<br />Enzi za ba Mkapa haya yangetokea bungeni? Nani wa CCM angesimama hasiunge mkono hoja? Mapinduzi haya japo madogo yameletwa na nani? Nijuze
<br />Enzi za ba Mkapa haya yangetokea bungeni? Nani wa CCM angesimama hasiunge mkono hoja? Mapinduzi haya japo madogo yameletwa na nani? Nijuze
Amemtaja Juma Kapuya kama mwanahisa wa Kampuni ya Simons group iliyouziwa UDA, na anasema kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza sakata lote Kapuya nae alikuwepo, kwa hiyo ni kama kesi ya nyani kumpelekea ngedere, amemtaka Kapuya kudeclare interest na kuomba radhi kwa kuidanganya kamati.
Amesema serikali haitaki kutoa tamko kazi yake ni kuomba miongozo tu na kuchukua hiyo hela na kujenga mahekalu Ulaya.
Enzi za Mkapa angalau kazi ilikuwa inaonekana! Mkapa alikuwa mkali sana kwa mawaziri wake. Na hata ukiangalia pesa nyingi ya EPA na madudu mengine yalifanyika mwishoni kabisa wa utawala wake tena alipokuwa ameanza kuumwa miguu mara kwa mara. Serikali ya Mkapa ilikuwa inaweka malengo na inayasimamia kwa nguvu zote!
Hii serikali ya sasa ukiwauliza wameshafanya nini cha maana tangu waingie madarakani watajibu nini?
Nadhani kuna issue mbili ambazo ni muhimu kuziangalia. Mwananchi/Citizen kama watu wengine wamelichukulia suala hili kwa mwanga wa "kutouzwa halali" kana kwamba ingeuzwa kwa bei ya juu na halali basi kusingekuwa na issue. Kwangu mimi, tatizo ni zaidi ya kuuzwa kwa bei ya chini, tatizo langu ni kwanini UDA haikuchukua majukumu ya DAR na kubadilishwa kuwa huo wakala wa Usafiri wa Haraka? Kiakili na kimantiki haikubaliki kuona kwamba UDA iiliyoundwa kusimamia usafiri wa umma jijini la Dar haikubadilishwa na kuifanya iwe ndio DART - yaani angalau wangeweka iwe UDART kuonesha mabadiliko hayo. Tatizo langu ni kuwa kwa jiji kama Dar lenye wakazi milioni karibu 4 wengi wao wakiwa ni wa kima cha chini na kati usafiri wa umma ndio suluhisho sahihi kwa wakazi hao. Haiwezekani kila sikuw awatu wanalalamikia usafiri na congestion lakini hawaoni kwamba kwa mtindo uliopo sasa wanalazimisha watu wengi kuwa na magari yao hata kama si lazima kiuchumi.
Ningefurahi sana kama kungekuwepo na watu kule Mwananchi/Citizen ambao wangeweza kuarticulate hii issue kwa mwanga huo. Tatizo siyo bei ya UDA ilivyouzwa bali gharama ambayo wananchi wanalipa na taifa linalipa hasa jijini Dar kwa UDA kuuzwa.
Yataibuka mengiIddi Simba ni mwenyekiti wa Body ya UDA,Prof. Juma Kapuya mdau wa Simons group iliyouziwa UDA, na yule mwenyekiti wa Simons group(jina limenitoka)-ni rafiki wa karibu wa kibiashara na RW1 KIKWETE. Taratibu tunaanza kupata network ya ili diri.Hawa wote ni wenyeji wa ikulu, ni biashara kutoka Ikulu. Masikini Nyerere alikua hajui ikulu kuna biashara gani-Biashara zenyewe ndio hizi.
Wabunge wa CCM waliosema kuwa hawaipitishi bajeti walikuwa wanaimba ili kujifurahisha. In fact, mbunge wa CCM kutoisupport bajeti wanaitafsiri kama utovu wa nidhamu. Ya ngeleja yaliwashinda, lakini wangeipitisha tu