu ardhini" Alisema neno sahihi linalotakiwa kutumika kama jina la kifaa hicho ni "kisimbuzi" na si "king`amuzi" kama linavyojulikana.Source: Ngoji .A (2012,machi 23).Bakita:king`amuzi si Kiswahili sanifu. Mwananchi, 057331, 10.