Bajeti ya Tanzania na Boda boda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ya Tanzania na Boda boda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee wa Usafi, Jun 23, 2012.

 1. M

  Mzee wa Usafi JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Mimi ni mmoja wapo ya Watanzania wachache tuliobahatika kupata kibaru angalau na kuingia kwenye mfumo rasmi wa kodi...PAYE. Pamoja na hilo pia nimekata health insurance hivyo nikiugua napata tiba kutoka kwa bima yangu... Ili nchi yoyote iendelee ni lazima ikusanye kodi na kuwajibika kutumia vizuri hizo kodi. Najua matumizi ya serikali ya magamba ni ya anasa hata kwa hicho kidogo wanacho kusanya....Nimesikitishwa zaidi na wabunge wetu kwa kushabikia boda boda wasitozwe kodi kisa kipato chao ni kidogo....Mimi nilidhani kuwa kila mtanzania anawajibu wa kulipa kodi kulingana na kipato chake anachopata sasa kwa nini wao wasichangie maendeleo ya nchi yao?. Hao boda boda hawalipa kodi na ndo wanaotumia facilities zote za serikali " hospitali" pale wanapopata ajali ambazo kwa sasa zimekithiri... Hao hao boda boda wanakodi piki piki kwa sh 5000 kwa siku, je kwa nini serikali isiwatoze hata sh 20,000 kwa mwaka. Hawa boda boda wengi wao hawana hata leseni ....ninalipa kodi kwa mwaka sawa sawa na mishahara yangu ya miezi mitatu na nusu ...Kila mtu anawajibu wa kulipa kodi kwa jinsi anavyopata....napinga kwa boda boda kutolipa kodi....
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli kila mtu anawajibika kulipa kodi! Na kwa kuwa viongozi na wanasiasa hawalipi kodi, hapa ndipo tatizo uanzia.
  Nadhani tunataka katiba mpya iweke wazi kwamba kila mtu anayegombea uongozi lazima awe na TIN na lazima awe ni mlipa kodi. Kushindwa kwake kufanya hivyo hatakiwi kupewa uongozi na ashitakiwe kwa kukwepa kulipa kodi
   
 3. Atukilia

  Atukilia JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 643
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Si haki watu wengine wasilipe kodi kwa sababu yeyote, kodi huwa na viwango sasa kuna maana gani kumkata PAYE mtu ambaye anamshahara wa shs 200,000 kwa mwezi wakati boda boda anapata zaidi ya hapo? nadhani wanasiasa wanaogopa kelele zao kama ilivyotokea Songea, sasa kila mlipa kodi akiamua kupiga kelele kodi italipwa? halafu boda boda inaua biashara ya teksi ambayo inalipa kodi hivyo mfumo wa mapato kupotea. Kifupi walipe kodi kama watu wengine na wawe na leseni na hizo pikipiki ziwe na namba maalum ya biashara. Najua watu watasema tukusanye kwenye migodi, sawa kuna udhaifu mkubwa huko lakini hakuondoi haja wao kulipa kodi based on equity theory
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Naona aibu sana nikilinganisha na jirani zetu wa East Africa kwamba Tanzania twajivunia ajira toka kwa boda boda,(badala madini gesi wafanyabiashara import nas export) na kilimo mazao ya bishara!!!!
  Njoo kwenye kodi wanategemea sana bia,sigara,simu......badala ya hapo juu!!!!!!!ni aibu sana sana kutegemea waagiza magari,sigara,bia,simu!!!
   
 5. SIM

  SIM JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 1,636
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  Nijuavyo mimi bodaboda wanalipia mapato 35000 kwa mwaka hiyo kodi unayoingelea ni ipi, au mnataka walipe ushuru wa maegesho???
   
 6. MotoYaMbongo

  MotoYaMbongo JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 1,858
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 160
  Acheni kelele, amueni 2015 sio mbali.
   
 7. M

  Mzee wa Usafi JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  hiyo sh 35,000 ni road lisence tu kaka....tunahitaji kodi ya mapato hasa kwa owners bana
   
 8. aikaruwa1983

  aikaruwa1983 JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,360
  Likes Received: 1,185
  Trophy Points: 280
  kodi kitu gani ww if huko uliko wanakukata kodi tafuta bdbd uje upinge mbung`a!!!
   
 9. EBENEZA MT

  EBENEZA MT JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 264
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  bodaboda wanalipa mapato 35000 tofauti na road license. na kila mwezi wanawapelekea wenye pikipiki 100,000 - 150,000 inategemea.
   
Loading...