Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,683
- 149,887
Habari wadau,
Hivi kama bajeti itapitishwa huku mabenki yakikabiliwa na kodi mpya ya matumizi ya ATM kama inavyopendekezwa, mabenki haya hayawezi kuongeza riba za mikopo kufidia tozo hiyo mpya?
Nauliza swali hili kwasababu naamini benki zikiongeza riba kwenye mikopo,basi hili litakuwa pigo kubwa sana kwa wajasiliamali wengi wa nchi hii.
Kama mabenki yataanza kutafuta chanzo cha kufidia kodi hii mpya,nashauri ni bora waongeza gharama za kutumia ATM hizo au gharama ya kumiliki/kuendesha account,gharama ya kuchukua fedha ndani ya benki(kwa teller) au gharama nyinginezo kuliko kuthubutu kuongeza riba za mikopo maana mtagusa wengi na zaidi mtaongeza umasikini wa mtu mmoja mmoja.
Sitaraji kabisa uamuzi wa aina hii kwa mabenki hata hivyo lolote laweza kutokea kutegemeana na bajeti nzima ya mwaka huu.