Bahati mbaya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bahati mbaya?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by STREET SMART, May 31, 2010.

 1. STREET SMART

  STREET SMART JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2010
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 666
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60
  Katika jamii yetu kumeenea hili jambo la bahati njema(GOOD LUCK) na bahati mbaya(BAD LUCK).Tumefika kipindi jamii inawaona watu wenye mafanikio(kazini/bizness) kuwa ni result ya good luck. Na maskini au wenye mafanikio kiasi ni result ya bad luck. Hebu wakuu tuyajadili haya:
  1. Kuna huu msemo/tabia ya kuamini kuwa One day yes(ipo siku ntafanikiwa tu)...je ipo kweli iyo one day.
  2.Je bahati nzuri/mbaya ipo? na mtu anaweza kufanyaje ku attract either of them
  3.Je kuna watu wamezaliwa na bahati njema(wana zali) na wengine wamezaliwa na bahati mbaya(wana gundu).
  4.Je imani/hali ya watu kushindwa jambo na kusema 'mungu hakupenda' ni sahihi? au ni kuficha weakness zetu?
  5. Msemo wa "LUCKY IS WHEN PREPARATION MEETS OPPORTUNITY" ni sahihi?
   
 2. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hakuna aliezaliwa na bahati mbaya ni kuendekeza umaskini tu!
   
 3. D

  Deck Joel Member

  #3
  May 31, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kwa kweli hakuna kitu kinachoitwa bahati mbaya, ila watu wamejenga mazoea tu,
  we fikiria mtu anazaa watoto bila mpangilio huku kipato chake ni kidogo kiasi cha kwamba
  hawezi kumudu gharama za kuwatunza na kuwasomesha, wengi wameendelea kufuata dhana
  potofu kwamba kila mtoto anakuja na bahati yake.
  Mimi naamini kitu ambacho mtu anakuja nacho tu, ni kipaji, na ili hicho kipaji kiweze kufanikiwa
  ni lazima kuwe na mazingira mazuri yaliyoandaliwa ili kukiendeleza, lakini wanaishia kusema tu
  "aliyekupa wewe ndiye kaninyima mimi",hii mara nyingi huwa ni misemo ya watu wasiojitambua.
   
 4. M

  Malila JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Neno bahati mbaya hutumika mara( si zote) ili kuficha udhaifu wetu,kwa matukio yaliyo nje ya uwezo wetu neno hili hutumika kufariji basi. Matumizi sahihi ya nafasi uliyo nayo( chance,time,location,kipaji etc) kwa wakati mwafaka ni miongoni mwa vitu vinavyochangia kitu kinachoitwa bahati na kinyume chake ndio huitwa bahati mbaya. Wapo waliozaliwa ktk mazingira mazuri yaliyoruhusu matumizi sahihi ya nafasi ile kwa wakati ule. Kumbuka jambo jema/baya la leo unalofanya ndio utakaloingia nalo kesho,kwa hiyo unaweza kuvuta nuksi kwa kufanya mabaya au ukavuta bahati kwa kufanya mema,kumbuka sio lazima iwe kesho. Yawezekana mazuri ya babu yako wewe ndio unafaidi. Neno one day yes,lipo na ni kweli inategemea maandalizi ya hiyo one day yes yako unataka iwe positive au negative. Umekaa bila kuchakalika halafu unategemea one day yes ya vipi hiyo?

  Kwa wanao amini neno la Mungu ni kwamba,kuna waliojaliwa na mola,yaani wao ni ku-shine tu. Na kuna wanao lipia laana ya babu/baba zao pia.

  Nachangia hoja.
   
Loading...