Bajeti ya Wizara ya Elimu aliyoisoma Mh. S. Kawambwa haikidhi matakwa ya elimu bora

A4.

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
670
108
Bajeti ya Wizara ya Eliwu iliyosomwa na Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi mh.Shukuru Kawambwa bado kaikidhi matakwa ya elimu bora kwa watz hasa watoto wa masikini maana haijaeleza UVUMBUZI WA TATIZO LA UBORA WA ELIMU UNAOTOTOLEWA BAINA YA WATOTO WA MATAJIRI, VIONGOZI WAKUBWA NA MTOTO WA MASIKINI.

Watoto wa viongozi wengi hapa nchini hasa mawaziri wanasoma ng'ambo elimu bora wakati wale wa masikini wanasoma elimu duni hapahapa ili hao watoto wa viongozi walioenda kusoma mataifa mengine wakirudi wachukue nafasi za baba zao waendekee kuwatawala wale waliosoma elimu duni. Mfano mzuri ni mh. Mbunge wa Kalenga wa sasa.

Nilikuwa najiuliza siku zote kwanini waziri wa wizara hii SIO lakini yupo tu? Nilikuwa cjui ni mbunge wa Bagamoyo kwa Mkuu! Hakika bajeti ya wizara ya Elimu cyo ya kupitisha. Labda kama ni bajeti ya wizara mpya inayojulikana kama BRN.
 
Nachojua elimu nchi tz inapuzwa,inakejeriwa ikuluni,magengeni,sokoni,bungeni,vyuoni na hata kwenye vikao vya vyama.wizara nyeti kama elimu huwezi kumkabidhi mtu dhaifu na legelege na asie makini km.kawambwa ukategemea elimu bora.brn nichanzo cha mafungu ya madeo na maofisa elimu.walimu njaa hakika watoto wa masikini bajeti haiwaoni funga mkanda ili tubadili mfumo wa utawala 2015 utakaowajali masikini.vingnevyo haiwezekani
 
Kwanza nataka ku~declare interest kuwa mimi siyo mwl., japo niliwahi kufundisha lakini pia mwenza wangu ni mwalimu, hivyo natambua matatizo yaliyo katika sekta ya elimu.

UDUNI WA MASLAHI BORA KWA WALIMU HAUWEZI KUISHA KWA SABABU YA MFUMO. MFUMO ULIOPO WA KIBAGUZI. MAAFISA ELIMU, WAKUU WA IDARA ZA ELIMU, WAKUU WA SHULE NA VYUO, WANAPATA MARUPURUPU MENGI PLUS WIZI NA RUSHWA, MBALI NA MISHAHARA YAO, WAKATI WALIMU WANAWALEA NA KUWAFUNDISHA WANAFUNZI WAKIISHI KWA MSHAHARA PEKE YAKE LICHA YA UGUMU WA KAZI KIMASLAHI, KIMAZINGIRA, N.K.
INGEFAA WATUMISHI WOTE WAISHI KWA MISHAHARA BADALA WENGINE KUPENDELEWA KAMA MAAFISA ELIMU AMBAO WANAJAZA MAGHOROFA MIJINI KAMA MBUNGE MMOJA ALIVYODAI BUNGENI WAKATI HUO SHULE HAZINA NYUMBA ZA WALIMU?
VIONGOZI HAWA WAMEKUWA WAKIIKINGIA SERIKALI NA KUWAZUIA WALIMU KUDAI MASLAHI YAO.
 
Teh teh teh hata ipite miaka 1000 sifikiri itatosha. Maana bajeti za familia zetu tu bado ni tatizo itakuaje kwa ya elimu.
 
Niliwahi sema humu kuwa ccm haina nia njema na watu wa nchi hii kwani inafifisha elimu ili iweze kuwatawala kirahisi. Si mnaona wanavyochangia watu kuwa maskini? Pembejeo wanapeleka katikati ya msimu, bei za mazao duni kuliko, vyama vya ushirika kuwakopa wakulima, na mishahara duni kwa wafanyakazi hasa waalimu. Kama si njia yao ya kutudidimiza kwenye umaskini ni kitu gani? Wanasema ccm itatawala milele kwa maana ya kuzalisha wajinga mashuleni ambao mwisho wao ni maskini watakaokuwa wanahongwa chumvi na kofia ili kuuza kura zao. Tuikatae hali hii ya kututengenezea wajinga kwa namna yoyote itakayofaa.
 
Asante sana Magdalena Sakaya. Watoto wenu hawasomi TZ, ndo maana hamtaki kumwajibisha MZIGO KAWAMBWA.
 
Wamezingatia kuwa waacheni wafu wazikane wenyewe kwa wenyewe,shame on you kawambwa
 
Asante sana Lekule Laizer, umeonyesha uzalendo kukubali kusomesha watoto wote shule za kata. Usiunge hoja mkono hadi wazir aeleze hyo tofauti ya watoto wa matajiri na viongozi na mtoto wa mfugaji.
 
Mimi ni mwalimu kinachofanya elimu yetu kudorora kiasi hiki ni ugawanyi wa madaraka kwa watu wasio na sifa, pia kupuuzwa kwa walimu katika mambo mbalimbali yakiwemo maslahi yetu, kutoshirikisha walimu katika uandaaji mitaala na mambo kadha wa kadha. Naomba wanjf tuungane na mh mbatia na mh sakaya tudai haki za watoto wa maskini katika upande wa elimu, leo hii hayati mwl. J. K. Nyerere kwa kuanzisha chama cha mapinduzi kwa ajili ya kutetea maslahi ya wafanyakazi na wakulima na baada ya kifo chake kikawa ni chama cha matajiri tu. Natamani kulia mie jamani hii hali ya elimu yetu miaka 100 ijayo itakuwaje?
 
imekidhi kuzalisha division 5, yaani wauza maji stendi sio elimu ya kumkomboa mtanzania.
WATANZANIA TUSIWAKUBALI WATU WA AINA HII:israel:
 
Tupitishe sheria moja tu kuwa kila kiongozi amsomeshe mwanae hapa hapa TANZANIA tena shule za umma tuone kama hizo shule za umma hazitaboreshwa. WATANZANIA TUTAENDELEA KUWA LEGELEGE kama tunakubali mifumo legelege:israel:
 
Watoto wao wanasoma nje matibabu wanatibiwa nje wao na familia zao pale watasema wanao zema ndio?ndiooooo100%wasio sema ndio?wa tz maskini ambao mpaka tv ya kuwaona wakila maisha bungeni hana kama anayo ipo ka pambo amepigwa kingamuzi hanahela ya kingamuzi.
 
Mfumo huu mbovu.utendaji hata wa maofisa elimu wengi ni wa ovyo.haea huiba mafungu na misaada inayotolewa kwa ajili ya kuinua elimu wakisaidiana na wakuu eengi wa shule ambao huteuliwa na maofisa hao upendeleo..wakuu wengi wa shule ni vihiyo na kwa hilo tu usitarajie usimamizi makini wa taaluma.kwa vile wengi wanateuliwa kwa upendeleo nai huteua vihiyo wenzao il wawasaidie shuleni.ni mfumo wa kwapua haraka....ndicho kinachoendelea.auditor akatiwe fungu hesabu kamaliza ukaguzi....unahitajika mfumo wa kumaliza mchwa mashuleni vinginevyo hata hivyo vijisenti vitaishia kwenye mifuko ya maofisa elimu na maeakala wao(wakuu wa shule)
 
Kwanza nataka ku~declare interest kuwa mimi siyo mwl., japo niliwahi kufundisha lakini pia mwenza wangu ni mwalimu, hivyo natambua matatizo yaliyo katika sekta ya elimu.

UDUNI WA MASLAHI BORA KWA WALIMU HAUWEZI KUISHA KWA SABABU YA MFUMO. MFUMO ULIOPO WA KIBAGUZI. MAAFISA ELIMU, WAKUU WA IDARA ZA ELIMU, WAKUU WA SHULE NA VYUO, WANAPATA MARUPURUPU MENGI PLUS WIZI NA RUSHWA, MBALI NA MISHAHARA YAO, WAKATI WALIMU WANAWALEA NA KUWAFUNDISHA WANAFUNZI WAKIISHI KWA MSHAHARA PEKE YAKE LICHA YA UGUMU WA KAZI KIMASLAHI, KIMAZINGIRA, N.K.
INGEFAA WATUMISHI WOTE WAISHI KWA MISHAHARA BADALA WENGINE KUPENDELEWA KAMA MAAFISA ELIMU AMBAO WANAJAZA MAGHOROFA MIJINI KAMA MBUNGE MMOJA ALIVYODAI BUNGENI WAKATI HUO SHULE HAZINA NYUMBA ZA WALIMU?
VIONGOZI HAWA WAMEKUWA WAKIIKINGIA SERIKALI NA KUWAZUIA WALIMU KUDAI MASLAHI YAO.

Hiyo ilikuwa mwaka gani, angalia hela halisi ya wizara. Maafisa elimu wamechoka hao mpaka unawahurumia.
 
Back
Top Bottom