Bajeti ijayo ni trilioni 15; nini maoni yako? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ijayo ni trilioni 15; nini maoni yako?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bado Kidogo 2015, Jun 5, 2012.

 1. Bado Kidogo 2015

  Bado Kidogo 2015 JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi kwa pamoja, heshima zenu.

  Nimeshwawishika kuandika uzi huu baada ya magazeti mengi ya leo kuandika bajeti ijayo ya 2012/2013 itakuwa 15trl na hapa nalinukuu gazeti la Mwananchi "BAJETI ya Serikali ya mwaka 2012/2013 inatarajiwa kutumia Sh15 trilioni katika vipaumbele saba ikilinganishwa na Sh13.5 trilioni zilizotengwa mwaka 2011/212"

  Suala la msingi katika uzi wangu ni hili. Hivi hii bajeti ni ya kuongeza figure tu au ina lengo la kumkomboa mwananchi wa chini? Mwaka jana wa fedha bajeti ya 13trl ni bajeti ilikuwa inaonekana kama mkombozi lakini katika bajeti hewa nadhani ile ilikuwa inaongoza.

  Mpaka hivi sasa taasisi nyingi za serikali zipo hoi yaani zinashindwa hata kujiendesha kwa vitu vidogo vidogo, almost kila kitu kinakwenda kwa mkopo!!!!

  Ukiacha hilo, miradi ya maendeleo ndiyo safari hii haikuguswa kabisa. Mingi ni kama imetelekezwa kutokana na uhaba wa fedha toka serikalini. Ikumbukwe bajeti hiyo haikutengenewa fedha ya mradi wa miaka 15 ambao ulizua balaa bungeni kwa nini uzinduliwe mwaka huu (2011/2012) lakini fedha yake isitengwe katika bajeti hiyo hali iliyoilazimu serikali kutoa majibu ya ziada.

  Kutokana na baadhi ya ushahidi huo nashawishika kusema bajeti ijayo ya 15trl isn just a figure but nothing.

  Nakaribisha maoni yenu wakuu.
   
 2. Kakulwa P

  Kakulwa P JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapo hakuna bajeti ni madudu tu ambayo ni kila mwaka yanapitishwa kwa mbwembwe tunaambiwa ni bajeti ya wananchi.

  Maana yangu ni kuwa Matumizi ni 10trllioni na fedha za maendeleo 5trilion hivyo bajeti ya ulaji tuuuuuuu maendeleo kiduchu. Inawezekana uelewa wangu ni mdogo lakini maendeleo ni mazuri kuliko chumia tumbo.

  Nashukuru mleta mada jamvini wadau watatoa maoni yao. Nasikia wizara ya uchukuzi bajeti ya mwaka unaoisha wameweza kuifanyia kazi 40% tu 60%hakuna utekelezaji wowote pesa kwishneii!!!!!!
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,808
  Trophy Points: 280
  How do we raise that amount of money? Mbona bajeti hii tumeshindwa kwa kiasi kikubwa kutoa hela la shughuli za maendeleo kama tulivyopanga kwenye bajeti? Tukiwa serious kukusanya kodi na kupunguza misahama na rushwa au kukwepa ulipaji kodi, labda we can achieve.
   
 4. Bado Kidogo 2015

  Bado Kidogo 2015 JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kakulwa P,

  Nilichokiona katika utekelezaji wa bajeti ya 2011/2012 ndicho kinachonifanya niamini kuwa hata hii ya 2012/2013 bado itakuwa usanii.

  Naanza kuwapa pole hasa wafanyakazi wa serikali ambao wanategemea miijuza katika bajeti pamoja na wananchi wote kwa ujumla.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hivi hazina walisema kuna sh ngapi vile kwa mda ganip? Sasa hizo trillion 15 wamezitoa wapi? Hilo changa la macho kuhadaa umma
   
 6. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mzee Jangala at work.
   
 7. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tukishindwa kabisa kupata kodi ya kutosha kuendesha serikali tutaenda kwa mjomba Obama tumpatie eneo la kulima atupe pesa ya kuendesha nchi tetehteet
   
 8. Bado Kidogo 2015

  Bado Kidogo 2015 JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama sijakosea bajeti ya 2011/2012 matumizi ya kawaida (recurrent expenditure) ilikuwa ni 9trl na balance ni maendeleo wakati mapato yetu tulikuwa tunategemea kupata almost 6trl (3trl deficit from recurrent exp.).

  Kiutendaji mara nyingi ukisema unatarajia kukusanya 6trl unaweza usifike, kukawa na deviation kidogo. Sasa bajeti ile tu imetushinda na kiashiria kibaya sana ni ukuaji wa deni la taifa ambalo saizi linakadiriwa kuzidi 35% ya GDP yetu!!!!!

  Hii inamananisha kuwa matapo ya ndani ni madogo hivyo kulazimika kukopa nje ili kuweza kuendesha shughuli za kawaida. Hii ni hatari sana.
   
 9. Olaigwanani lang

  Olaigwanani lang JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 480
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  asilimia kubwa huishia kwenye chai na posho tuu......
  wabunge wa magamba badala ya kuelekeza iweje watabaki kukandia mikutano ya M4C...
   
 10. Bado Kidogo 2015

  Bado Kidogo 2015 JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kashaijabutege tema hoja hizo ni typing errors.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Bajeti ya Tanzania ni ndogo sana; trilioni 15 ni sawa na dola bilioni kama 13 hivi ambazo kwa kweli hazitoshi kabisa. Yaani bajeti yetu haifikii bajeti ya Jiji la NY! Binafsi naamini tunahitaji bajeti isiyopungua bilioni 50 dola kwa mwaka na tutakuwa tunaweza kuona matokeo katika mabadiliko ya quality of life kwa watu wengi zaidi tutakapoanza kufikia bajeti ya bilioni 100 dola! Hii ya bilioni 13 ni bajeti ya wavivu wa kufikiri, wazembe wa kupanga na goigoi wa kutenda. Hatupendi kufikiri juu ya uwezo wetu!
   
 12. Bado Kidogo 2015

  Bado Kidogo 2015 JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa mtaji huu waandae vikao vingi sana kutetea bajeti kupita maana naona wazi bungeni nwiki ijayo hapatatosha kabisa. Kila mbunge ameshituka kuwa 2015 siyo salama kama hatatetea wananchi ambao ndiyo waliomtuma.
   
 13. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,808
  Trophy Points: 280
  Pamoja na udogo huo wa bajeti na kuota kupata dola billion moja kwa mwezi ili kupunguza umaskini, bado hatuwezi kukusanya wenyewe kodi ya kuendesha bajeti hiyo. Mwaka huu ndio imekuwa worse...maana shughuli chache sana za maendeleo zimefanyika
   
 14. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,110
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Mimi naamini kwa uongozi huu wa Jk tutapiga sana gitaa lakini hawatasikia, kama ni lazimz wamalize kipindi chao cha uongozi tusubiri 2015 tupigie kura viongozi waadilifu wenye uwezo wa kufanya kazi na hata kutuletea maendeleo. Hawa wanatimiza ndoto zao za kuingia ikulu....hawakuwa na agenda yoyote ya maendeleo na Mungu awarehemu.
   
 15. t

  thinka JF-Expert Member

  #15
  Jun 5, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hata budget ikiwa trl 50 lakin kama inflation ni 40% haina maana.
   
 16. Bado Kidogo 2015

  Bado Kidogo 2015 JF-Expert Member

  #16
  Jun 5, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  MMJ hii ni aibu, yaani wewe umekwenda mbali sana hii ya 13trl imetushinda kabisa katika utekelezaji sembuse hii ya 15trl. Ni mpaka tutakapoanza na kuamua kujikwamwua katika lindi hili la umaskini wa mali na kufikiri ndipo tutakapakaribia angalau kuwa na dhamira ya kweli ya kuondoa umaskini.

  Viongozi wetu wameamua kuridhika kwa kuwa wao wanamali na uhakika wa familia zao kwenda shule nzuri na kuishi basi wanaona inatosha na kuacha kufikiri kwa ajili ya wengine, hali hii ni mbaya sana na ndiyo chanzo cha wengi kukimbilia kutaka kuwa viongozi kwa malengo ya kujinufaisha.
   
 17. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #17
  Jun 5, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Hio figure itakuwa imeongezeka kwa sababu ya mikoa mipya tu mishahara ya kishikaji...last year mfano wizara ya ujenzi budget yake ilikuwa 1.4 tr lakini uhalisia walipaa billioni 400 wakati huo wanadaiwa billion 380 na wakandarasi wa bara bara kwa hio hamna kitu ...ndio maana barabara nyingi zimesimama labda zile tu zinazofadhiliwa ..barabara inajengwa kwa hisani ya watu wa jp
   
 18. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #18
  Jun 5, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Hii ndio Magamba bana watu walio fuzu chuo cha mbwembwe na usanii,
  Hiyo ni bajet iliyolenga kupumbaza watu,
  yaani ni usanii mtupu.
   
 19. G

  GOMA Member

  #19
  Jun 5, 2012
  Joined: Dec 5, 2007
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  I have a few questions in my mind; 1. How will this budget be raised( normal pratices and same style, the government has no other creativity to generate income other than taxes- and if so, that means the government will aim on raising the taxe rates and hence much burden to citizens. Nonsense!) 2. How are the budget priorities come in place( I really really don't know). 3. I would expect prior to a new budget to be informed on the balance of 2011/2012 budget( whether negative or positive)
  :confused2:
  I understand, the country has so much potentials to raise that sum other than from poor citizens( taxe payers), a bit sense of accountability, creativity, awarness, and uzalendo:angry:! I pray the current move by people's power take effect:clap2:
   
 20. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #20
  Jun 5, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mbivu na mbichi zitajulikana pale bungeni, wiki chache zijazo
   
Loading...