Alex Katto
Senior Member
- Mar 3, 2013
- 155
- 20
Natumaini wote mu wazima wa afya
Siku mbili hizi zilizopita baadhi ya wawakilishi wa sirikali wametoa tangazo la kupiga marufuku bodaboda na bajaji kufika mjini, sasa mi ninachojiuliza ni kwamba, nini sababu kuu ya kuzuia, na pia je wanajua kuwa vijana wengi ndio wamejiari kupitia vyombo hivyo?
Sasa hawaoni kuwa watasababisha ongezeko la ukosefu wa ajira na matokeo yake tutaanza kukabwa na kuibiwa visimu vyetu, pia biashara hii ilikuwa inachangia sana pato la nnchi, je hawaoni kuwa pato la nnchi litashuka pia kwa namna fulani?
Hebu tutafakari juu ya hili na kama kuna mtu anajua zaidi juu ya hili naomba atufafanulie zaidi tujue.
=============
=============
March 14, 2014:
Waandamana Ofisi za CHADEMA:
Siku mbili hizi zilizopita baadhi ya wawakilishi wa sirikali wametoa tangazo la kupiga marufuku bodaboda na bajaji kufika mjini, sasa mi ninachojiuliza ni kwamba, nini sababu kuu ya kuzuia, na pia je wanajua kuwa vijana wengi ndio wamejiari kupitia vyombo hivyo?
Sasa hawaoni kuwa watasababisha ongezeko la ukosefu wa ajira na matokeo yake tutaanza kukabwa na kuibiwa visimu vyetu, pia biashara hii ilikuwa inachangia sana pato la nnchi, je hawaoni kuwa pato la nnchi litashuka pia kwa namna fulani?
Hebu tutafakari juu ya hili na kama kuna mtu anajua zaidi juu ya hili naomba atufafanulie zaidi tujue.
=============
BODABODA,BAJAJI NA GUTA ZAPIGWA MARUFUKU JIJINI DAR ES SALAAM.
Wakihojiwa na TBC 1,Kamanda wa polisi bwana Sulemani Kova,Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam bwana Saidi Mecki Sadiki ,pamoja na Afisa Mfawidhi kanda ya mashariki,Conrad Shio wa Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi kavu (SUMATRA) wameweza kuelezea jinsi mchakato huu utakavyokuwa jijini Dar es Salaam.
Wote waliweza kutoa sababu mbalimbali ya kwanini wameamua kushirikiana katika kuhakikisha vyombo hivi vya usafiri haviingii sehemu za mijini.
Vyombo hivi vya usafiri yaani bajaji,bodaboda na maguta ( baiskeli zenye matairi matatu) vitakatazwa kuingia sehemu zote za CBD (mijini).
Wakitolea mifano wa sehemu hizo ni,ukitokea Bunju hadi kuja Tegeta,mwisho wa vyombo hivyo utakuwa ni Mwenge
Pia ukitokea Mbezi ya Msuguli mwisho itakuwa Kimara kwahiyo ukija Ubungo utazuiliwa.
Kwahiyo maeneo yoote ya mijini Posta ikiwemo,vyombo hivi havitaruhusiwa kuingia
SABABU ZA KUZUIWA KUINGIA.
Viongozi hawa watatu waliweza kutoa sababu mbalimbali za kwanini vyombo hivi vimekatazwa kuingia sehemu za mijini.
Sababu hizo ni kama zifuatazo
2. Kuzuia matukio ya ualifu yanayofanyika kwakutumia sana bodaboda.Yaani bodaboda zinatumika sana kwenye matukio ya uhalifu kama wizi na ujambazi.
3. Kuzuia msongamano wa vyombo vya usafiri jijini.
4. Kupunguza ajali zinazosababishwa haswahaswa na vyombo hivi mfano bodaboda.kamanda Kova alitolea mfano kuwa unakuta kijana wa bodaboda yupo mataa lakini hata kama taa hazijamruhusu yeye anapita na kuacha magari kubakia kwenye mataa. Hapa aliuliza kwani waliosimama sio watu???? Kwahiyo alisema vyombo hivi madereva wake wengi hawafati sheria za barabarani
HITIMISHO.
Walisisitiza kuwa vyombo hivyo vimeruhusiwa kwa shughuli za biashara pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam.
Pia kwa wale watu wanaotumia kama usafiri wao binafsi yaani sio kibiashara wanaruhusiwa kuingia navyo mijini hususani pikipiki kwa sharti la kuwa pekee yaani bila kumpakiza mtu nyuma.
Kamanda Kova aliongeza na kusema,kama mtu akitoka pembezoni mwa mji mfano Bunju au Tegeta basi akifika Mwenge ambapo ndio mwisho wa bodaboda za biashara, atatakiwa achukue usafiri wa umma na kuendelea na safari zake.
Kamanda Kova alisema kama sheria inatakiwa itende haki kotekote maana kuna watu wanaweza kudanganya kuwa pikipiki anayoiendesha siyo ya biashara kwahiyo mtu aliyembeba ni rafiki au mpenzi wake na ikachukuliwa kawaida lakini itaonekanaje kwa wale wafanya biashara wanaopakiza nao watu kama hawa??? Kwahiyo sharti ni uwe mwenyewe kwenye pikipiki yako.
Naye Afisa Mfawidhi wa SUMATRA Kanda ya Mashariki Bw. Conrad Shio ameeleza kuwa sheria ya usafirishaji kusimamia Bajaji na Bodaboda iko wazi na kuongeza kuwa serikali ina wajibu wake na pia waendesha pikipiki na Bajaji wanawajibu wao wa kuzingatia kanuni taratibu na kanuni zilizowekwa.
Sisi kama SUMATRA tunaendelea kufanya kila tuwezalo kukabiliana na vitendo vyote vya uvunjivu wa sheria za barabarani
Afisa Mfawidhi wa SUMATRA Kanda ya Mashariki Bw. Conrad Shio akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu sheria inayosimamia usafiri wa Bajaji na Bodaboda nchini.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna (CP) Suleiman Kova akitoa ufafanuzi ameeleza kwa waandishi wa habari kuhusu wakazi wa jiji la Dar es salaam hususan madereva wa bodaboda na Bajaji kufuata sheria za barabarani na kajenga tabia ya kufanya tathmini ya safari zao iwapo wanakidhi vigezo vya usalama barabarani ili kuepusha madhara.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kutoa agizo kwa viongozi na watendaji wa jiji la Dar es salaam kuhakikisha kuwa wanawaondoa na kuwachukulia hatua za kisheria wanaovunja sheria za jiji kwa kuendesha shughuli mbalimbali katika maeneo yasiyoruhusiwa.
=============
March 14, 2014:
Waandamana Ofisi za CHADEMA:
Jengo la makao makuu ya CHADEMA yaliyopo mtaa wa ufipa Kinondoni yameviwa ma vijana waendesha boda boda wa jijini Dar muda huu wakitaka waonane na viongozi wa chama hicho kuwaeleza kero na manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa maofisa wa jiji pamoja na askari polisi katika utekelezaji wa mujukumu yao ya kujipatia riziki.
Kutokana na hali hiyo tayari polisi wameshazingira eneo zima la makao makuu ya CHADEMA kwa ajili ya tahadhari ya jambo lolote.