Bajeti kugusa mabenki, mabenki hayawezi kuongeza riba za mikopo kufidia kodi mpya kwenye sekta hii?

Nilivyoelewa Inayokatwa ni charges ya kutumia ...mfano kama kutuma mil 1 kitumio ni 5000 hyo ndio itakatwa asilimia 10 kwa hyo serikali itagawana na voda na tigo ila sasa impact yake ni kuwa je zile charges zinazobaki zitawalipa wenye makampuni ya kutuma na kupokea pesa? Sasa hofu ndio hapo kama jamaa nao wakiongeza charges hapo ndio utakuwepo mzozo ila hv vitu vinaenda parrarel kama wenye makampuni wakiongeza charges maana yake na kiwango cha kukatwa hyo hela na serikali inaongezeka inayotokea hapo ni
 
Kenya wanaotumia bank ni zaidi ya milioni 20
sisi wanaotumia bank ni milioni 3 tu
tulipaswa kuvutia zaidi watu watumie bank kwa kupunguza kodi
badala yake tumeongeza kodi

Tatizo kubwa ni kwamba sehemu kubwa ya watanzania ni masikini wa kutupwa. Na kingine kilicho changia ni uwepo wa huduma za pesa kwa simu.
Benki za Tanzania zipo kwa ajili ya wafanyabiashara na wafanyakazi wanaopitisha mishahara yao na sio wananchi wa kawaida.
 
Mabenki yetu yanavyopenda kuwafilisi watu nyumba,hilo ongezeko watalielekeza huko huko.
 
sasa wanafunz tutaanz kutumiwa pesa z matumizi kweny barua ...nchi isharudi enzi z utumwa ila ukiwa wa kisasa zaidii.....du pole TZ kw kuing'ang'ani CCM
 
Habari wadau,

Hivi kama bajeti itapitishwa huku mabenki yakikabiliwa na kodi mpya ya matumizi ya ATM kama inavyopendekezwa, mabenki haya hayawezi kuongeza riba za mikopo kufidia tozo hiyo mpya?

Nauliza swali hili kwasababu naamini benki zikiongeza riba kwenye mikopo,basi hili litakuwa pigo kubwa sana kwa wajasiliamali wengi wa nchi hii.

Kama mabenki yataanza kutafuta chanzo cha kufidia kodi hii mpya,nashauri ni bora waongeza gharama za kutumia ATM hizo au gharama ya kumiliki/kuendesha account,gharama ya kuchukua fedha ndani ya benki(kwa teller) au gharama nyinginezo kuliko kuthubutu kuongeza riba za mikopo maana mtagusa wengi na zaidi mtaongeza umasikini wa mtu mmoja mmoja.

Sitaraji kabisa uamuzi wa aina hii kwa mabenki hata hivyo lolote laweza kutokea kutegemeana na bajeti nzima ya mwaka huu.

Hapa benki wataongeza gharama za kwenye Atm sana
 
Waongeze tu tukome.

Hii nchi bila maskini kufikia hatua ya kukamuliwa na kunyang'anywa kila kitu hakutakua na mapinduzi ya kweli ya kifikra.

Ili CCM iondoke madarakani ni lazima maskini tupitie mateso kupita kiasi ili tu'evolve na kufanya maamuzi sahihi kwa kuchagua watu sahihi.
Ubarikiwe sana mkuu .
 
naweza nisijue mkurabita ni what kind of a donkey but ulichosema si kweli!
Kwa mujibu wa ripoti nilyowahi kuisoma miaka michache iliyopita (2013) ilikuwa ni asilimia 17 ya watu wazima (adult population) nchini Tanzania ndio walikuwa wanapata access ya akaunti za benki (idadi hiyo ilikuwa ni watu milioni 3.7) huenda hizo statistics haziko mbali sana, kuna baadhi ya mambo tupo nyuma sana, ila tumepiga hatua kwenye hizi mobile money, machapisho ya ripoti nyingi hututumia kama mfano mzuri.
 

Attachments

  • 6414nsa05.pdf
    258.4 KB · Views: 41
Kwa mujibu wa ripoti nilyowahi kuisoma miaka michache iliyopita (2013) ilikuwa ni asilimia 17 ya watu wazima (adult population) nchini Tanzania ndio walikuwa wanapata access ya akaunti za benki (idadi hiyo ilikuwa ni watu milioni 3.7) huenda hizo statistics haziko mbali sana, kuna baadhi ya mambo tupo nyuma sana, ila tumepiga hatua kwenye hizi mobile money, machapisho ya ripoti nyingi hututumia kama mfano mzuri.
Mkuu unabishana na kilaza,uyo ajui chochote zaidi ya kupinga.
 
Ongezeke lolote la kodi anayeumia ni final consumer. Wengine wana transfer hiyo tax cost na kuwa mawakala wa kukusanya kodi.
Kwa upande wa benki ni lazima waongeze gharama maana ile income waliyokuwa wanaipata itabidi ipungue,sasa ili wabaki ktk projection zao wanaongeze gharama.
Madhara mengine naona kutakuwa na slightly financial panic itayosababisha wateja kutoa fedha zao benki,wengine hasa kwa hofu ya hizo kodi ambazo uelewa wake kwa wengi ni mdogo.
 
Mkuu unabishana na ******,uyo ajui chochote zaidi ya kupinga.

#gasper do santos hujamuelewa #Cannabis kasema nini, sembuse kuelewa nilichosema! acha story za kwenye kahawa!
Unakuwa kama yule mtangazaji aliyesema yanga ina fans zaidi ya million 35 Au tigo has more than 31 millions of subscribers! This is 2016, 3yrs kwenye uchumi ni kubwa sana! we now have around 11 million of accounts holders! Mambo yaliyofanyika baada ya hizo reports kuanzia regulations mpaka idadi ya watu ni kubwa.
 
Back
Top Bottom