Bajeti ya harusi ya gharama ndogo

Ushauri mzuri. Kingine Ni gaharama isiyo ya msingi ya keki na mapambo. Weka ndafu hata 2 ama 3, watu watakula nyama na kufurahi. Weka chakula na vinywaji. Wekeza kwenye mziki lakini achana na mc.
 
Acha kumwingiza mwenzio kwenye matatizo. Kwa ukumbi huo na idadi hiyo ya watu andaa pesa isiyopungua milioni 12
 
Tunaomba mchanganuo wa hiyo mil.5. Ukumbi, mapambo, chakula, usafiri, na mengineyo!!

Mkuu usikremu, ili kutoa mchanganuo rasmi, ni lazima jamaa adisclose baadhi ya vitu, wapi anaishi, kuna umbali gani na hotel or ukumbi atakaochukua, cost za hotel or ukumbi uliokusudiwa ni upi nk, nk!
...
Akidisclose yote haya naweza kumpigia hesabu na kumuekea na dots!
...
General overview milioni tano inatosha na kubaki!
Kwa mfano:
hoteli= mill 1
chakula= laki 5
Usafiri na malazi ya wageni= mill 1 na nusu
na hiyo mill 2 iliyobaki kwa vikorombwezo vingine!
...
Usifanye mchezo na mill 5 kwa watu 50 wewe!
Hiyo hela ni kubwa sana!
 

Kukremu kumekujaje tena...
Nadhani anachukulia maisha ya mjini, lets say Daslama. Mimi najifunza ndo maana nimeuliza, vitu common sana ni ukumbi na mapambo yake, usafiri wa maarusi na wageni, chakula na anasa zingine.. Labda tumuulize mleta uzi, ni mazingira gani, wapi anategemea ndoa/sherehe itafanyika wapi.
 
Usafiri na malazi ya wageni?! Kwa nini uwalipie wewe hoteli? SI wafikie kwa mabinamu zao?
 

Kaka nakupongeza kwa hatua ya kuepuka gharama zisizo muhimu katika suala la harusi. Nadhani ni wakati muafaka sasa kwa watu kutochangishwa kwa ajili ya harusi. Ikiwezekana tuwe twaandaa chakula kidogo na vitu kama vinywaji waalikwa wajinunulie. Vyema pia ikiwa harusi ikafanyika mchana.
 
LIKUD.. sijui kama utapendelea ndoa za kiserikali?

they are less expensive..

mambo mengine mtamaliziana mnakojua ninyi..
 
Last edited by a moderator:
1.Ukumbi=1,000,000

2.Mapambo=1,000,000

3.Vinywaji bia 3@=330,000

4.Chakula plate 12000=600,000

Mc & Music=600,000

Magari-
Wazazi pande zote mbili=300,000

Gari-Maharusi=400,000

Coaster(Waalikwa)=
150,000.

Jumla kuu=4,380,000
Balance=620,000(Dharura)
NAWATAKIA MAANDALIZI MEMA.
 
Usafiri na malazi ya wageni?! Kwa nini uwalipie wewe hoteli? SI wafikie kwa mabinamu zao?

Hahahahaaaa!
King'asti bora ulivyokoment hapo, nadhani LIKUD atazidi kuamini kama mill 5 ni nyingi kwa waalikwa 50!
...
Kama utaangalia vizuri hapo utagundua kuna kiwango kikubwa cha hela kimezi hapo!
 
Kwa budget hyo wafanya harusi Nzuri tu na ya maana, na kuna vpengere vingine hapo possibility ya kunusuru pesa bado ni kubwa; hivyo tulizeni mawazo hamna haja ya kupannic hela yatosha sana hiyo
 
Navyojua mimi harusi ya kawaida kama ulivyosema wewe kwa kuzingatia na idadi ya watu uliotaja laki2 inatosha kabisa, lakini nimegundua kuwa watu wengi siku hizi wanachanganya kati ya harusi na sherehe ya harusi, kama ni sherehe inategemea na wewe mwenyewe ulivyojipanga na unataka ikafanyikie wapi! Huwa sioni umuhimu wa watu kuteketeza mamilioni ya pesa kwa kitu ambacho ni kusherekea tu maharusi wengi huwa na changamoto nyingi na uwezo wa kupata hela nyingi wakati mmoja huwa taabu, watafutieni japo kiwanja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…