Bajeti Mpya ya Serikali Kuinua Maisha ya Mtanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti Mpya ya Serikali Kuinua Maisha ya Mtanzania?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Jun 12, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo

  Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo amemaliza kusoma bajeti ya serikali ya TSh 9.5 trilioni. Muhtasari wa bajeti hiyo na Picha kibao kwa yaliyojiri kwenye kikao hicho cha bajeti shuka mwisho wa habari hii. Kwa kiwango kikubwa bajeti iliyosomwa leo ilichambuliwa jana na Rais Jakaya Kikwete, hasa katika eneo la kupambana na msukosuko wa uchumi. Kipya alichoeleza ni jinsi ya kupata ongezeko la bajeti kutoka 7.2 trilioni za mwaka 2008/09.

  Sehemu ya bajeti

  Mheshimiwa Spika, kutokana na maelezo niliyoyatoa hapo juu, Bajeti ya mwaka 2009/10 imezingatia mikakati ya kitaifa inayolenga kuchangia katika kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania. Mchanganuo wa Bajeti kwa baadhi ya sekta ukijumuisha mishahara ya watumishi wa umma kwa mwaka 2009/10 ni kama ifuatavyo:

  (i) Elimu imetengewa shilingi bilioni 1,743.9 ikilinganishwa na shilingi bilioni 1,430.4 kwa mwaka 2008/09, sawa na ongezeko la asilimia 22. Sekta hii bado inaendelea kuchukua sehemu kubwa ya Bajeti kutokana na umuhimu wake.

  (ii) Kilimo kimetengewa kiasi cha shilingi bilioni 666.9 ikilinganishwa na shilingi bilioni 513.0 za mwaka 2008/09 pamoja na fedha za marejesho za EPA, sawa na ongezeko la asilimia 30. Aidha, serikali inadhamini mikopo ya Benki kwa sekta ya kilimo kupitia vyama vya ushirika na makampuni ya watu binafsi kwa mazao mbalimbali.

  (iii) Miundombinu imetengewa jumla ya shilingi bilioni 1,096.6 ikilinganishwa na shilingi bilioni 973.3 mwaka 2008/09, sawa na ongezeko la asilimia 12.7;

  (iv) Afya imetengewa shilingi bilioni 963.0 ikilinganishwa na shilingi bilioni 910.8 mwaka 2008/09, sawa na ongezeko la asilimia 5.7;

  (v) Maji imetengewa shilingi bilioni 347.3 ikilinganishwa na shilingi bilioni 231.6 zilizotengwa mwaka 2008/09 sawa na ongezeko la asilimia 50; na

  (vi) Nishati na madini imetengewa shilingi bilioni 285.5 ikilinganishwa na shilingi bilioni 378.8 zilizotengwa mwaka 2008/09, sawa na upungufu wa asilimia 24.6 Hali hii imesababishwa na kumalizika mikataba ya kuzalisha umeme kwa makampuni ya kukodi ya Dowans, APR na Aggreko. Hatua nyingine zinachukuliwa katika mwaka 2009/10 kutafuta mikopo kutoka mashirika ya kimataifa na nchi marafiki ili kuweza kupata rasilimali zaidi za kufanikisha miradi ya nishati nchini. Nchi na mashirika ya fedha ya kimataifa yameonesha nia ya kutusaidia zikiwemo Korea ya Kusini, Saudi Fund, BADEA, na OPEC Fund.
   
 2. S

  Sumji R I P

  #2
  Jun 12, 2009
  Joined: Jun 11, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MziziMkavu,
  asante kwa muhitasari huu wa bajeti
   
 3. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,210
  Likes Received: 312
  Trophy Points: 180
  .

  Danganya toto hii. Kama zingetumika trilioni 1.4 kwenye Elimu mwaka unaomalizika si tungeona matokeo yake! Nani anaweza kuthibitisha ELIMU ilitumia trilioni 1.4 mwaka unaokwisha?

  Tumeshaona udanganyifu katika takwimu za serikali za Elimu siku za nyuma (niliweka ushahidi hapa JF. Haki Elimu waliona dosari pia). Wanatenga kisha karibu nusu ya fedha zote zinabaki Hazina kwa matumizi ya kimya kimya.

  Hizi fedha za Elimu zitanunulia kanga za uchaguzi na kutumika kwa takrima mwaka kesho. We need an independent budget implementation and monitoring agency.
   
 4. Van Walter

  Van Walter Senior Member

  #4
  Jun 17, 2009
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 171
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  tuache kujidanganya mwakani hakuna maendeleo yoyote zaidi ya kuiba mihela yote hiyo ili ccm iwe na fedha za campaign...kwahiyo wenye akili tushajua hapo..mkullo hana jipya jamani....mkitaka mapya ni kuipa kura za hapana tu mwakani hadi ccm ipate adabu na kujua kuwa watanzania sasa tumechoka hasa na tunataka uongozi uliothabiti
   
 5. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2009
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Jamani wadau... kwani huu uhuni wa Chama Cha Mafisadi (CCM) utaisha lini????, they doctor every budget, eti VAT is now 18% instead of 20%!!! Then wafanyakazi ambao ndio walipa kodi wakubwa kwa Government wameachwa waendelee kuumia na kodi za makato ya Income tax, I thought kwamba wangewafikiria wafanyakazi... lakini duh!!
   
Loading...