Bajaj, bodaboda marufuku kuingia katikati ya jiji la Dar es Salaam! Waandamana ofisi za CHADEMA

Alex Katto

Senior Member
Mar 3, 2013
155
20
Natumaini wote mu wazima wa afya

Siku mbili hizi zilizopita baadhi ya wawakilishi wa sirikali wametoa tangazo la kupiga marufuku bodaboda na bajaji kufika mjini, sasa mi ninachojiuliza ni kwamba, nini sababu kuu ya kuzuia, na pia je wanajua kuwa vijana wengi ndio wamejiari kupitia vyombo hivyo?

Sasa hawaoni kuwa watasababisha ongezeko la ukosefu wa ajira na matokeo yake tutaanza kukabwa na kuibiwa visimu vyetu, pia biashara hii ilikuwa inachangia sana pato la nnchi, je hawaoni kuwa pato la nnchi litashuka pia kwa namna fulani?

Hebu tutafakari juu ya hili na kama kuna mtu anajua zaidi juu ya hili naomba atufafanulie zaidi tujue.

=============
BODABODA,BAJAJI NA GUTA ZAPIGWA MARUFUKU JIJINI DAR ES SALAAM.

Wakihojiwa na TBC 1,Kamanda wa polisi bwana Sulemani Kova,Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam bwana Saidi Mecki Sadiki ,pamoja na Afisa Mfawidhi kanda ya mashariki,Conrad Shio wa Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi kavu (SUMATRA) wameweza kuelezea jinsi mchakato huu utakavyokuwa jijini Dar es Salaam.

Wote waliweza kutoa sababu mbalimbali ya kwanini wameamua kushirikiana katika kuhakikisha vyombo hivi vya usafiri haviingii sehemu za mijini.

Vyombo hivi vya usafiri yaani bajaji,bodaboda na maguta ( baiskeli zenye matairi matatu) vitakatazwa kuingia sehemu zote za CBD (mijini).

Wakitolea mifano wa sehemu hizo ni,ukitokea Bunju hadi kuja Tegeta,mwisho wa vyombo hivyo utakuwa ni Mwenge

Pia ukitokea Mbezi ya Msuguli mwisho itakuwa Kimara kwahiyo ukija Ubungo utazuiliwa.
Kwahiyo maeneo yoote ya mijini Posta ikiwemo,vyombo hivi havitaruhusiwa kuingia

SABABU ZA KUZUIWA KUINGIA.

Viongozi hawa watatu waliweza kutoa sababu mbalimbali za kwanini vyombo hivi vimekatazwa kuingia sehemu za mijini.
Sababu hizo ni kama zifuatazo

2. Kuzuia matukio ya ualifu yanayofanyika kwakutumia sana bodaboda.Yaani bodaboda zinatumika sana kwenye matukio ya uhalifu kama wizi na ujambazi.

3. Kuzuia msongamano wa vyombo vya usafiri jijini.

4. Kupunguza ajali zinazosababishwa haswahaswa na vyombo hivi mfano bodaboda.kamanda Kova alitolea mfano kuwa unakuta kijana wa bodaboda yupo mataa lakini hata kama taa hazijamruhusu yeye anapita na kuacha magari kubakia kwenye mataa. Hapa aliuliza kwani waliosimama sio watu???? Kwahiyo alisema vyombo hivi madereva wake wengi hawafati sheria za barabarani

HITIMISHO.
Walisisitiza kuwa vyombo hivyo vimeruhusiwa kwa shughuli za biashara pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam.
Pia kwa wale watu wanaotumia kama usafiri wao binafsi yaani sio kibiashara wanaruhusiwa kuingia navyo mijini hususani pikipiki kwa sharti la kuwa pekee yaani bila kumpakiza mtu nyuma.

Kamanda Kova aliongeza na kusema,kama mtu akitoka pembezoni mwa mji mfano Bunju au Tegeta basi akifika Mwenge ambapo ndio mwisho wa bodaboda za biashara, atatakiwa achukue usafiri wa umma na kuendelea na safari zake.

Kamanda Kova alisema kama sheria inatakiwa itende haki kotekote maana kuna watu wanaweza kudanganya kuwa pikipiki anayoiendesha siyo ya biashara kwahiyo mtu aliyembeba ni rafiki au mpenzi wake na ikachukuliwa kawaida lakini itaonekanaje kwa wale wafanya biashara wanaopakiza nao watu kama hawa??? Kwahiyo sharti ni uwe mwenyewe kwenye pikipiki yako.

Naye Afisa Mfawidhi wa SUMATRA Kanda ya Mashariki Bw. Conrad Shio ameeleza kuwa sheria ya usafirishaji kusimamia Bajaji na Bodaboda iko wazi na kuongeza kuwa serikali ina wajibu wake na pia waendesha pikipiki na Bajaji wanawajibu wao wa kuzingatia kanuni taratibu na kanuni zilizowekwa.

“Sisi kama SUMATRA tunaendelea kufanya kila tuwezalo kukabiliana na vitendo vyote vya uvunjivu wa sheria za barabarani”

Picha+na+3.JPG


Afisa Mfawidhi wa SUMATRA Kanda ya Mashariki Bw. Conrad Shio akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu sheria inayosimamia usafiri wa Bajaji na Bodaboda nchini.

Picha+na+2.JPG


Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna (CP) Suleiman Kova akitoa ufafanuzi ameeleza kwa waandishi wa habari kuhusu wakazi wa jiji la Dar es salaam hususan madereva wa bodaboda na Bajaji kufuata sheria za barabarani na kajenga tabia ya kufanya tathmini ya safari zao iwapo wanakidhi vigezo vya usalama barabarani ili kuepusha madhara.

Picha+na+1.JPG


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kutoa agizo kwa viongozi na watendaji wa jiji la Dar es salaam kuhakikisha kuwa wanawaondoa na kuwachukulia hatua za kisheria wanaovunja sheria za jiji kwa kuendesha shughuli mbalimbali katika maeneo yasiyoruhusiwa.

=============
March 14, 2014:

Waandamana Ofisi za CHADEMA:

Jengo la makao makuu ya CHADEMA yaliyopo mtaa wa ufipa Kinondoni yameviwa ma vijana waendesha boda boda wa jijini Dar muda huu wakitaka waonane na viongozi wa chama hicho kuwaeleza kero na manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa maofisa wa jiji pamoja na askari polisi katika utekelezaji wa mujukumu yao ya kujipatia riziki.

Kutokana na hali hiyo tayari polisi wameshazingira eneo zima la makao makuu ya CHADEMA kwa ajili ya tahadhari ya jambo lolote.

attachment.php


attachment.php


B3.jpg

B1.jpg


B2.jpg
 
Hizo bodaboda ni kero na kwa ufinyu wa barabara za katikati ya mji uwepo wa bodaboda huleta usumbufu zaidi.

Kuziruhusu ziwe zinafika katikati ya mji ni sawa na kufuga bata sebuleni.
 
natumaini wote mu wazima wa afya ,
siku mbii hizi zilizopita baadhi ya wawakilishi wa sirikali wametoa tangazo la kupiga marufuku bodaboda na bajaji kufika mjini, sasa mi ninachojiuliza ni kwamba, nini sababu kuu ya kuzuia, na pia je wanajua kuwa vijana wengi ndio wamejiari kupitia vyombo hivyo? sasa hawaoni kuwa watasababisha ongezeko la ukosefu wa ajira na matokeo yake tutaanza kukabwa na kuibiwa visimu vyetu, pia biashara hii ilikuwa inachangia sana pato la nnchi, je hawaoni kuwa pato la nnchi litashuka pia kwa namna fulani? hebu tutafakali juu ya hili na kama kuna mtu anajua zaidi juu ya hili naomba atufafanulie zaidi tujue.
hakuna hata mji mmoja duniani unaokataza matumizi ya pikipiki kufika katikati ya jiji,na hakuna hata sababu yenye nguvu ya kuzuia pikipiki zisifike mjini,ukweli ni huu:mkurugenzi wa sumatra,mkuu wa wilaya ya ilala ,mkurugenzi wa jij(hawa wote wachaga)wote chadema,kinachofanyika ni kuwatia bodaboda dhiki na shida ili vijana waichukie serikali ili msemo wao kwamba hawajariwi na serikali hii iwe kwa vitendo,walijaribu jiji mwaka jana kuingia mkataba na kampuni ya 'mwafrika'kwa ajiri ya kukamata pikipiki lakini nape alisimama kidete lilikufa. na hili ndo maana ipo dar peke yake kwa vile dar ndo tanzania yenyewe ukipata support dar kwingine kwepesi,kwa hiyo hao wanatumia vyeo vyao kufanikisha malengo yao kisiasa,.
Source;mimi mwenyewe mdau wa pikipiki.
 
BODABODA,BAJAJI NA GUTA ZAPIGWA MARUFUKU JIJINI DAR ES SALAAM.

Wakihojiwa na TBC 1,Kamanda wa polisi bwana Sulemani Kova,Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam bwana Saidi Mecki Sadiki ,pamoja na Afisa Mfawidhi kanda ya mashariki,Conrad Shio wa Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi kavu (SUMATRA) wameweza kuelezea jinsi mchakato huu utakavyokuwa jijini Dar es Salaam.

..... Read 1st post!
 
Kwa kipindi kirefu sasa Tanzania na Mtaifa mengine yamekuwa yakilia suala la ukosefu wa ajira kwa vijana. lakini sisi tumefanikiwa kupata njia rahisi ya kupunguza tatizo hilo hasa kwa kada za vijana wasio na ujuzi maalumu. inasemekana zaidi ya ajira 600 zinaongezeka kila siku kutokana na boda boda na waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowasa amekiri hilo.

tukiangalia historia kwa ufupi inaonyesha mlolongo mzuri wa vyombo vya serikali likiwemo bunge kutambua na kuthamini ajira ya madereva boda boda. waziri wa fedha wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya 2013/14, alitangaza kuondoa kodi kwa boda boda lengo lake ikiwa ni kuchochea ajira hiyo. jeshi la polisi ambalo kwa sasa ndo linaendesha shughuli za utekaji wa boda boda pale jangwani, limekuwa na program mbali mbali za kuwapa mafunzo madereva wa boda boda juu ya taratibu na kanuni za barabarani. Mfano mwingine halisi unotuonyesha kutambuliwa kwa ajira hiyo ni ufunguzi wa kituo cha boda boda mkoni Mwanza.

swali langu hapa ni kwanini na ni wapi Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amepata mamlaka ya kutangaza kihama kwa boda boda? kuwazuia boda boda wasije mjini ni sawa na kuvunja amani. kwa sababu tunajua kuwa wapo vijana wengi ambao kimsingi wanendesha maisha yao ya kila siku(zikiwemo familia zao) kwa kipato cha boda boda. lakini pia wapo vijana mabao walikuwa vijiweni wakivuta bangi na pengine wakifanya shughuli ya ukabaji saa za jioni sasa watu hawa ni madereva wa boda boda na sio vibaka tena kama ilivyokuwa hapo awali. sasa ni sababu hipi ya kumfanya boss huyu awafungie kuingia posta na maeneo mengine ya mjini?

tukiafanya uchambuzi wa kina ni dhahiri kuwa bado hatujawa na tatizo la boda boda kiasi cha kuwazuia wasije mjini, tatizo tulilokuwa nalo kubwa ni kwamba madereva wengi wa boda boda hawajui sheria za bara bara na wengine hawana lesseni za kuendesha vyombo vya moto. tatizo hili linashughulikiwa na polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kutoa mafunzo na kuwarekebisha kwa faini ndogo ndongo inapotokea wankwenda kinyume. sasa ni sababu hipi itaturidhisha na maamuzi yaliyotolewa?

UNYANYASAJI

watu hawa mbali na kuzuiwa kuja mjini bado jeshi la polisi linafanya vitu vinavyofanana na vile vilivyofanywa na kampeini ya kuondoa wahamiajai haramu. sote tunatumia bara bara na kosa la barabarani adhabu yake tunajua ni ya usalama barabarani. yaani traffic case na sio ya kumuweka mtu kizuizini (detention). sasa kinachoendelea sasa ni detention within the same state (mateka ndani ya dola moja), sheria zetu nadhani zinazuia kumuweka mtu mateka na ni uvunjifu wa haki za binadamu kumuweka mtu mateka.

kuanzia jana na leo polisi kwa kutii amri ya mkubwa wanaendesha shughuli ya kuwaweka watu (madereva boda boda) mateka katika eneo la jangwani nyuma ya majengo ya wachina na klabu ya Yanga. suala hili ni la unyanyasaji kwani kuwazuia kuja mjini sio uhalali wa kuwakusanya na kuwaruda eneo fulani kama inavyokuwa kwa waamiaji haramu wanosubiri kurudishwa kwao. tujiulize swali kwani ukimkamata mtu aliyefanya kosa la barabarani unampeleka mateka au unampeleka polisi kwa ajiri ya charge za traffic?

lakini mbali na kuwanyanyasa madereva wa boda boda, wapo watu ambao kimsingi hawana hatia lakini wananyanyasika, watu hawa ni pamoja na familia za madereva boda boda ambao kimsingi wanasubiri baba au kaka alete chakula pale nyumbani ili wale. watu hawa wanawadogo zao wanasoma kwa sababu ya boda boda hizo. je ni kwanini tunavuruga amani ya nchi kwakufanya maamuzi yetu wenyewe bila kujali taratibu?

namshauri mkuu wa mkoa aondoe tangazo lake hilo, na awaruhusu waendelee na shughuli zao kama kawaida, ila aendeshe kampaini maalumu ya kuwasajili boda boda hao katika vyama vyao, na pia apendekeze itungwe sheria ndogo ndogo kupitia madiwani na mabaraza ya kutunga sheria ndani ya mkoa, kutunga sheria inayosimamia usafiri huo. ikiwa ni pamoja ya kuangalia usajili wao, lesseni zao, usalama wao mfano kutovaa element, mikataba yao ya kazi kwa walioajiriwa na maboss mabali mbali, utaratibu wa kulipa kodi, n.k

Lakini pia Jeshi la Polisi Usalama Barabarani liweke mazingira maalumu ya kuendeleza uelimishaji wa masuala ya usalama barabarani kwa madereva hawa na watumiaji wa usafiri wa boda boda lakini sio kurupuka na kutumia mabavu ili kuwatishia, hapana.

Wanyonge nao ni Watu.
 
Safi sana ili kupunguza msongamano ingawa walikuwa wanasaidia uharaka mjini
 
Jengo la makao makuu ya CHADEMA yaliyopo mtaa wa ufipa Kinondoni yameviwa ma vijana waendesha boda boda wa jijini Dar muda huu wakitaka waonane na viongozi wa chama hicho kuwaeleza kero na manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa maofisa wa jiji pamoja na askari polisi katika utekelezaji wa mujukumu yao ya kujipatia riziki.

Kutokana na hali hiyo tayari polisi wameshazingira eneo zima la makao makuu ya CHADEMA kwa ajili ya tahadhari ya jambo lolote.

attachment.php


attachment.php


B3.jpg

B1.jpg


B2.jpg
 
Hao wanjua haki zao na wakombozi wao wako wapi ingawa ungeweka picha inge-sound zaidi!
 
Aisee kwahiyo hata wale wa Tegeta,Kinyerezi,Chanika,Vikindu,kiluvya wamefika Makao makuu Ya CDM kudai haki ? Mungu awalinde na vitu vizito visije vikawadondokea kwani nasikia polisi huko sasa hivi wanajipendekeza ili wapate rewards kama mwenzao.
 
  • Thanks
Reactions: Dr.
Back
Top Bottom