Bakhresa tuonelee huruma wapemba

Bakhresa tuonelee huruma wapemba

pole mkuu hii imenkera hata miee Yakhee Huyu bakhresa asijifanye ana chongo wakti ana macho mambili.
 
Kuna uhusiano gani wa ukubwa wa mkondo nå books vyake anavouzia vyakula nå vinywaji ushenzi nå roho mbsya tu usiojali utu ukajali kitu.

Aaah kijana waswahili wanasema ukichinja kuku wa mwenzako miguu ya kuelekea ww yuko kifaida zaidi hivi hujiulizi Bakhresa katoka kisiwa gani sikwamba asaidii anasaidia sasa sianawapa nafasi wengine wapate riziki zao

Pray for him anunue Meli nakununua meli shughuli pevu kijana na sivile vibot sijui kilimanjaro,seabus havina uhimili Wakuhimili mkondo kuwa muelewa au mnataka kufa km mafungu km mv spice au kusafiri roho juu nilisikiaga kilimanjaro ilizidiwa na watu waliokuwa nje ya boat wakafa maji.
 
Maalimu tumekusikia poleni Sana,bila shaka bakhresa ujumbe ataupata tu...
 
Muanzisha uzi anamawazo potofu sana, usafiri wa abiria au ya raia hayapaswi kumtegemea mfanyabiashara mmoja na si suala la kuwaachia wafanya biashara kwa asilimia 100. Likiwa hivyo ndio madhara yake hayo na nyie abiria mmshaamini huyo bakhresa ndio mwenye wajibu huo hilo ni kosa. Wajibu huo ni wa serekali ya zanzibar kwa kushirikiana na wafanyabiashara.
 
Taarifa kwa Wazanzibari wenzangu na wengine kwa jumla ni kwamba meli mpya inayotengenezwa huko Korea, MV MAPINDUZI 2 inatarajiwa kufika Zanzibar mnamo mwaka 2015.
 
Mali ya smz ya bil 20 inamaliziwa kupata rangi in a kuja february
 
Kwa huyo sahauni.kwake pesa mbele kwa mbele.
Nilishawahi kuonana naye tukakubaliana biashara fulani lakiini akachukua idea yangu .
Sio mtu mkweli . Wala hasaidii masikini kwani anauza mpaka chapati na sambusa biashara ya watu wa chini.
So usitarajie chochote kutoka kwake.
 
Kuna uhusiano gani wa ukubwa wa mkondo nå viooks vyake anavouzia vyakula nå vinywaji ushenzi nå roho mbsya tu usiojali utu ukajali kitu. mi kilio change kwa nini anathamini kitu kuliko utu?

Kiuhalisia ujumbe wako nimeuelewa ila nakushauri ukiandika mada tafadhali ipitie tena,fanya marekebisho ya maneno yaliyokosewa ndipo uitume ili uweze kueleweka vizuri/kumsaidia msomaji aelewe kwa urahisi ujumbe wako.
 
Waambieni wabunge wenu,Hamad Rashid anaishi Mikocheni lakini ni mbunge wenu na akija mnamchagua tena ,yeye sio waziri na hana nyadhifa zozote za kumfanya aishi Dar, lakini anaishi Mikocheni Dar Es Salaam.Chagueni Watumbatu wenzenu mnaoishi nao huko huko ,hao ndio wanajua shida zenu,hata wabunge wanaoishi Unguja lakini ni wabunge wa Pemba wapigeni chini,kuandika hapakuhusu Bakhresa haisaidii kitu yeye anafanya biashara na hizo ni meli zake hamuwezi kumpangia,bali mnaweza kuiamuru serikali ya Zanzibar kuwanununulia meli ili kuondoa hiyo kadhia kwani Pemba ni Zanzibar,,kwa hiyo SMZ ina wajibu wa kuwahudumia wananchi wake pale inapoona wanapata shida,pia mwambieni Maalimu Seifu yeye ni kiongozi mkuu pia raisi Shein pia anatoka Pemba hao ndio wa kuwaambia na hao ndio mna haki nao lakini sio Bakhresa.

Mi mpemba, nimekuelewa mfianchi,asante sana
 
acha kulialia wewe,na wewe kuwa kama bakhresa kisha uwasaidie wapemba wenzako.........kama we unaijua dini kweli omba dua uwe kama yeye,usimlaumu bakhresa wa watu kama we unajua kulaumu mlaumu aliyefanya kuwe na tofauti kati ya wewe na bakhresa..........
 
Huyu jamaa kaandika kiswahili lakini sio hiki kilichosanifishwa. hiki cha kipemba. All in all tumekuelewa Mpemba.....ushauri wangu nadhani umejitahidi sana kutumia hili jukwaa as social network but ongeza juhudi za kupaste hiki kilio chako haswa kwenye zile offical page za facebook za makampuni yake anayomiliki kama azamtv, au azam fc n.k. Nadhani watakusikia zaidi na if possible tuma kama kero kwa wahariri wa magazeti mbalimbali then angalia kama malalamiko yako yatapewa nafasi ya kuchapishwa
 
Back
Top Bottom