Tetesi: Bakhresa kuhamia Rwanda

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,527
865
Baada zoezi la kupunguza wafanyakani takribani 150. miezi miwili iliyopita ili kuendana na gharama za uendeshaji wa kiwanda cha maji ya matunda.

Kuna fununu ya kuwa mpango mzima uliokuwepo kwa sasa ni kuhamisha kiwanda hicho na kukipeleka Nchini Rwanda,ambako kuna unafuu wa kodi ,hii hasa inatokana na kuelemewa na utitiri wa kodi ulioko nchini kwani kwa sasa hakuna ukwepaji wa kodi hivyo faida imepungua tofauti na huko nyuma kabla ya uchaguzi mkuu.
 
Bila shaka wewe ni kati ya wanaopaswa kunufaika na elimu ya bure. Uhamishe kiwanda Tanzania upeleke Rwanda (yenye idadi ya watu sawa na wilaya ya kinondoni!) Kuanzisha kiwanda inategemea upatikanaji wa wateja, malighafi, urahisi wa nguvu kazi n.k jiulize Rwanda wana sifa zipi kuishinda Tanzania?
 
Huyu tayari Ana viwanda Rwanda. Anajua anachokifanya.
 
Soma katiba ya Zanzibar utagundua kuwa zenji ni nchi yenye bendera, wimbo nk.
Kwani wewe hukumbuki walivyomkomalia Mzee Pinda, pale alipokanusha bungeni kuwa si nchi?
 
Hiyo nchi ipo bara gani?
1. Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la
Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka
na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
2. Zanzibar ni miongoni mwa Nchi mbili zinazounda Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.

2A. Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali, Rais
aweza kuigawa Zanzibar katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo
kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la
Wawakilishi. ................

Soma Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
 
Wanaolipa kodi bila figisufigisu watabaki na hao ndio wenye kwa nchi,utitili wa viwanda nyonyaji hauna faida kwa nchi bora tuwe na viwanda vichache vyenye faida.
 
Huyu Jamaa jiwe kweli.
Kwani hujui bakhresa kwamba amewekeza Rwanda miaka mingi?
Pia suala la kupunguza wafanyakazi pia linaendana na Technology.
Technology ikiongezeka ndio mjue na ajira zitapungua tu kwa nyie mnaopenda kuajiriwa.

Tambua kwamba Kiwanda Cha Maziwa Zanzibar ni kiwanda bora Ukanda wa Africa Mashariki,lakini wafanyakazi wake ni wachache mno kutokana na kwamba seheme nyingi sana na mfumo wa kiwanda ni wakujiendesha wenyewe.Ukienda pale unatashangaa teknolojia inatotumika pale.
Idadi ya watu wa Rwanda ni wachache sana,na lazima ujue wanahitaji soko gani
Tambua kwamba Bakhresa sio Njaa kali kama wewe,Team ya AZAM FC mfano ni kwamba pale yeye hapati chochote,anatoa mamilioni kwenye Ligi kuu kwa kila team.Sasa angekuwa mtu mwingine si angeachilia mbali tu.
Bado anaendesha kwa faida,tena sana,Kama umetoka Mkoani nakuhamia Dar umemjua Bakhresa juzi basi funga kopo ukae kimyaa,ujambe ulale.
Halafu wafanyakazi 150 kwa wafanyakazi ailioajiri bakhresa ni sawa na kapunguza tone la maji kutoka kwenye Bahari.

Bila shaka wewe ni kati ya wanaopaswa kunufaika na elimu ya bure. Uhamishe kiwanda Tanzania upeleke Rwanda (yenye idadi ya watu sawa na wilaya ya kinondoni!) Kuanzisha kiwanda inategemea upatikanaji wa wateja, malighafi, urahisi wa nguvu kazi n.k jiulize Rwanda wana sifa zipi kuishinda Tanzania?

hoja ya kizamani kabisa, nani kakuambia atauza rwanda tu? mbona tunakunywa alvaro ni ya hapa? mbona tunatumia blue band, tunatafuna apple za south afrika, hiv huoni bei ya rwenzori na kilimanjaro maji, nini tofauti ktk bei?!
 
Baada zoezi la kupunguza wafanyakani takribani 150. miezi miwili iliyopita ili kuendana na gharama za uendeshaji wa kiwanda cha maji ya matunda.

Kuna fununu ya kuwa mpango mzima uliokuwepo kwa sasa ni kuhamisha kiwanda hicho na kukipeleka Nchini Rwanda,ambako kuna unafuu wa kodi ,hii hasa inatokana na kuelemewa na utitiri wa kodi ulioko nchini kwani kwa sasa hakuna ukwepaji wa kodi hivyo faida imepungua tofauti na huko nyuma kabla ya uchaguzi mkuu.

Uongo mtupu.

Bakhresa hajawahi kuwa mkwepa kodi. Kinyume chake, Bakhresa ameshawahi kuwa mlipa kodi namba moja Tanzania.

Ikiwa ni uwekezaji nje ya nchi, pitia tovuti yao uone Bakhresa ameshawekeza viwanda nchi ngapi za Afrika. Mbali ya uwekezaji wa Duniani huko.

Wacha ufataani usio na mpango.
 
Back
Top Bottom