Bajeti ya Wizara ya Kazi na Ajira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ya Wizara ya Kazi na Ajira

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PrN-kazi, Aug 5, 2011.

 1. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Bajeti ya Wizara ya Kazi na Ajira ndo leo inasomwa: bila shaka walioko karibu na eneo la tukio wana mengi ya kutujuza hususani sisi wana-jamii wa JF.
   
 2. Wa kusoma

  Wa kusoma JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,315
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  ameshasema ajira zimeongezeka mara dufu unasubiri nini hapo?
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Tunahitaji mabadiliko makubwa ya sera ya ajira Tanzania.Soko la ajira limevamiwa na raia wa kigeni sheria ya kulinda ajira ya wafanyakazi waTanzania inahitajika haraka.Leo ukitembelea sekta yoyote unayoijua utakutana na wafanyakazi wenye uraia wa mataifa mbali mbali waKenya na waHindi wanaongoza.

  Jaribu kuangalia sekta ya utalii utashangaa mpaka tour guide ni wakenya na wazungu !!!.makampuni ya uwakala wa utalii eg A & K,Sokwe Asili,Leopard Tours,Serena lodges,TGT,Grumeti Reserves,B to B,Wldersun Safaris na Ranger Safaris zinaongoza kwa kuajiri wafanyakazi raia wa kigeni kuanzia jikoni,stores,accounts,mapokezi na madereva.

  Nauliza kuna sababu zipi za kuendelea kuwa na wizara ya Kazi na Ajira wakati kazi zinazoweza kufanywa na watanzania zimeporwa na wageni ?.Ukitembelea viwanda vinavyomilikiwa na waHindi utashangaa nchi hii inavyoendeshwa wahindi wamejazwa hakuna mfano wake.Juzi nilitembelea kiwanda cha kusindika mafuta ya alizeti SUNOLA nikakutana na waHindi wanahesabu magunia ya Alizeti.Ebu fikiria mgeni analetwa kuhesabu magunia ya Alizeti ?.
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Nimemfuatilia huyu Binti Kawawa anaonekana kuwa na akili, she has really impressed me kwa alivyochangia!
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kasema nini huyu binti Kawawa?
   
 6. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />
  Hata na hiyo ni habari; nashukuru kuipata.
   
 7. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hali ya ajira kwa vijana ni tata, na ni bomu tarajiwa. Inatakiwa mikakati thabiti ya kukuza sana uchumi ili kuzalisha ajira nyingi.
   
 8. c

  calmdowndear JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 602
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  tatizo la ajira ni dunia nzima..kuanzia america mpaka eurozone na jana wenyewe mmeona stocks zilivyo plument

  tatizo letu ni umeme ...huwezi kuwa na ajira kama umeme huna....unless JK alete major infrastructure projects kama Nairobi -Thika road
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280

  A
  . Kuna matatizo ambayo watanzania tuna paswa kubadiliaka&#8230;
  1.Uvivu 2. Kutokujari 3. kutokuwajibika 4. Lugha&#8230;kama kuna mtu anashughulika na makampuni ya utalii atakuwa anayafahamu haya vizuri jinsi watanzania tunavyofanya madudu kwa hayo niliyoyataja&#8230;

  B. kwenye kiwanda cha SUNOLA wale wahidi wana uraia wa Tanzania hivyo ni watanzania yaani utanzania wa makaratasi...
   
 10. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kama Tanzania ingejipanga tatizo la ajira lingekuwa dogo mno kama si kulimaliza kabisa ni kupe mfano kufungwa kwa kiwanda cha kutegeneza matairi(General Tyre) kumekosesha watanzania wangapi? ikumbukwe kilimo cha mpira kingepanuka na Tanzania ndiyo iliyokuwa inategemewa Afrika mashariki...kiwanda cha kutegeneza magunia nacho hivyo hivyo...Pamba kama tungekuwa na viwanda vya kutosha kilimo cha pamba kingeongezeka, watu wangeajiriwa kwenye viwanda husika na kutegeneza ngo kutoka hapa badala ya kusafirisha pamba kwenda nje...Kwenye blue tuko pamoja
   
 11. S

  Saracen Senior Member

  #11
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 147
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hivi mmeona presentation ya daraja la Kigamboni?
   
 12. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Tatizo la ajira haliwezi kuisha kirahisi kwani wanaoitwa wawekezaji wanakuja mikono mitupu na briefcase kisha wanahamisha fedha zote kwao, mafasi zote za juu wanakamata wao tena mishahara yao mikubwa mara hata 10 ya wazawa, pia hawawekezi chchote mitaji wanaiba hapa hapa. Mifano mizuri ni kampuni ya Airtel, Zantel, GGM, Kiwira, NASACO, TAZARA, TRC kila sehemu zimehujumiwa na viongozi na ajira za watu kwa maelfu zimeotea.
  JK anaota ndoto za kuongza ajira wakati kwa vitendo anazidi kupunguza ajira... hii ni n ini? (nahifadhi maneno)....Hakuna kiongozi yeyote wa CCm aliye serious kabisa
   
 13. F

  FJM JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nimebahatika kuona Waziri Gaudensia Kabaka na Naibu wake Makongoro wakijibu hoja/maswali ya wabunge jioni wakati wa hitimisho wa bajeti ya wizara ya kazi ajira na vijana. Tatizo kubwa nililoona na la msingi sana ni kwamba both Waziri na Naibu wake hawaonekani kujua mambo mengi kuhusu Wizara yao! Na hasa Makangoro, anaonekana hata haelewi maswali yaliyouliuzwa na matokeo yake anaishia kusoma vifungu vya sheria. Kwa mfano, mwenyekiti wa Kamati inayosimamia wizara hii Jennista Mhagama aliuliza nafasi ya Wizara katika kusimamia upatikanaji wa haki kwa wafanyakazi "wanyonge" pale mahakama inapoamuru. Makongoro anasema tatizo ni watu kutojua sheria!

  Jambo kubwa alilouliza Mhagama hapa ni "Haki za wanyonge". Hawa watu hawana uelewa mpana wa sheria yes, lakini wanaelewa pale wanapodhulumiwa. Hata hivyo ukweli ni kwamba baadhi ya wamiliki wa hivi viwanda i.e Jambo Plastic wana ukaribu na 'wakubwa' na hivyo wanakuwa na jeuri ya hata kutotii amri ya mahakama. Na hapa ndipo serikali kupitia wizara anayokalia Makongoro wangetakiwa wasimame na hawa wanyonge. Matokeo yake amejibu - hawajui sheria! Sasa Wizara inafanya nini ili hawa wanyonge wajue sheria?

  Lakini kubwa zaidi ni nafasi ya KITI CHA SPIKA kutosimamia hoja za wananchi kama zinavyowakilishwa na wawakilishi wao yaani wabunge. Nilitegemea Naibu Spika aliyekuwa anaongoza kikao atamke waziwazi kuwa waziri na naibu wake wamekuwa wanatoa majibu yasiyoridhisha na wanaonekana hata kutofahamu vizuri mambo mengi yanayot0kea katika wizara hii. Hivyo angewapa muda i.e 24hrs waje na majibu! Hii ndio tafsiri halisi ya nini maana ya kuwa na kiti cha spika.

  Kama kuna mtu yuko karibu na Makongoro na bosi wake Mama Kabaka basi wawape somo maana majibu yao leo bungeni yameanika utupu wao 'upstairs'. They just dont seem to know what is happening around their Ministry. What a shame!
   
 14. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #14
  Aug 5, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Nilidhani wangezungumzi ku ammend the Employment & Labour Relation Act no 6, imejaa wizi mtupu, Kapuya na Kipenka waliiforce ipite in favour of the Employers/Owners.
   
 15. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hakuna mikakati maalumu ya serikali katika kuwapatia ajira wananchi wake.
   
 16. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  ni hatari kubwa sana kuwa na mawaziri wasio jua nini maana ya unaemployment au watu wasio na uhai. wakulima wa kitanzania ni wale watu wanaowakilisha jamii ya watu wasio na uhai, pamoja na wavuvi na wauza sokoni. Wizara ya kazi na Ustawi wa jamii maana yake , ni wizara inayohusika katika kujenga working class na kuwapeleka watu katika dalaja la pili kimaisha katika jamii. Yaani watu wenye uwezo wa kujihudumia wenyewe kiafya,kielimu,kupata mikopo benki ya kutatua matatizo yao na kuborsha maisha ya familia zao. Yaani watanzania wote waishi ki-oysterbay type.

  Unapokuwa na waziri asiyejua nini maana ya wizara ya kazi na ana -thubutu kusema watu wasio na kazi hawajui sheria. Huyu waziri ni hatari ni hatari katika jamii kupita hata majambazi sabini wenye mastola. nani sasa ategemewe kuwasafilisha wanyonge kuelekea katika maisha ya daraja la pili, kama siyo yeye? Kasumba ya maisha ya kitanzania ni kuwa mtu kuishi maisha ya daraja la pili lazima uwe msomi, viongozi wote wenye kasumba hii, hawajengi nchi ila wnatesa wanyonge.

  Baba akizaliwia katika nyumba ya nyasi, lazima mtoto wake azalie katika nyumba ya bati na mjukuu wake naye aolee na kushi katka nyumba ya vigae. haya ndio masiha ya kusafilisha mnyonge toka mashambani mpaka maisha ya mjini . Ndio maana tuna waziri na wizara ya kazi.

  Kuwapatia watu kazi ni muhimu kupita kabisa kuwapatia watu kadi za chama. Viwanda vya wawekelezaji lazima viwe na masharti mazuri ya kuwekeleza ili mzalendo apewe kipaumbele. Lakini wakiwa na amsharti ya kutaka raia zao waletwe kufanya kazi na kutaka watanzania wafaidike kidogo katika ajira. Huo tena ni utumwa na safari ya mnyonge kuelekea maisha ya dalaja la pili katika jamii yatagonga mwamba. Tutajikuta tuna viwanda vingi lakini ajira kwa mzawa ni kero.

  NI vizuri kabisaa kuwatafuta wawekelzaji wa Ulaya, marekani na Israel wawekeze katika viwanda na kilimo, maana wao hawaleti watu wao kufanya kazi za wazalendo kama ilivyo kwa waasia au waarabu, bali wao wa ulaya , hufundisha wazalendo jinsi ya kufanya kazi zao.

  Mataifa ya ulaya marekani na Israel hayana shida ya kuwatafutia soko la Ajira watu wao nje ya nchi zao kama ilivyo kwa asia na uarabuni. Hivyo hata marekani akikodisha ardhi ya kulima mahekali mia, atafaidika mtanzania kwa kupata kazi. Naomba raisi amfukuze kazi waziri wa kazi na naibu wake pamoja na watendaji wakuu wote wa wizara ya kazi. La sivyo mnyonge wa nyumba ya nyasi atapata mjuukuu katika nyasi nae atazalia nyumba ya nyasi..
   
Loading...